Showing posts with label SIASA. Show all posts
Showing posts with label SIASA. Show all posts

Tuesday, November 13, 2012

Taswira Kutoka Mkutano Mkuu Wa CCM Dodoma.


 Wajumbe wa Mkutano Mkuu, Makamu wa Rais, Dk. Mohamed Gharib Bilal (kulia), Waziri Mkuu Mstaafu Cleopa Msuya na Rais Mstaafu wa Zanzibar, Dk. Salim Ahmed Salim, wakifuatilia matukio kwenye mkutano huo, ukumbini.
  Kamanda Asas wa UVCCM mkoa wa Iringa akitazama nakala ya UHURU alipotembelea banda la kampuni ya Uhuru Publications Ltd, wanaochapishaji wa magazeti ya Uhuru, Mzalendo na Burudani, kwenye viwanja vya Kizota
Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete na meza kuu, wakishiriki kucheza wimbo maalum ulimbwa na Vicky Kamata kabla ya kuanza mkutano huo
                        
                 PICHA ZOTE NA BASHIR NKOROMO
                                   

Friday, October 19, 2012

CHADEMA Wamnadi Mgombea Udiwani Shinyanga


 Dkt Slaa akimtambulisha mgombea udiwani wa chama chake wa kata ya Mwawaza,Shinyanga
 Dkt.Slaa akihutubia
 Mgombea udiwani wa CHADEMA
Ndg Wilfred Lwakatare,Mkurugenzi wa taifa wa ulinzi na usalama na mratibu wa kitaifa wa kampeni za udiwani

Huu ni mkutano wa kumnadi mgombea wa CDM wa udiwani katika kata ya Mwawaza ulioongozwa na Katibu Mkuu wa chama hicho Dr Wilbroad Slaa.Kumbuka huu ni mkutano tu katika mojawapo ya vijiji vya kata hiyo.


Monday, October 15, 2012

Makongoro Nyerere Aanguka Usiku Wa Nyerere



ASHINDWA KUTETEA KITI MARA, AMPA ANGALIZO MSHINDI, TARIMBA ATAMBA DAR, WAMBURA ATUPWA MAKONGORO Nyerere ameadhimisha vibaya kumbukumbu ya miaka 13 ya kifo cha baba yake, Mwalimu Julius Nyerere baada ya kuangushwa kwenye uchaguzi wa kuwania Uenyekiti wa CCM Mkoa wa Mara uliofanyika juzi na kumalizika usiku wa kuamkia jana. Jana ilikuwa ni siku ya maadhimisho ya kumbukumbu ya miaka 13 tangu kufariki kwa Baba wa Taifa, Mwalimu Nyerere yaliyofanyika kwenye Uwanja wa Kambarage, mjini Shinyanga yaliyokwenda sanjari na kuzimwa kwa Mwenge wa Uhuru. 

Katika uchaguzi huo wa Mkoa wa Mara, Makongoro aliyekuwa akitetea kiti hicho, alipata kura 422 na kuzidiwa na mpinzani wake wa karibu, Christopher Sanya aliyepata kura 481 huku tisa zikiharibika. Uchaguzi huo ilibidi urudiwe kwa kuwashindanisha wagombea wawili, kwani katika awamu ya kwanza wagombea wote hawakupata nusu ya kura kama kanuni za chama hicho zinavyotamka.

 Awali, katika nafasi hiyo wagombea walikuwa watatu. Katika awamu ya kwanza, Sanya alipata kura 469, Makongoro (402) na mgombea mwingine, Enock Chambiri aliyewahi kuwa Mwenyekiti wa CCM mkoani Mara alipata kura 144. Baada ya matokeo hayo ya awali, Chambiri aliondoka ukumbini hapo. Matokeo ya uchaguzi huo uliofanyika katika Ukumbi wa CCM Mkoa, yalitangazwa na Msimamizi Mkuu wa uchaguzi huo ambaye ni Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa, Nazir Karamagi. 

Akizungumza baada ya uchaguzi huo, Makongoro alisema kuwa anakubaliana na matokeo hayo na kumuasa mshindi kufanya kazi kwa mujibu wa katiba. Pia alimtaka mshindi huyo kuvunja makundi aliyosema yameshamiri ndani ya chama hicho.

 "Naomba uwe mwadilifu, Mkoa huu wa Mara ni mgumu sana kuufanyia kazi. Kazi ya uenyekiti siyo lelemama, hii ndiyo nafasi kubwa ambayo itatusaidia katika uchaguzi wa 2015." "Wewe ndiye kiongozi mkuu wa mkoa huu wa kupanga uongozi katika uchaguzi mkuu hivyo ukishindwa tutayumba, tunaomba utoe ushirikiano na ukemee hii dhambi ya kukata majina, kwani inaweza ikaingia kwenye ngazi ya Serikali za Mitaa."

 Waliochaguliwa katika nafasi ya Mjumbe wa Halmashauri ya Mkoa kupitia wilaya ni Josephat Seronga, Ester Nyarobi, Zuhura Makongoro, Jackson Waryoba, Josephat Kisusi na Felister Nyambaya. Wengine ni Grace Bunyinyiga, Thabita Idd, Abdallah Jumapili, Kananda Kananda, Mariam Mkono na Samson Gesase. Katika nafasi ya uenezi, Maximillian Ngesi amefanikiwa kutetea nafasi yake kama ilivyokuwa kwa Katibu wa Uchumi na Fedha, Marwa Mathayo.

                                                           MWANANCHI


Tuesday, October 9, 2012

Sabi alilia kuchezewa ‘rafu’ uchaguzi UVCCM Mara



Aliyekuwa mgombea nafasi ya Uenyekiti wa Umoja wa Vijana Mkoa wa Mara, Gabriel Mnasa Sabi (kulia) akifafanua jambo wakati alipozungumza na waandishi wa habari kuhusiana na uchaguzi wa Umoja wa Vijana (UVCCM) mkoa wa Mara leo katika mgahawa wa Hadees jijini Dar es salaam. Kushoto ni Sheweji Mkumbura ambaye ni rafiki yake. 

ALIYEKUWA mgombea nafasi ya Uenyekiti wa Umoja wa Vijana Mkoa wa Mara, Gabriel Mnasa Sabi ameuomba uongozi wa juu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) pamoja na Umoja wa Vijana makao makuu, kuingilia kati chaguzi za umoja ambazo zimetawaliwa na vitendo vya hujuma na rushwa.
Sabi ambaye juzi aishindwa kwa tofauti ya kura 14 dhidi ya Ditu Manko , amesema jijini Dar es salaam mara tu baada ya kutua leo asubuhi kuwa uchaguzi wao haukuwa huru na haki kwani matokeo yalijulikana kabla ya kupiga kura.
Alisema kuwa alitangaziwa matokeo hayo wakati wa kampeni kwa madai kuwa nafasi ya uenyekiti lazima itoke wilaya ya Tarime kutokana na nguvu ya kifedha.
“Hali hiyo ilinifanya kunyong’onyea hata kabla ya uchaguzi, hata hivyo nilipiga moyo konde na kuingia kwenye uchaguzi, matokeo yakawa yaleyale, nilishangazwa sana na wafuasi wangu wakaamua kutoendelea na uchaguzi huo,” alisema Sabi.
Alisema kuwa baada ya matokeo hayo, fujo zikaanza kwani wafuasi wake walichoka kuona vitendo vya uonevu vya waziwazi na kuongeza kuwa pamoja na wafuasi wake kutoka, uchaguzi huo uliendelea na kuhoji hao waliochaguliwa walipata kura hizo kwani sidhani kama idadi ya wapiga kura kwa mujibu wa katiba ilifikiwa.
“Kasoro hizi si za kuziacha kwani zinawagawa wanachama, ni lazima zikemewe  kwani bado kuna chaguzi nyingi ndani ya chama,” alisema.
Alifafanua kwa kusema kuwa hana tatizo na uongozi wa juu wa CCM kutokana na sera madhubuti zenye kuleta maendeleo ya nchi, ila kilio chake ni viongozi wanaokipaka matope chama hasa wa ngazi ya chini.

Sunday, October 7, 2012

MWANAHABARI WA GAZETI LA MWANANCHI IRINGA TUMAINI MSOWOYA AWA MWENYEKITI WA UV CCM MKOA WA IRINGA




Mwandishi  wa habari  wa gazeti la Mwananchi mkoa  wa Iringa Bi.Tumain Msowoya  (pichani ) ameibuka  na ushindi  wa kishindo katika uchaguzi wa nafisi ya uenyekiti wa umoja  wa vijana  wa chama cha mapinduzi (UVCCM) mkoa  wa Iringa kwa kuwagalagaza wanaume  wawili  waliojitokeza akiwemo mwanahabari mwenzake Abba Ngilangwa wa radio Nuru Fm pamoja na mwalimu wa shule ya sekondari ya  wazazi wa jumuiya ya wazazi wa chama cha mapinduzi sekondari ya Mwembetogwa Bw Ramadhan Baraza .

Msowoya  ambaye amepata  kura zaidi ya 100  wapinzani  wake  wameambulia mabawa kwa  kupata kura chini ya 4o kila mmoja .vuta  subira matokeo yanakuja  dakika  chache kuanzia  sasa.

Saturday, October 6, 2012

John Mnyika:Taarifa ya ufafanuzi kuhusu utafutaji wa mafuta na gesi asili nchini iliyotolewa na Wizara ya Nishati na Madini tarehe 21 Septemba 2012 ifutwe kwa kuwa italinda ufisadi na kukwaza utetezi wa rasilimali za taifa:



  Mbunge wa Ubungo(CHADEMA)John Mnyika
---
Waziri wa Nishati na Madini Prof. Sospeter Muhongo afute taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu wa wizara hiyo kuwa lengo la agizo lake la kupitiwa kwa mikataba yote 26 ya utafutaji mafuta na gesi asili ni “kuhakikisha kwamba endapo kuna mapungufu katika mikataba hiyo, mapungufu hayo yasijirudie tena katika mikataba mipya ya baadaye” kwa kuwa ikiachwa ilivyo italinda ufisadi na kukwaza utetezi wa rasilimali za taifa.

Ufafanuzi uliotolewa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini unatoa mwanya kwa mikataba mibovu kulindwa wakati ambapo kuna madai tuliyotoa toka mwaka 2011 kwamba baadhi ya mikataba hiyo imeingiwa kifisadi na mwaka huu wa 2012 zimeibuka tuhuma za vigogo wa serikali kuingiziwa fedha kifisadi katika akaunti zao za nchini Uswisi na makampuni ya nje ya utafutaji mafuta na gesi asili.

Tafsiri ya ufafanuzi huo uliotolewa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini ni kwamba hata kama mikataba iliyopo ina mapungufu yasiyozingatia maslahi ya taifa, matokeo ya mapitio hayo hayatarekebisha mikataba iliyopo bali mikataba ya baadaye.

Taarifa hiyo ya Katibu Mkuu wa Wizara ni ya kurudi nyuma tofauti na kauli za awali za Waziri Muhongo zilizokubaliana na madai yetu ya toka mwaka 2011 ndani na nje ya bunge ikiwemo kwa nafasi yangu ya Waziri Kivuli wa Nishati na Madini ya kutaka mikataba yote ipitiwe upya, isiyozingatia maslahi ya taifa ivunjwe au ifanyiwe marekebisho makubwa na mikataba mipya isiingiwe mpaka kwanza kuwepo sera na sheria bora zenye kulinda uchumi na usalama wa nchi.

Itakumbukwa kwamba tarehe 15 Septemba 2012 wakati wa uzinduzi wa Bodi Mpya ya Wakurugenzi ya Shirika la Maendeleo la Petroli Tanzania (TPDC) Waziri wa Nishati na Madini aliagiza bodi hiyo kuipitia mikataba yote 26 ya utafutaji mafuta na gesi asili ili kujiridhisha endapo maslahi ya taifa yalizingatiwa.

Agizo hilo la Waziri limeendana na mapendekezo niliyotoa mwaka 2011 ya kutaka mapitio ya mikataba yote ya mafuta na gesi asili ambapo pamoja na mambo mengine niliitaka Serikali kupitia Wizara ya Nishati na Madini na taasisi zake kuacha kuingia mikataba ya muda mrefu  ya utafutaji wa mafuta na gesi asili katika maeneo mbalimbali nchini yenye mianya ya kuhujumu uchumi wa nchi na haki za wananchi masuala ambayo yalipingwa na Waziri wa zamani.
Kutokana na kutozingatiwa kwa mapendekezo hayo tarehe 21 Februari 2012 nilitoa kauli ya kutaka Waziri wa Nishati na Madini wa wakati huo William Ngeleja kuwajibishwa kwa kuendelea kuruhusu kusainiwa kwa mikataba bila maagizo ya msingi kuzingatiwa na kueleza kwa umma sababu za serikali kuendeleza usiri na kuacha kufanya mapitio ya mikataba mibovu iliyopo.
Nilitoa kauli hiyo baada ya tarehe 20 Februari 2012 Serikali kusaini mkataba wa kutafuta mafuta na gesi asili na kampuni ya Swala katika maeneo ya Kilosa Mkoani Morogoro na Pangani Mkoani Tanga na Januari 2012 Serikali kuweka saini mikataba na kampuni za kimataifa za Petrobras Tanzania Ltd, Heritage Rukwa Tanzania Ltd na Motherland Industies Ltd na Oktoba 2011 Serikali kusaini mikataba mingine na kampuni za Ndovu Resource na Heritage Oil za Uingereza kwa ajili ya utafutaji wa nishati ya mafuta na gesi katika kisiwa cha Songosongo na Ziwa Rukwa huku nchi ikiwa haina mwelekeo sahihi wa sera, sheria, mipango na usimamizi wa sekta hizo nyeti kwa usalama na uchumi wa nchi na maisha ya wananchi kwa ujumla.

Waziri Muhongo na Katibu Mkuu Maswi wanapaswa kuendelea kuonyesha kwa maneno na matendo tofauti yao na viongozi waliowatangulia katika Wizara ya Nishati na Madini Waziri Ngeleja na Katibu Mkuu Jairo kwa kutoa ufafanuzi wa ziada na kuchukua hatua zaidi vinginevyo taarifa kwa vyombo vya habari iliyotolewa tarehe 21 Septemba 2012 itakuwa ni mwendelezo wa kulinda udhaifu wa kimfumo uliojikita katika Wizara hiyo na serikali kwa ujumla.
Ni vizuri Waziri na Katibu Mkuu wakaendelea kuzingatia ushauri niliwapa bungeni kwamba sehemu kubwa matatizo katika sekta za nishati na madini yamechangiwa na sababu za kibinadamu za kutowajibika ipasavyo kisera, kimaamuzi, kiusimamizi na kiutendaji kwa viongozi wa kiserikali wenye dhamana na watendaji wengine na hivyo kusababisha ugumu wa maisha kwa wananchi na kuathiri uchumi wa nchi; hivyo nguvu zielekezwe katika kurekebisha hali hiyo.

Imetolewa tarehe 4 Oktoba 2012 na:
John Mnyika (Mb)
Waziri Kivuli wa Nishati na Madini

ICISO KUANZA MIDAHALO JIMBONI KWA PROF MSOLLA LEO



Mbunge wa  Kilolo Prof Peter Msolla ambaye leo anaanza Mdahalo huo
Mbunge wa jimbo la Isimani ambaye pia ni waziri wa nchi ofisi ya  waziri mkuu Sera na uratibu wa bunge Mhe Wiliam Lukuvi ambaye atafuata kwa mdahalo huo tarehe 10 mwezi huu
Mbunge wa jimbo la Iringa mjini Mch Peter Msigwa (chadema) bado zamu yake

Mbunge wa  jimbo la Kalenga ambaye ni waziri wa fedha na uchumi Dkt Wiliam Mgimwa bado muda  wake

WABUNGE mkoani Iringa kukutanishwa na wapiga kura wao katika mdahalo wa kutathimini haki na fursa sawa kwa jinsi zote majimboni mwao.

Katika mdahalo huo ulioandaliwa na mtandao  wa mashirika yasiyo ya kiserikali katika mkoa wa Iringa(ICISO -UMBRELLA) kwa kushirikiana na mitandao ya AZAKI  ya halmashauri ya manispaa ya Iringa (IMUCISO) na Iringa Vijijini (IRUNGO) na wilaya ya Kilolo (KIDINGOU) ,Mbunge wa jimbo la Kilolo Prof. Peter Msolla kuanza Leo katika jimbo lake.

Akizungumza  na waandishi wa habari jana ofisini kwake katibu mtendaji wa ICISO-UMBRELLA Raphael Mtitu alisema kuwa tayari wabunge wa majimbo yote wamepewa barua za ushiriki wao katika midahalo hiyo.


Mititu alisema mbali ya Kuanza Leo katika jimbo la Kilolo midahalo Kama hiyo itafanyika jimbo la Kalenga linaloongozwa na waziri wa fedha na uchumi Dkt Wiliam Mgimwa, jimbo la Iringa mjini linaloongozwa na mchungaji Peter Msigwa na jimbo la Isimani linaloongozwa na waziri wa nchi ofisi ya waziri mkuu sera ya uratibu wa bunge Wiliam Lukuvi

Alisema kuwa   lengo la mdahalo huo ni kuongeza uewelewa kwa wananchi kuhusu umuhimu wa haki na fursa sawa kwa jinsia katika mkoa wa iringa na wilaya zake kwa ujumla."lengo ni kuwapa wanajamii uelewa juu ya haki za kijinsia na kupunguza matukio ya ubaguzi na unyanyasaji wa kijinsia katika ngazi mbalimbali katika kaya,familia na jamii.

Aidha mdahalo hiyo itakayofanyika tarehe tofauti na ukianza na jimbo la kilolo tarehe 6 mwezi huu katika shule ya sekondari image na kufuatia jimbo la ismani katika ukumbi wa christopher itunundu tarehe 10 ni muendelezo wa mradi wa kuimarisha mahusiano kati ya wananchi na wawakilishi wao ambao unatelekezwa kwa njia ya midahalo.
walengwa wa midahalo hiyo ni wananchi wote na wanaombwa wajitokeze kwa wingi kwa lengo la kupata elimu hiyo ya fursa sawa kwa jinsia zote.
MWISHO

ISMAIL JUSSA: NIMEWASILISHA BARUA YA KUJIUZULU NAFASI YANGU CUF.


Jana asubuhi nimewasilisha kwa Mwenyekiti wa Chama Taifa, Mheshimiwa Profesa Ibrahim Lipumba barua ya kuomba kujiuzulu nafasi ya Naibu Katibu Mkuu wa Chama Cha Wananchi (CUF) kwa upande wa Zanzibar, uamuzi ambao nimeomba uanze kutekelezwa rasmi tarehe 10 Oktoba, 2012.
Nimechukua uamuzi huu baada ya kuzungumza na kushauriana na viongozi wangu wa juu wa Chama ambao ni Mwenyekiti, Profesa Lipumba, Makamu Mwenyekiti Mheshimiwa Machano Khamis Ali na Katibu Mkuu Maalim Seif Sharif Hamad takriban miezi miwili iliyopita. Nawashukuru baada ya kunitaka niwape muda wa kulitafakari walinikubalia lakini wakaniomba nibakie hadi tutakapokamilisha baadhi ya shughuli muhimu za Chama katika kipindi hichi.
Sababu kubwa zilizonisukuma kukiomba Chama kiniruhusu niachie nafasi hii ni kutokana na muda mrefu sasa kuhisi kwamba majukumu niliyo nayo ya kuwa msimamizi mkuu wa utendaji wa Chama kwa upande wa Zanzibar na wakati huo huo kuwa Mjumbe wa Baraza la Wawakilishi wa jimbo la Mji Mkongwe hakunipi fursa ya kujifaragua na kutumikia nafasi zote mbili kwa ufanisi unaotakiwa. Nataka kuona kazi ya kuibana Serikali ndani na nje ya Baraza ili iwajibike zaidi kwa wananchi inaimarika zaidi.

Sambamba na sababu hiyo ni kwamba nimekusudia kutumia muda mwingi zaidi kutoa mchango mkubwa zaidi katika harakati za wananchi wa Zanzibar zinazoendelea za kuhakikisha kuwa Zanzibar inarejesha mamlaka yake kamili kitaifa na kimataifa itakayofuatiwa na kuwepo kwa Muungano wa Mkataba kati yake na Tanganyika yenye mamlaka kamili kitaifa na kimataifa.
Harakati zinazoendelea Zanzibar kwa njia za amani na za kidemokrasia kwa kutumia mchakato wa Katiba Mpya zinahitaji kuungwa mkono na kupewa msukumo wa dhati na Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi waliochaguliwa na wananchi wa Zanzibar kwenda kusimamia maslahi yao na ya nchi yao. Nimetafakari na kuona kwamba nikiwa sina majukumu mengine ya kiutendaji nitakuwa na muda kutosha wa kulifanya hili mimi na Wawakilishi wenzangu tunaotoka CUF na CCM, vyama viwili vya siasa vilivyomo Barazani.

Nafurahi kwamba leo nimetimiza azma yangu hiyo. Pamoja na uamuzi huu, naendelea kubaki kuwa Mjumbe wa Baraza Kuu la Uongozi la Taifa na Mjumbe wa Mkutano Mkuu wa Taifa. Nawahakikishia viongozi na wanachama wenzangu wa CUF kwamba tutaendelea kushirikiana pamoja katika shughuli nyengine zote za kisiasa za Chama na kwa pamoja tutafanya kazi kuyatimiza malengo tuliyojiwekea. Naahidi kumpa ushirikiano kikamilifu mwanachama yeyote atakayeteuliwa kujaza nafasi ninayoiwacha.
HAKI SAWA KWA WOTE
ISMAIL JUSSA
Zanzibar

Sunday, September 30, 2012

Katibu Mkuu wa CHADEMA Dr Willbroad Slaa amepokea wanachama wapya kutoka familia ya mwanasiasa mkongwe nchini na Waziri wa Nchi 0fisi ya Rais(Mahusiano na Uratibu) Mh Stephen Wasira,Estha Wasira na Lilian Wasira.



Katibu Mkuu wa CHADEMA, Dk. Willibrod Slaa, akiwakabidhi kadi ya uwanachama wa chama hicho kwa Lilian Wassira na ndugu yake Esther, baada kujiunga na chama hicho. Lilian na Esther ni watoto wa George Wassira Kaka wa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Uhusiano) Stephen Wassira.Picha na Michael Matemanga-Mwananchi)
-----
Baada ya kamanda Makongoro Wasira kujiunga na M4C siku chache zilizopita, leo tena watoto wengine wa Wasira wamejiunga na M4C na kukitupia virago Chama cha Baba yao CCM. Waliojiunga leo katika Makao makuu ya Chadema na kukabidhiwa kadi na Katibu Mkuu wa Chadema Dr Slaa ni kamanda Ester Wasira na Lilian Wasira.

Lilian Wasira (Mwanasheria, graduate wa TUDARCO):(i) Alielezea furaha yake kwa kujiunga na chama makini na chenye kuleta matumaini mapya kwa Mtanzania

(ii) Aliwaasa vijana, akina mama na wazee wajiandikishe kwa wingi nafasi itakapotokea na 2015 wakamalizie kazi ya ukombozi kwa kuipigia CHADEMA kura

(iii) Amewaasa Watanzania kuacha kulalamikia maovu ya CCM na kuchukua hatua ya kuiweka CCM pembeni na kuleta Chadema kama chama mbadala. Alisema hakuna sababu ya kuwa na mfumo wa vyama vingi kama watanzania hawathubutu kuchagua chama mbadala na badala yake kuendelea kuichagua CCM na kulalamika kila siku kuwa CCM imeshindwa kuongoza nchi.

(iv) Kwamba CCM imekuwa madarakani kwa zaidi ya miaka 50 hivyo ni wakati sasa wa kuiweka pembeni na kuingiza chama kipya, mawazo mapya na kujenga mfumo mpya wa uongozi. Hakuna kitu CCM imeshindwa kufanya kwa miaka 50 inaweza kufanya kwa miaka 5 au 10 ijayo.

(v) Anasema ana imani na sera za chadema kuwa ndizo zitatukomboa. Amewapa moyo viongozi wa CHADEMA wasitishwe na vitisho na mauaji yanayofanywa na dola na kusema yupo tayari kwa M4C na yupo tayari kulipuliwa kama walivyolipuliwa wanachadema wengine na kuuawa kama itambidi afanye hivyo.

(vi) Kwamba CHADEMA ni Chama kinachosubiri kuingia Ikulu isipokuwa tu watu wajiandikishe, wapige kura na walinde kura.

(vii) Naye alimalizia kwa kusema, “Kwa msaada wa Mungu Tanzania mpya inakuja.” Dkt. Slaa alitiwa moyo sana na ujasiri ulioonyeshwa na vijana hawa pamoja na maneno ya kizalendo waliyoongea na akawakarisha kwenye uwanja wa mapambano ya M4C.

Saturday, September 29, 2012

Nassari Asikiliza Kero Za Wananchi Arumeru



 Nassari MB akiwa na Jackson Makalla (chini kushoto mwenye Kombati) walipokuwa Ngarenanyuki jana
Nassari akihutubia na kusikiliza maswali ya wananchi

KUSHINDA UMEYA NA NAIBU MEYA, NAO UCHAGUZI WA ILEMELA WAAHIRISHWA KUTOKANA NA PINGAMIZI LA MATATA



Meya wa jiji la Mwanza Stanslaus Mabula kupitia CCM (katikati) akiwa na Naibu Meya John Minja (CCM) wakitambulishwa na Mkurugenzi wa jiji la Mwanza Wilson Kabwe baada ya kutangazwa washindi  kufuatia uchaguzi uliofanyika leo katika ukumbi wa halmashauri ya jiji la Mwanza.


 Kikao cha Uchaguzi cha Halmashauri ya Manispaa ya Nyamagana jijini Mwanza kimemchagua diwani wa Kata ya Mkolani Mh. Stanslaus Mabula wa CCM kuwa Meya wa jiji hilo mara baada ya kumshinda mshindani wake Charles Chinchibela wa CHADEMA aliyepata kura 8 ile hali Mabula akipata kura 11.

Ni picha ya pamoja Meya Mabula, mkuu wa wilaya ya Nyamagana Baraka Konisaga(katikati) na Naibu meya John Minja wakiwa katika ofisi ya Mstahiki Meya 


Diwani wa kata ya Kitangili Henry Matata (aliyevuliwa uanachama CHADEMA) akisalimiana na diwani mwenzake Marietha Chenyenge huku mkononi akiwa na hati ya Mahakama ya Hakimu Mkazi Mwanza iliyozuia kufanyika wa Meya na Naibu Meya mpaka pale kesi iliyofunguliwa na diwani huyo kupinga CHADEMA kuteua wagombea wa nafasi hizo, kwa chati  mbunge wa jimbo la Ilemela Highness Kiwia (aliyesimama) akiwa bize na simu yake ya kiganjani, kabla ya kuahirishwa kwa uchaguzi wa Manispaa ya Ilemela.
Ikumbukwe kuwa leo kulikuwa na chaguzi mbili za Ma- Meya na Ma- Naibu wake wa Halmashauri ya jiji la Mwanza (Nyamagana) na Manispaa ya Ilemela, baada ya uchaguzi wa Nyamagana kumalizika na wajumbe wake kuondoka ukumbini  ili kuwapisha wajumbe wa wilaya ya Ilemela, nao waliketi katika ukumbi wa uchaguzi wakisubiri kushiriki uchaguzi wa kuteuwa Meya na Naibu Meya wao ambapo uchaguzi huo haukufanyika kufuatia diwani wa kata ya Kitangili kufungua kesi katika mahakama ya Hakimu Mkazi Mwanza kupinga kuvuliwa uanachama, kupinga kuenguliwa katika mchakato wa kuwania nafasi ya Meya hadi hapo uamuzi wa kesi yake utakapo tolewa, kutokana na kuwa na hati ya Mahakama inayomruhusu aidha kuruhusiwa kushiriki kupitia chama chake cha zamani (CHADEMA) au chama chake kutofanya uteuzi wa wagombea.

Aliyekuwa mgombea nafasi ya Meya wa Manispaa ya Ilemela Abubakar Kapera diwani kata ya Nyamanoro (kulia)   na kushoto kwake ni diwani wa kata ya Kirumba Danny Kahungu aliyekuwa akiwania nafasi ya Naibu Meya Ilemela  wote kutoka CHADEMA ndani ya ukumbi wa uchaguzi kabla ya uchaguzi wao kuahirishwa kutokana na zuio.

Kutoka kushoto ni aliyekuwa Meya wa jiji la Mwanza kabla ya jiji hilo kugawanywa kuwa Manispaa na Halmashauri, diwani Manyarere akiwa na diwani Rose Brown na diwani wa viti maalum ndani ya ukumbi wa Uchaguzi kutafuta Meya na Naibu wake Nyamagana.

Madiwani wa CCM wilaya ya ilemela kabla ya uchaguzi wao kuahirishwa.

Madiwani wa CHADEMA wakiwa na mbunge wao  wa wilaya ya Ilemela Highness Kiwia (katikati) wakisubiri taratibu za uchaguzi ambao hata hivyo haukufanyika.

Meya wa jiji la Mwanza (wa3kutoka kushoto) Naibu Meya (wa kwanza kushoto) wakiwa pamoja na Madiwani wa CCM wakimsikiliza mbunge wa viti maalum Maria Hewa (wa pili kutoka kulia) aliyekuwa akisema "Chama kimerudisha heshima yake katika jiji la Mwanza"
Picha na habari na Libeneke la 
http://gsengo.blogspot.com/

Waliotoswa CCM Wafichua Siri



FILIKUNJOMBE ADAI YEYE, MKONO, LUGOLA WALIPONZWA NA PINDA, NAPE ATAKA WASIORIDHIKA WAKATE RUFAA, WASOMI WAPONGEZA 

SIKU moja baada ya Halmashauri Kuu ya CCM (Nec), kutangaza majina ya wagombea, baadhi ya vigogo walioachwa kwenye uteuzi huo wameeleza ya moyoni, huku Mbunge wa Ludewa, Deo Filikunjombe akisema anaamini ametoswa kwa sababu alitia saini ya kutokuwa na imani na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda. Katika Bunge la 10 lililoketi Aprili mwaka huu, baadhi ya Wabunge wa CCM akiwamo Filikunjombe, Mbunge wa Musoma Vijijini, Nimrod Mkono na Mbunge wa Mwibara, Kangi Lugola, waliunga mkono hoja ya kutokuwa na imani na Pinda iliyokuwa imeanzishwa bungeni na Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe wa Chadema. 

Wabunge hao wa chama tawala, waliungana na wenzao wa upinzani kutaka kupiga kura za kutokuwa na imani na Pinda kutokana na kile kilichoelezwa kuwa ameshindwa kuisimamia Serikali kwa kuwawajibisha mawaziri wazembe. Hata hivyo, mpango huo haukufanikiwa baada ya Spika wa Bunge Anne Makinda kueleza kuwa haukufuata taratibu zinazotakiwa.
 

 Filikunjombe alipotakiwa jana kuzungumzia kuenguliwa kwake kwenye kinyang'anyiro cha uchaguzi wa ndani ya chama, alisema anaamini yeye na wenzake hao wa CCM, wametoswa kwa sababu ya kushiriki mpango wa kumng'oa Waziri Mkuu Pinda. Hata hivyo, alisema amelazimika kukubali hali hiyo na kupokea matokeo, kwa kuwa hatua yake ya kusaini kitabu hicho ilitokana na nia njema kutaka Waziri Mkuu ajiuzulu ili mambo fulani muhimu katika jamii yafanyike. 

Filikunjombe alibainisha kuwa alisaini kitabu hicho cha kutokuwa na imani na Pinda akiwa na akili timamu na alikuwa anajua kinachoweza kutokea kutokana na hatua yake hiyo. "Nimesaini kitabu kile kwa nia njema, nikiwa na akili timamu na sijutii uamuzi wangu huo, ila siwezi kuwasemea Kigwangalla (Khamis mbunge wa Nzega) na Bashe (Hussein). Lakini sisi watatu (yeye, Lugola, Mkono) tumeenguliwa kwa sababu hiyo (ya kutokuwa na imani na Pinda)." Aliendelea: "Nashangaa leo naonekana adui wa chama wakati nilikuwa nakinusuru na kusema kweli adui wa CCM ni Wabunge wa chama hicho ambao hawakusaini kitabu hicho cha kutokuwa na imani na Waziri Mkuu, " alisema Filikunjombe. 

Mkono Mbunge wa Musomo Vijijini, Nimrod Mkono alisema kutoswa kwake ni uamuzi wa watu aliowaita wenye chama. "Walikata jina langu nikakata rufaa, likarudishwa Dodoma, lakini walipokutana wakaona sifai. Wakaamua kunifukuza sasa hapo mimi nifanye nini?" alihoji Mkono. Mkono alisema huu ni utaratibu wa chama chao cha CCM ambao umewapa baadhi ya watu haki ya kuwafukuza wengine bila kuwapa fursa ya kujitetea. "Kama ilivyotokea kwangu wamekaa na kuona Mkono hafai, fukuza basi wakafanya hivyo na hiyo haijalishi kama nilisaini kutokuwa na imani na Waziri Mkuu au la.

 Suala la msingi ni kuwa Mkono amefukuzwa na atarudi kama ilivyokuwa kwa mwana mpotevu." alisema bila kufafanua. Kigwangalla Mbunge wa Nzega, Dk Hamis Kigwangalla alisema anaheshimu uamuzi wa vikao vilivyokaa na kufikia uamuzi uliochukuliwa na kwamba, ataendelea kuwa mwanachama na kukitumikia chama pamoja na wananchi kwa nguvu zote bila kinyongo. “Nitaendelea kuheshimu vikao vya chama changu na kuwa mwanachama hai ingawa sijajua wametumia vigezo gani kuteua majina hayo,” alisema Dk Kigwangalla. Bashe Kwa upande wake Bashe alisema kilichotokea ni uamuzi wa chama na vikao halali vilivyokaa na kuchukua uamuazi huo. 

“Sijui kwa nini jina langu halikupitishwa, lakini nitaendela kuwa mwanachama na kuwatumikia wananchi wenzangu wa Nzega,” alisema Bashe. Katika kuhakikisha hilo, Bashe alisema leo anakwenda Nzega kupeleka mifuko ya saruji tani 18 kwa ajili ya ujenzi wa ofisi za kata za chama hicho wilayani humo. 

Nape ajibu Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye alitaka makada waliotoswa na wenye kinyongo wawasilishe malalamiko yao CCM kwa maandishi badala ya kulalamika nje ya utaratibu."Wathibitishe kwa maandishi nasi chama tutajua la kufanya, kwani wabunge hao hawakuingia katika vikao vilivyotoa maamuzi sasa nashangaa kusikia katika vikao tuliwajadili na hoja iliyowaondoa ni hiyo," alisema Nape. Maoni ya wasomi Wakizungumzia uteuzi huo wasomi na wanasiasa walitoa maoni tofauti huku baadhi wakisema chama kinatakiwa kuwa na sera na mtizamo wa kuliletea maendeleo taifa bila kujali kama chama kinaongozwa na wazee au vijana.

 Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Dk Benson Bana alisema uamuzi huo wa CCM umeonyesha kuwa, ndani ya chama hicho hakuna aliye juu kuliko mwenzake. “Wapo waliosema wakitoswa patachimbika, lakini wametoswa na hapajachimbika, uamuzi wa kuwatosa watu wa aina hii utarejesha nidhamu ndani ya chama hicho licha ya kuwa kazi bado ni kubwa,” alisema Dk Bana. Profesa Gaudence Mpangala alisema vijana kupewa nafasi kubwa ya kugombea nafasi mbalimbali ndani ya CCM, hakuna maana kuwa sera na mtizamo wa chama hicho utabadilika. 

 “Kuwa na wanachama au wagombea wenye umri wa wastani(vijana) sio kigezo cha chama kufanya vyema kwa sababu hawawezi kubadili sera na mtizamo wa chama husika,” alisema Mpangala. Dk Kitila Mkumbo alisema kuingiza vijana wengi katika mpambano huo ni hatua ya ukomavu wa kisiasa kwa kuwa chama hicho awali hakikuwa na utaratibu mzuri wa kuwapa nafasi ya uongozi vijana. “Awali Chadema ndio kilionekana chama kinachowapa nafasi zaidi vijana, lakini kwa hatua hii ya CCM ni nzuri, sasa tunasubiri utendaji wao kama utakuwa na manufaa kwa taifa,” alisema Mkumbo. 

 Bashiru Ally alisema kama kigezo cha kuweka vijana wengi kitazingatia msimamo, fikra na ufanisi katika utendaji kazi wao basi taifa lina kila sababu ya kuunga mkono hatua hiyo.Alisema kwa kuwa vijana ndio chachu ya maendeleo kwa mataifa mbalimbali duniani, hatua ya CCM kuwapa nafasi vijana ni nzuri kama wakiifanya kazi hiyo kwa manufaa ya taifa kwanza. 

Habari hii imeandikwa na Ibrahim Yamola, Fidelis Butahe, Elizabeth Edward na Joseph Zablon,Mwananchi .

Friday, September 28, 2012

Chadema:Mtoto wa Waziri Steven Wassira Ajiunga na Chadema



Viongozi wa Tawi la Chadema Houston wamkabidhi Kadi ya Chadema Makongoro Wassira.Picha na Habari na CHADEMA
---
Katika watu wanaikashifu Chadema na kuwa na maneno ya maudhi ni Waziri Wassira. Sasa kwa kuonyesha kuwa M4C haina msamaha hata kwa familia yake mtoto wake aishie USA aitwae Makongoro Wassira amejiunga na M4C.

Akizungumza wakati anakabidhiwa kadi alisema yeye ni wa kwanza tu kujiunga M4C lakini ndugu zake wote wapo mbioni kujiunga na anadhani baba yake pekee ndie atabaki CCM.  
 

BREKING NYUUUUZZZZZ: CCM YAIMWAGA CHADEMA KATIKA UMEYA JIJINI MWANZA



HABARI ZIMETUFIKIA PUNDE KWAMBA CHAMA CHA MAPINDUZI (CCM)  KIMEKIBWAGA CHAMA CHA DEMOKRASIA NA MAENDELEO (CHADEMA) BAADA YA MGOMBEA WAKE WA KITI CHA UMEYA KATIKA JIJI HILO KUJIZOLEA KURA 11 DHIDI YA 8 YA MPINZANI WAKE KWENYE UCHAGUZI ULIOFANYIKA NA KUMALIZIKA MUDA MFUPI ULIOPITA

. HABARI ZAIDI ZAJA PUNDE

Zitto: Ubunge sasa basi




 Na: Frank Sanga na Anthony Kayanda, Kigoma, MWANANCHI.

MBUNGE wa Kigoma Kaskazini (Chadema), Zitto Kabwe amesema hana mpango wa kugombea ubunge mwaka 2015 badala yake anajipanga kuwania urais. Zitto alisema hayo jana alipozungumza na wananchi katika mjadala ulioandaliwa na asasi ya kiraia ya Meza ya Duara uliokuwa unafanyika maeneo ya Soko la Mwanga, mjini Kigoma. Zaidi ya watu 200, ambao walihudhuria katika mjadala huo wa wazi walimuuliza maswali mbalimbali mbunge huyo, huku mmoja akigusia kuhusu tetesi za mara kwamba Zitto anataka kugombea urais katika uchaguzi ujao.

 “Nimefanya kazi kubwa katika kazi yangu ya ubunge, nimeleta mabadiliko mengi kuanzia bungeni mpaka jimboni. Nadhani inatosha na hata nikiongezewa miaka mingine sitaweza kufanya yale yaliyonishinda katika kipindi cha miaka kumi. “Kama Mungu ataniweka mpaka mwaka 2015, sitagombea ubunge tena kwa sababu kazi niliyofanya inatosha. Natangaza rasmi kuwa nitagombea urais kupitia chama changu cha Chadema, bila kusababisha msuguano wowote na sitaki kuingia katika historia ya kurudisha nyuma harakati za upinzani kushika dola,” alisema Zitto.

 “Nataka kuleta changamoto mpya, nitawaeleza watu wa chama changu nia hiyo na nitatoa hoja za msingi. Hata kama sitapata ridhaa yao, lakini huo ndio msimamo wangu. “Iwapo chama kikiona sistahili au sifai, nitakubaliana na uamuzi huo. Watu wengi wanadhani urais ni cheo, hawajui kuwa ni nafasi ambayo inakufanya ufanye vitu ambavyo ni vikubwa na vya maendeleo kwa wananchi.” Atangaza kugombea urais Katika hatua nyingine Zitto alisema ana mpango wa kuwania urais kupitia Chadema katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015. “Kwanza nataka niwahakikishia watu wa Kigoma msiwe wanyonge…mna uwezo wa kutoa rais wa nchi hii,” Zitto alianza kujibu swali hilo na kuendelea. 

Hata hivyo Zitto alipoulizwa baadaye na Mwananchi kuwa mwaka 2015 atakuwa na miaka 39, hivyo kukosa sifa ya kugombea urais kwa mujibu wa katiba alijibu; “Nadhani nina uwezo wa kuwa rais, sidhani kama Katiba inaweza kumzuia mtu mwenye uwezo asigombee na ndio maana ninaamini kuwa kipengele cha kuwa na miaka 40 kitabadilishwa katika katiba mpya.”

 “Nchi za Kidemokrasia lazima vyama vibadilishane utawala wa kuongoza nchi kama ilivyo katika nchi za Ghana na Zambia. Tanzania inatakiwa kuiga mfano wa nchi hizo,” alisema Zitto Katika kukazia hilo, Zitto alisema anashangazwa na umaskini uliopo Tanzania wakati mwaka 1976 uchumi wake ulikuwa sawa na nchi ya Malaysia, lakini mpaka kufikia mwaka 2001, Malaysia ilipunguza idadi ya watu wanaoishi chini ya dola moja kutoka asilimia 56 mpaka kufikia asilimia tatu huku Tanzania ikipunguza kutoka 51 mpaka 46. Katika hatua nyingine, Zitto alikana kuwa, Chadema ni chama cha udini, ukanda, ukabila ila akasisitiza kuwa ni chama cha kitaifa. 

 “Ndugu zangu naomba mnielewe, Chadema si chama cha ukabila, ukanda wala udini bali ni chama cha kitaifa. Hizo ni propaganda za wapinzani wetu,” alisema Zitto baada ya kuulizwa na mmoja wa washiriki kuhusu tuhuma za chama hicho kuwa cha Kikanda.

 “CCM imewahi kudai CUF ni chama cha Waislamu, na sasa wanasema Chadema ni chama cha Wakristo, sasa wao CCM ni chama cha wapagani au cha watu gani?” Alihoji Zitto. Alisema ili kuthibitisha kuwa Chadema si chama cha Kikanda, matokeo ya urais wa mwaka 2010, Dk Wilbroad Slaa aliongoza dhidi ya wagombea urais wengine kwa kupata kura nyingi katika Jimbo la Manyovu mkoani Kigoma na hivyo kufanya kupata asilimia nyingi kuliko sehemu yoyote Tanzania. 

 Chanzo: http://www.mwananchi.co.tz/habari

Wednesday, September 26, 2012

CHADEMA Arusha Wamefanya Mkutano Wao Leo



 Godbless Lema akihutubia

 Joshua Nassari (Mb) akihutubia
Ally Bananga,kada aliyejitoa CCM Arusha

Friday, September 21, 2012

TUME YA UCHAGUZI TAIFA YAVIONYA VYAMA VYA SIASA DHIDI YA LUGHA CHAFU.

Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Mh. Jaji Mstaasfu Damiani Lubuva wakati wa ufunguzi wa mkutano wa Tume na Viongozi wa Vyama vya Siasa nchini. 
Mkurugenzi Jullius Mallaba akizungumzia maandalizi ya uchaguzi mdogo wa madiwani kata 29 Tanzania.
Wadau waliohudhuria kikao hicho. 
Picha Juu na Chini ni Baadhi ya wadau walioshiriki kikao hicho.
Na Datus Boniface.
Mwenyekiti wa tume ya taifa ya uchaguzi  (NEMC ) Jaji mstaafu Mh . Damian Lubuva amevionya vyama vya siasa kuwa, hawatavumilia tabia ya baadhi ya wagombea wa vyama vya siasa kutoa lugha chafu za kashfa dhidi ya wagombea wengine au vyama kipindi cha kampeni.
Onyo hilo amelitoa jijini Dar es salaam, katika mkutano wa tume na viongozi wa vyama vya siasa.
 “tume haitavumilia tabia hiyo ambayo si ya kiistarabu, inachochea vurugu, wadau wanapoona wamedhalilishwa kwa lugha ya kashfa wapeleke malalamiko mara moja kwa kamati ya maadili katika kata husika”alisema
Awali, kaimu katibu mkuu wa chama cha U.D.P, Isaac Cheyo, alisema daftari la wapiga kura ni bovu kutokana na kuchanganya taarifa za wapiga kura kwa kata tofauti, hali iliyonyima fursa wananchi kupiga kura.
Naye, mwenyekiti wa chama cha N.l.D, Dk. Emmanuel Makaidi alibainisha utendaji mbovu wa tume ya uchaguzi akidai kwa kipindi cha mwaka jana imekuwa na kesi 47 za malalamiko juu ya chaguzi.
Alisema NEC kwa kipindi hicho imefanya madudu zaidi ambayo ilikuwa ikisimamiwa na viongozi waliopita akiwemo Rajabu Kiravu.
Hata hivyo aliongeza kuwa siyo jambo la kushangaza watendaji hao kuachia ngazi kwa pamoja kutokana na mdudu hayo waliyoyafanya.
Alienda mbali zaidi na kusema, kwa kipindi hicho NEC ilifanya madudu kwa kuchakachua uchaguzi mzima ikiwa ni pamoja kubadilisha kwa nembo za vyama vya siasa bila taarifa.
Alihoji kuwa ikiwa NEC inanyoshewa kidole na kila madau iweje uhalali wake wa kuendelea kufanyakazi nchini.