Showing posts with label Warembo. Show all posts
Showing posts with label Warembo. Show all posts

Tuesday, May 13, 2014

Avunja Ndoa yake kwa kutamani maisha ya Wema Sepetu...




Kuiga  ni  kawaida  kwa  wengi.Wapo  walioiga  mambo  fulani  na   hatimaye  wakafanikiwa, na  pia  wapo  walioiga  vitu  flani  wakaharibikiwa.Huyu  aliiga  na  akaharibu  kila  kitu...
Ni  msanii  wa  siku  nyingi  katika  fani.Alitamba  zaidi  akiwa  Kaole, na  hata  mwanzoni  mwa  ujio  wa  filamu  za  Kanumba  alizidi  tu  kashaini....
Kiasili  ni  mweusi  japo  siku  hizi  kuna  weupe  fulani  katika  ngozi  yake  nyororo.Ana  sura  nzuri  yenye  mvuto,umbo  aslia  la  kibantu,meno  yake  meupe  yamepambwa  na  mwanya  mdogo  na  kufanya  iwe  fahari  kumuona  akitabasamu...
Hana  kashfa  ya  kuvaa  nguo  fupi  sana  ila  aliwahi  kukumbwa  na  skendo  kubwa  zaidi.Mkumbuke  vizuri.Mrefu  wa  wastani,anajua  kutembea,anaongea  kwa  mapozi  huku  akipenda  kulamba  papi  ya  midomo  yake. Umemjua???....Hapana, siyo  huyo...!!

Huyu  ni  mpole  kiasili  na  anapendwa  sana  na  mama  yake.Katika  maigizo  ana  uwezo  wa  kukufanya  uamini  unachoangalia  ni  kitu  halisi.Japo  huwezi  kumtaja, ila  ndani  ya  wasanii  kumi  anapaswa  kuwamo...


Na  ingawa  mvuto  wake  umepungua  kiasi,ila  bado  mrembo  sana.Lakini  wakati  anaigiza  Kaole  alikuwa  mrembo  zaidi.Kwa  uzuri  wake ,  alivuma  na  kila  habari  inayohusu  mwanaume  maarufu  na  mwenye  pesa


Habari  ya  kutakiwa  na  kila  mwanaume , wenye  rangi  na    vipato  tofauti  zilisikika  kila  kona.Baadhi  alitoka  nao  na  wengine  haikuwa  bahati  yao....


Toka  kitambo  almanusura  aolewe, ila  ni  miaka  ya  juzi juzi  ndipo  aliolewa.Uzuri  wake  si  wa  kutafuta, kila  mwenye  macho  na  ngozi  ya  kuhisi  atautambua....


Mbali  na  majanga  yote  aliyopitia  katika  maisha  yake,mengine  yakibaki  kumchafua  na  watu  kudhani  hawezi  kuolewa  na  mwanaume  yeyote  kabla  ya  ile  bahati  ya  mtende  akaolewa; yeye  aliamua  kuachana  na  ndoa  yake  kwa  kuona  aishi  katika  umaarufu  wake....


Mara  kadhaa  alikuwa  akiwaambia marafiki  zake  kuwa, mwenye  hadhi  na  anayetakiwa  kuishi  kama  Wema  Sepetu  sio  Wema  bali  ni  yeye  na  wakongwe wengine  waliosotea  sanaa  na  kuipigania  kama  roho  zao  na  kuilinda  kama  mboni  ya  jicho  lao.....


Akaona  ndoa  sio  mahala  pake,bila  sababu  za  msngi  akaamua  kumwambia  mumewe  watengane....Japo  haikuwa  rahisi ,lakini  walitengana!!



Cha  kufurahisha  ni  kwamba  bado  Wema  anaishi  kama  Wema  na  bado  yeye  haishi  kama  Wema  Sepetu  na  ndoa  haipo  tena...Umemjua  ninayemzungumzia?

Tuesday, October 9, 2012

Washiriki Redds Miss Tanzania 2012 wakaribishwa Monduli kwa shangwe


Dada wa Mbunge wa jimbo la Monduli na Waziri Mkuu mstaafu Kalaine Lowasa akiwavisha warembo wanaoshiriki shindano la Redds Miss Tanzania 2011, mgolole wa kimasai wakati warembo hao walipoandaliwa tafrija maalum ya kuwakaribisha katika mji wa Monduli.Kushoto ni Mke wa Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge w Monduli, Regina Lowasa.Warembo hao wapo Kanda ya Kaskazini kutembelea vivutio mbalimbali vya Utalii vilivyopo katika mikoa hiyo
Dada wa Mbunge wa jimbo la Monduli na Waziri Mkuu mstaafu Kalaine Lowasa akiwavisha warembo wanaoshiriki shindano la Redds Miss Tanzania 2011, mgolole wa kimasai wakati warembo hao walipoandaliwa tafrija maalum ya kuwakaribisha katika mji wa Monduli.Kushoto ni Mke wa Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge w Monduli, Regina Lowasa.Warembo hao wapo Kanda ya Kaskazini kutembelea vivutio mbalimbali vya Utalii vilivyopo katika mikoa hiyo
Dada wa Mbunge wa jimbo la Monduli na Waziri Mkuu mstaafu Kalaine Lowasa akiwavisha warembo wanaoshiriki shindano la Redds Miss Tanzania 2011, mgolole wa kimasai wakati warembo hao walipoandaliwa tafrija maalum ya kuwakaribisha katika mji wa Monduli.Kushoto ni Mke wa Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge w Monduli, Regina Lowasa.Warembo hao wapo Kanda ya Kaskazini kutembelea vivutio mbalimbali vya Utalii vilivyopo katika mikoa hiyo
 Robert Lowasa nae alivishwa Mgolole kutokana na mchango wake mkubwa alioutoa kufanikisha warembo hao kufika mji i
 Warembo wakiwa wamekaa na mavazi yao yimasaai
 Baadhi ya wadau waliohudhuria tafrija hiyo
 Nao walikuwepo
 Viongozi wa kamati ya Miss Tanzania
 Picha ya pamoja
Mke wa Waziri Mkuu Mstaafu, Regina Lowasa akicheza mziki wa Kwaito na Warembo wanaoshiriki shindano la Redds  Miss Tanzania 2012, wakati wa tafrija maalum ya kuwakaribisha warembo hao katika mji wa Monduli jana mkoani Arusha. Warembo wa Redds  Miss Tanzania wapo Kanda ya Kaskazini kutembelea vivutio mbalimbali vya Utalii vilivyopo katika mikoa hiyo. 
Mke wa Waziri Mkuu Mstaafu, Regina Lowasa na mtoto wake Robert Lowasa 'Bob" wakicheza mziki wa Kwaito na Warembo wanaoshiriki shindano la Redds  Miss Tanzania 2012, wakati wa tafrija maalum ya kuwakaribisha warembo hao katika mji wa Monduli jana mkoani Arusha. Warembo wa Redds  Miss Tanzania wapo Kanda ya Kaskazini kutembelea vivutio mbalimbali vya Utalii vilivyopo katika mikoa hiyo. 

Saturday, October 6, 2012

MRITHI WA REDD'S MISS TANZANIA SALHA ISRAEL KUPATIKANA KATIKA HAWA




 
BRIGITTE ALFRED ni Mshiriki namba 26 akitokea Kitongoji cha Sinza na anawakilisha Kanda ya Kinondoni jijini Dar es Salaam.
ANANDE RAPHAEL ni mshiriki namba 11 akitokea Mkoa wa Kilimanjaro akiwakilisha Kanda ya Kaskazini.
 
BABYLOVE KALALA ni Mshiriki na 9 akitokea mkoa wa Kagera, akiwakilisha Kanda ya Ziwa.
 
CAREN  ELIAS mshiriki 23 anatokea Mbeya anawakilisha Nyanda za Juu Kusini
 
CATHERINE MASUMBIGANA ni mshiriki na 15 akitokea Kitongoji cha Chang'ombe anawakilisha kanda uya Temeke jijini Dar es Salaam.
 
DIANA HUSSEIN amepata namba ya ushirtiki 20, akitokea kitongoji cha Dar Indian Ocean, akiiwakilisha Kanda ya Kinondoni jijini Dar es Salaam.
  
FINA REVOCATUS anavaa namba 12 akitoka Chuo cha Usimamizi wa Fedha IFM, akiwakilisha Kanda ya Vyuo Vya Elimu ya Juu.
BELINDA MBOGO  ni mshiriki na 29 akitoka mkoa wa Dodoma akiwaklilisha Kanda ya Kati
 
EDDA SYLVESTER amepata namba 22, akitoka Kigamboni na anaiwakilisha Kanda ya Temeke jijini Dar es Salaam.
 
ELIZABETH DIAMOND anavalia namba 2 akitokea mkoa wa singida, akiwakilisha kanda ya Kati.
 
FATMA RAMADHANI nambari yake 25 akitoka chuo cha Uandishi wa habari Arusha ASJ, anawakilisha Kanda ya Elimu ya Juu.
FLAVIAN MAEDA anavalia namba 10 akitokea kitongoji cha Kurasini mwakilishi wa kanda ya Temeke jijini Dar es Salaam.
Kutoka Kahama- Shinyanga ni HAPPINESS RWEYEMAMU ananamba 8 anawakilisha Kanda ya Ziwa.
HAPPYNESS DANIEL namba yake ya ushiriki ni 19 anatokea jiji la Mwanza akiwakilisha Kanda ya Ziwa.
IRINE VEDA anatokea Lindi na kupata namba 16 akiuwakilisha Kanda ya Mashariki
JESCA HAULE ni mshiriki namba 14, akitoka kitongoji cha Chang'ombe anawakilisha Kanda ya Temeke jijini Dar es Salaam.
JOYCE BALUHI anatoka Morogoroakiwa ni mshiriki 13 anawakilisha Kanda ya Mashariki.
JOYCE BALUHI ni mshiriki 13 akitokea kitongoji cha Dar Indian Ocean, akiiwakilisha Kanda ya Kinondoni jijini Dar es Salaam.
Huyu ni LIGHTNESS MICHAEL anavalia 5, akitokea Dodoma akiwakilisha Kanda ya Kati.
Kutoka mkoa wa Manyara ni LUCY STEPHANO mshiriki namba 4 akiwakilisha Kanda ya Kaskazini.
MAGDALENA ROY mshiriki namba 6, kutoka Kitongoji cha Dar City Centre akiwakilisha Kanda ya Ilala.
Anaitwa Mary Chizi akitokea kitongoji cha Ukonga, anavalia namba 17, akiwakilisha Kanda ya Ilala jijini Dar es Salaam.
Yeye ni MAGDALENA ROY mshiriki nambari 18, kutyoka mkoa wa Iringa akiwakilisha Kanda ya Nyanda za Juu Kusini.
Jinalake ni NOELA MICHAEL yupo na namba 27, anashikilia taji la kitongoji cha Tabata na ni mwakilishi tegemeo wa Kanda ya Ilala.
Rose Lucas ana namba 28 akitokea Mkoa wa Pwani akiwakilisha Kanda ya Mashariki
VENCY EDWARD  ni mshiriki nambari 7, akitoka Mkoa wa Rukwa akiwakilisha Kanda ya Nyanda za Juu Kusini
WARID FRANK huyu ni mshiriki namba 30 akitokea Arusha ana kuiwakilisha  Kanda ya Kaskazini.
Anaitwa ZUWENA NASIB akiwa ni mwakilishi pekee wa chuo Kikuu Huria OUT.
 
Mkufunzi Mkuu, anaitwa Irine Karugaba alikuwa mmopja wa washiriki wa Miss Tanzania 2011.