Wednesday, July 4, 2012

TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI - SEKRETARIETI YA AJIRA KATIKA UTUMISHI WA UMMA

 

 

 

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
                       
OFISI YA RAIS

SEKRETARIETI YA AJIRA KATIKA UTUMISHI WA
                                    
UMMA

 

 

 

 

 

 

 

Kumb. Na EA.7/96/01/B/183                                                                   29 Juni, 2012

 

TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI

 

Katibu wa Sekretarieti ya Ajira Katika Utumishi wa Umma anakaribisha maombi ya Watanzania wenye sifa na uwezo wa kujaza nafasi za kazi 569 mbalimbali kwa Waajiri (Taasisi za Umma) kama ifuatavyo:

Katibu Mkuu Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Wizara ya Maji, Wizara ya
Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, Katibu Tawala Mkoa wa Arusha, Iringa, Kigoma,
Mwanza (Geita), Mara, Morogoro, Rukwa, Ruvuma, Tanga, Halmashauri ya Jiji la
Mwanza, Halmashauri ya Manispaa ya Sumbawanga, Lindi, Halmashauri ya Wilaya ya
Chato, Chamwino, Chunya, Kahama, Kishapu, Kiteto, Kongwa, Kyela, Magu, Maswa,
Mbozi, Meatu, Monduli, Mbinga, Mbulu, Mpanda, Msalala, Mpwapwa, Rufiji, Rungwe,
Simanjiro, Shinyanga, Songea, Tandahimba, Ukerewe na Halmashauri ya Mji Njombe.

 

Aidha,   tangazo   hili   linapatikana   kwenye   tovuti   zifuatazo:   www.ajira.go.tz,
www.utumishi.go.tz na www.pmoralg.go.tz

 

NB: MASHARITI YA JUMLA KWA KAZI ZOTE.

i.Waombaji wote wawe ni Raia wa Tanzania wasiozidi umri wa miaka 45. ii.Waombaji wote waambatishe cheti cha kuzaliwa.

iii.WAOMBAJI KAZI KWA NAFASI ZA AFISA MTENDAJI WA KATA DARAJA LA II,
       
AFISA MTENDAJI WA KATA DARAJA LA III,  AFISA MTENDAJI WA KIJIJI DARAJA
       
LA II,  AFISA MTENDAJI WA KIJIJI DARAJA LA III NA AFISA MTENDAJI MTAA
       
DARAJA LA III  AMBAO WALIOMBA NAFASI KAMA HIZO KATIKA TANGAZO LA
       
TAREHE 25 MEI 2012 HAWAPASWI TENA KUOMBA NAFASI HIZI
 
iv.Waombaji ambao tayari ni watumishi wa Umma na wamejipatia sifa za kuingilia
       
katika kada tofauti na walizonazo, wapitishe barua zao za maombi ya nafasi za
        kazi kwa waajiri wao na Waajiri wajiridhishe ipasavyo.

1


 

 

 

 

 

 

v.Nafasi ya kazi inayoombwa iandikwe katika kichwa cha habari cha barua na juu
      
ya bahasha, kutozingatiwa hili kutasababisha maombi ya kazi kuwa batili.

vi.Waombaji  waambatishe  maelezo  binafsi  yanayojitosheleza                                                                                                                    (Detailed  C.V)  yenye

anwani na namba za simu za kuaminika pamoja na majina ya wadhamini (referees) watatu wa kuaminika.

vii.Maombi   yote   yaambatane na vyeti vya taaluma, maelezo, nakala za vyeti vya kidato
         cha nne na kidato cha sita kwawale waliofikia kiwango hicho na vyeti vya kuhitimu
        
mafunzo mbalimbali kwa kuzingatia sifa za kazi husika. Viambatanisho hivyo vibanwe
        
sawa sawa kuondoa uwezekano wa kudondoka/kupotea.

-   Postgraduate/Degree/Advanced Diploma/Diploma/Certificates.

-   Cheti cha mtihani wa kidato cha IV na VI

-   Computer Certificate

-   Vyeti vya kitaaluma (Professional certificates from respective boards)

-   Picha moja "Passport size" ya hivi karibuni iandikwe jina kwa nyuma.

viii."Testmonials", "Provisional Results", "Statement of results", hati matokeo za
         
kidato   cha   nne   na   sita (FORM   IV   AND   FORM   VI   RESULTS   SLIPS)

HAVITAKUBALIWA.

ix.Waombaji waliostaafishwa katika Utumishi wa Umma hawaruhusiwi kuomba isipokuwa
        kama wanakibali cha Katibu Mkuu Kiongozi.

x.Waombaji kazi ambao tayari ni waajiriwa katika nafasi za kuingilia walioko katika
        utumishi wa umma wasiombe  na wanatakiwa kuzingatia  maelekezo  yaliyo
       
katika Waraka Na CAC. 45/257/01/D/140 wa tarehe 30 Novemba 2010.
 
xi.Uwasilishaji wa taarifa na sifa za kugushi zitapelekea wahusika watachukuliwa
       
hatua za kisheria.

xii.WAAJIRI   WOTE   WALIOPO   NJE   YA   DAR   ES   SALAAM   WANAOMBWA
        
KUSAMBAZA  MATANGAZO  HAYA  KWENYE  MBAO  ZA  MATANGAZO  NA
        
MAENEO MENGINE.

xiii.Mwisho wa kupokea barua za maombi ni tarehe 14 Julai, 2012

xiv.Aidha, uwasilishaji wa barua kwa mkono katika ofisi za Sekretarieti ya ajira
         
HAURUHUSIWI.

xv.Maombi yanaweza kuandikwa kwa Lugha ya Kiswahili au Kiingereza na yatumwe
        
kupitia posta kwa anuani ifuatayo.

 

Katibu,                                             AU                  Secretary,

Sekretariati ya Ajira katika                                  Public Service Recruitment

Utumishi wa Umma,                                             Secretariat,

SLP.63100,                                                             P.O.Box 63100

Dar es Salaam.                                                      Dar es Salaam

 

 

 

 

 

 

2


 

 

 

 

 

 

Nafasi hizo (569) za kazi mbalimbali katika Utumishi wa Umma mbalimbali ni kama ifuatavyo:

1.0   MHAIDROJIOLOJIA DARAJA LA II (HYDROGEOLOGISTS GRADE II ) -
         NAFASI 16

Nafasi hizi ni kwa ajili ya Katibu Mkuu Wizara ya Maji na Katibu Tawala Mkoa wa Geita

1.1   MAJUKUMU YA KAZI

·   Kukusanya  Takwimu, kutafiti pamoja na kutayarisha  Taarifa za  Kihadrolojia
     
zenye maelezo fasaha ya kitaalaamu

·   Kujenga (installation ) na kukarabati vifaa vya utafiti wa maji chini ya Ardhi na
     
kukarabati vituo vya kuratibu rasilimali za maji chini ya ardhi

·    Kusimamia uchimbaji wa visima vya maji na kuhakiki uwezo wa kisima kutoa
     
maji. (Pumping Test)

·   Kukusanya sampuli za maji na udongo kwa ajili ya kufanya uchunguzi wa
     
kimaabara.

·   Kutathimini    (monitoring )rasilimali za maji chini ya ardhi kwenye sehemu za

kidakio cha maji ( sub catchment)

 

1.2   SIFA ZA MWOMBAJI

·   Kuajiriwa wenye Shahada ya Jiolojia au jiofizikia na haidrolojia kutoka vyuo vikuu
     
vinavyotambuliwa na Serikali.

·   Wawe na ujuzi wa kutumia Kompyuta.

 

1.3   MSHAHARA

Kwa kuzingatia Ngazi za mishahara ya Serikali yaani TGS E.

 

2.0   MHANDISI DARAJA LA II - MAJI (WATER ENGINEER GRADE II) - NAFASI 3

Nafasi hizi ni kwa ajili ya Katibu Tawala Mkoa wa Tanga, Geita, Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga

 

2.1   MAJUKUMU YA KAZI

·   Atafanya kazi chini ya uangalizi wa Mhandisi aliyesajiliwa (Professional engineer)
     
na bodi ya usajili ya Wahandisi ili kupata uzoefu unaotakiwa.

·   Kufanya ukaguzi wa Miradi ya Maji

·   Kufuatilia utekezaji wa Sheria, Kanuni za Maji

·   Kutayarisha bajeti ya mwaka ya Maji

·   Kusimamia na kuratibu kazi za Maji zinazotolewa na makandarasi

 

2.2   SIFA ZA MWOMBAJI

·   Kuajiriwa mwenye Shahada ya Uhandisi wa Rasilimali za Maji kutoka vyuo vikuu
      vinavyotambuliwa na Serikali. Wawe na ujuzi wa kutumia kompyuta.

 

2.3   MSHAHARA

Kwa kuzingatia Ngazi za mishahara ya Serikali yaani TGS E kwa mwezi.

3


 

 

 

 

 

 

 

3.0   MHIFADHI WANYAMAPORI II - NAFASI 13 (IMERUDIWA)

Nafasi hizi ni kwa ajili ya Wizara ya Maliasili na Utalii

3.1   MAJUKUMU YA KAZI

·    Kufanya doria ndani na nje ya maeneo ya hifadhi au mbuga za wanyama

·    Kusimamia utekelezaji wa utaratibu wa uwindaji na utalii

·    Kulinda binadamu na mali zake dhidi ya wanyama hatari.

·    Kukusanya na kulinda nyara za Serikali

·    Kufanya usafi na ulinzi

·    Kubeba na kutunza vifaa vya doria

·    Kudhibiti uingiaji na utokaji wa watu na mali kwenye hifadhi

·    Kutunza vielelezo vya ushahidi vya nyara

·    Kudhibiti wanyamapori waharibifu

·    Kukagua vibali na leseni za matumizi ya wanyamapori.

·    Kudhibiti mioto mikali kwenye mapori.

 

3.2   SIFA ZA MWOMBAJI

·    Kidato cha IV au Kidato cha VI

·    Wenye Stashahada/Astashahada ya Uhifadhi wa Wanyamapori kutoka Chuo cha

Usimamizi wa Wanyamapori Mweka  au Chuo kingine kinachotambuliwa na Serikali.

·    Waliopitia  mafunzo  ya  nidhamu  na  ukakamavu  yanayotolewa  na  vyuo  vya

wanyamapori watapewa kipaumbele.  Wale watakaopata nafasi lakini hawana
mafunzo  hayo,  watapewa  mafunzo  husika  kama  sehemu  ya  mafunzo  ya
"Induction".

 

3.3   MSHAHARA

Kwa kuzingatia viwango vya Serikali ngazi ya Mshahara TGS.B na C kwa mwezi.

4.0   MKUFUNZI MSAIDIZI DARAJA LA I (ASSISTANT TUTOR GRADE I) - NAFASI
         35

Nafasi hizi ni kwa ajili ya Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto

4.1   MAJUKUMU YA KAZI

·   Kufundisha masomo ya fani mbalimbali zinazofundishwa katika vyuo

·   Kuandika mtiririko na mpangilio wa masomo

·   Kusimamia masomo ya vitendo

·   Kuwapima wanachuo wakati wa mazoezi na kwenye mitihani

 

4.2   SIFA ZA MWOMBAJI

·   Kuajiriwa wahitimu wa Kidato cha Nne/Sita waliofuzu mafunzo ya Stashahada
     
kutoka Chuo Cha Maendeleo ya Jamii (Rungemba au Buhare) au Chuo kingine
      kinavyotambuliwa na Seikali
AU

 

 

4


 

 

 

 

 

 

·   Kuajiriwa wahitimu wa Kidato cha Nne/Sita waliofuzu mafunzo ya Stashahada
     
kutoka Chuo Cha Ufundi kinachotambuliwa na Seikali katika fani zifuatazo:

i.      Uashi (Masonry) - Nafasi 5

ii.      Useremala (Carpentry) - Nafasi 6

iii.      Uunganishaji Vyuma (Welding) - Nafasi 4

iv.      Ushonaji (Sewing)- Nafasi 5

v.      Ufundi Magari (Motor Vehicle Mechanics) - Nafasi 5

vi.      Umeme (Electrical) - Nafasi 5

vii.      Kompyuta (Computer) - Nafasi 5

 

4.3   MSHAHARA

Kwa kuzingatia viwango vya Serikali yaani ngazi ya Mshahara TGS B. kwa mwezi.

 

5.0   AFISA MTENDAJI WA KATA DARAJA LA II (WARD EXECUTIVE OFFICER
         GRADE II) - NAFASI 55

Nafasi hizi ni kwa ajili ya Halmashauri ya Wilaya ya Kiteto, Maswa, Mbulu, Meatu, Rungwe na Shinyanga

5.1   MAJUKUMU YA KAZI

·    Atakuwa Mtendaji Mkuu wa Kata na kiungo cha Uongozi kwa Idara zote katika

kata na atashughulikia masuala yote ya kata

·    Atakuwa Mhamasishaji mkuu wa Umma katika mikakati mbalimbal.i ya uzalishaji,

mali, kuondoa njaa na Umasikini.

·    Atakuwa ni Katibu wa kamati ya maendeleo ya kata.

·    Ataratibu na kusimamia upangaji wa shughuli za maendeleo ya kata, vijiji na

Mtaa.

·    Atatafsiri sera na kusimamia utekelezaji wa sheria ndogondogo katika Kata

yake.Atamsaidia Mkurugenzi Kuratibu na kusimamia shughuli za Uchaguzi katika

Kata.

·    Kumsaidia na kumwakilisha Mkurugenzi katika kusimamia maendeleo ya eneo

lake.

·    Kusimamia utendaji kazi wa wataalamu na watendaji wengine katikangazi ya

Kata.

·    Kuratibu na kuandaa taarifa za utekelezaji na kuziwasilisha kwa mkurugenzi na

nakala kwa Katibu Tarafa.

·    Atakuwa mwenyekiti katika vikao vinavyowahusisha wataalamu na watendaji wa

vjiji, na NGO'S katika kata yake.

·    Atakuwa Msimamizi na mratibu wa takwimu zote zinazokusanywa katika vijiji,

vitongoji, na kata yake.

 

5.2   SIFA ZA MWOMBAJI

·    Kuajiriwa wenye Shahada ya Sanaa yenye mwelekeo wa Sayansi ya Jamii

(Social  Sciences)  Utawala,    (Public  Administration  and  Local  Gorvernment),

 

5


 

 

 

 

 

 

Sheria   au   Sifa   nyingine   inayolingana   na   hizo   kutoka   Chuo   chochote kinachotambuliwa na Serikali.

 

5.3   MSHAHARA

Kwa kuzingatia viwango vya Serikali yaani ngazi ya Mshahara TGS D. kwa mwezi.

6.0   AFISA MTENDAJI WA KATA DARAJA LA III (WARD EXECUTIVE OFFICER
         GRADE III) - NAFASI 68

Nafasi hizi ni kwa ajili ya Halmshauri ya Wilaya ya Chunya, Kongwa, Kyela, Mbozi, Msalala, Mvomero, Shinyanga na Kishapu

6.1   MAJUKUMU YA KAZI

·    Atakuwa Mtendaji Mkuu wa Kata na kiungo cha Uongozi kwa Idara zote katika

kata na atashughulikia masuala yote ya kata

·    Atakuwa Mhamasishaji mkuu wa Umma katika mikakati mbalimbali ya uzalishaji,

mali, kuondoa njaa na Umasikini.

·    Atakuwa ni Katibu wa kamati ya maendeleo ya kata.

·    Ataratibu na kusimamia upangaji wa shughuli za maendeleo ya kata, vijiji na

vitongoji.

·    Atatafsiri sera na kusimamia utekelezaji wa sheria ndogondogo katika Kata

yake.Atamsaidia Mkurugenzi Kuratibuna kusimamia shughuli za Uchaguzi katika

Kata.

·    Kumsaidia na kumwakilisha Mkurugenzi katika kusimamia maendeleo ya eneo

lake.

·    Kusimamia utendaji kazi wa wataalamu na watendaji wengine katika ngazi ya

Kata.

·    Kuratibu na kuandaa taarifa za utekelezaji na kuziwasilisha kwa mkurugenzi na

nakala kwa Katibu Tarafa.

·    Atakuwa mwenyekiti katika vikao vinavyowahusisha wataalamu na watendaji wa

vjiji, na NGO'S katika kata yake.

·    Atakuwa Msimamizi na mratibu wa takwimu zote zinazokusanywa katika vijiji,

vitongoji, na kata yake.

 

6.2   SIFA ZA MWOMBAJI

·    Kuajiriwa  waliohitimu  kidato  cha  nne  au  sita  na  kuhudhuria  mafunzo  ya

Stashahada yenye mwelekeo wa Sayansi ya Jamii (Social Sciences) Utawala,
(Public Administration and Local Gorvernment), Stashahada ya Sheria au Sifa
nyingine  inayolingana  na  hizo  kutoka  Chuo  chochote  kinachotambuliwa  na
Serikali.

 

6.3   MSHAHARA

Kwa kuzingatia viwango vya Serikali ngazi ya Mshahara TGS C kwa mwezi.

 

 

6


 

 

 

 

 

 

7.0   AFISA MTENDAJI WA KIJIJI DARAJA LA II (VILLAGE EXECUTIVE OFFICER
         GRADE II) - NAFASI 25

Nafasi hizi ni kwa ajili ya Halmashauri ya Wilaya ya Mpwapwa, Maswa na Rombo.

7.1   MAJUKUMU YA KAZI

·    Atakuwa Mtendaji na Mshauri Mkuu wa Serikali ya Kijiji na Kamati zake katika

Mipango ya Maendeleo ya kijamii na Utekelezaji wa Mipango ya Maendeleo.

·    Atakuwa Afisa Mhasibu wa Serikali ya Kijiji na atasimamia  mapato na matumizi

ya  Serikali ya kijiji

·    Atakuwa Mlinzi wa Amani na Msimamizi wa Utawala Bora katika Kijiji.

·    Ataratibu na kusimamia upangaji wa utekelezaji wa Mipango ya Maendeleo ya

kijiji

·    Atakuwa Katibu wa Kamati ya Halmashauri ya Kijiji.

·    Atatafsiri Sera, ataratibu na kusimamia utekelezaji wa Sheria ndogondogo za

Halmashauri ya Kijiji.

·    Ataratibu  na  kuandaa  taarifa  ya  utekelezaji  wa  kazi  katika  eneo  lake  na

kuziwasilisha kwenye Halmashauri ya Kijiji na baadae kwenye kata .

·    Ataongoza  vikao  vya  maendeleo  ya  Kijiji  vitavyowahusisha  wananchi  na

wataalamu waliopo kwenye eneo lake.

·    Atahamasisha  wananchi  katika  kampeni  za  kuondoa  njaa,  umasikini,  na

kuongeza uzalishaji mali.

·    Atasimamia matumizi bora ya Nguvu kazi.

·    Atakuwa Kiongozi wa Wakuu wa Vitengo vya Kitaalamu Katika Kijiji.

·    Atasimamia ukusanyaji wa kumbukumbu za walipa kodi, wataalamu mbalimbali

na NGO waliopo katika kijiji.

 

7.2   SIFA ZA MWOMBAJI

·    Kuajiriwa wenye elimu ya kidato cha IV na VI  waliohitimu Stashahada ya

kawaida  katika  fani  yoyote  yenye  mwelekeo  wa  Sayansi  ya  Jamii                                                                                                        (Social

Sciences) Utawala, (Public Administration and Local Gorvernment), Stashahada ya  Sheria  au  Sifa  nyingine  inayolingana  na  hizo  kutoka  Chuo  chochote kinachotambuliwa na Serikali.

 

7.3   MSHAHARA

Kwa kuzingatia viwango vya Serikali ngazi ya Mshahara TGS C kwa mwezi.

 

8.0   AFISA MTENDAJI WA KIJIJI DARAJA LA III (VILLAGE EXECUTIVE OFFICER
        
GRADE III) - NAFASI 181

Nafasi hizi ni kwa ajili ya Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu, Kyela, Magu, Mbozi, Mbulu, Msalala, Meatu, Mvomero na Rungwe

8.1   MAJUKUMU YA KAZI

·   Atakuwa Mtendaji na Mshauri Mkuu wa Serikali ya Kijiji na Kamati zake katika
     
Mipango ya Maendeleo ya kijamii na Utekelezaji wa Mipango ya Maendeleo.

 

7


 

 

 

 

 

·   Atakuwa Afisa Mhasibu wa Serikali ya Kijiji na atasimamia  mapato na matumizi
      ya  Serikali ya kijiji

·   Atakuwa Mlinzi wa Amani na Msimamizi wa Utawala Bora katika Kijiji.

·   Ataratibu na kusimamia upangaji wa utekelezaji wa Mipango ya Maendeleo ya
     
kijiji

·   Atakuwa Katibu wa Kamati ya Halmashauri ya Kijiji.

·   Atatafsiri Sera, ataratibu na kusimamia utekelezaji wa Sheria ndogondogo za
     
Halmashauri ya Kijiji.

·   Ataratibu  na  kuandaa  taarifa  ya  utekelezaji  wa  kazi  katika  eneo  lake  na
     
kuziwasilisha kwenye Halmashauri ya Kijiji na baadae kwenye kata.

·   Ataongoza  vikao  vya  maendeleo  ya  Kijiji  vitavyowahusisha  wananchi  na
     
wataalamu waliopo kwenye eneo lake.

·   Atahamasisha  wananchi  katika  kampeni  za  kuondoa  njaa,  umasikini,  na
     
kuongeza uzalishaji mali.

·   Atasimamia matumizi bora ya Nguvu kazi.

·   Atakuwa Kiongozi wa Wakuu wa Vitengo vya Kitaalamu Katika Kijiji.

·   Atasimamia ukusanyaji wa kumbukumbu za walipa kodi, wataalamu mbalimbali
      na NGO waliopo katika kijiji.

 

8.2   SIFA ZA MWOMBAJI

Kuajiriwa  wenye  Elimu  ya  Kidato  cha  Nne  au  cha  sita  waliohitimu  Astashahada
(Certificate) katika Fani yoyote yenye mwelekeo wa Sayansi ya Jamii (Social Sciences)
Utawala, (Public Administration and Local Gorvernment), Astashahada ya Sheria au
Sifa nyingine inayolingana na hizo kutoka Chuo chochote kinachotambuliwa na Serikali.

8.3   MSHAHARA

Kwa kuzingatia viwango vya Serikali yaani ngazi ya Mshahara TGS B kwa mwezi.

9.0   AFISA MTENDAJI MTAA DARAJA LA III  (MTAA EXECUTIVE OFFICER
         GRADE III) - NAFASI 8

Nafasi hizi ni kwa ajili ya Halmashauri ya Wilaya ya Kahama na Shinyanga.

9.1    MAJUKUMU YA KAZI

·   Atakuwa Mtendaji na Mshauri Mkuu wa Serikali ya Mtaa na Kamati zake katika
     
Mipango ya Maendeleo ya kijamii na Utekelezaji wa Mipango ya Maendeleo.

·   Atakuwa Afisa Mhasibu wa Serikali ya Mtaa na atasimamia  mapato na matumizi
     
ya  Serikali ya Mtaa

·   Atakuwa Mlinzi wa Amani na Msimamizi wa Utawala Bora katika Mtaa

·   Ataratibu na kusimamia upangaji wa utekelezaji wa Mipango ya Maendeleo ya
     
Mtaa

·   Atakuwa Katibu wa Kamati ya Halmashauri ya Mtaa.

·   Atatafsiri Sera, ataratibu na kusimamia utekelezaji wa Sheria ndogondogo za
     
Halmashauri ya Mtaa

 

 

8


 

 

 

 

 

·   Ataratibu  na  kuandaa  taarifa  ya  utekelezaji  wa  kazi  katika  eneo  lake  na
     
kuziwasilisha kwenye Halimashauri ya Mtaa na baadae kwenye Kata.

·   Ataongoza  vikao  vya  maendeleo  ya  Mtaa  vitavyowahusisha  wananchi  na
     
wataalamu waliopo kwenye eneo lake.

·   Atahamasisha  wananchi  katika  kampeni  za  kuondoa  njaa,  umasikini,  na
     
kuongeza uzalishaji mali.

·   Atasimamia matumizi bora ya Nguvu kazi.

·   Atakuwa Kiongozi wa Wakuu wa Vitengo vya Kitaalamu Katika Mtaa.

·   Atasimamia ukusanyaji wa kumbukumbu za walipa kodi, wataalamu mbalimbali
      na NGO waliopo katika Mtaa.

 

9.2   SIFA ZA MWOMBAJI

·   Kuajiriwa wenye Elimu ya Kidato cha Nne au cha sita waliohitimu Astashahada
     
(Diploma) katika Fani yoyote yenye mwelekeo wa Sayansi ya Jamii (Social
     
Sciences) Utawala, (Public Administration and Local Gorvernment), Atashahada
      ya  Sheria  au  Sifa  nyingine  inayolingana  na  hizo  kutoka  Chuo  chochote
     
kinachotambuliwa na Serikali.

 

9.3    MSHAHARA

Kwa kuzingatia viwango vya Serikali ngazi ya Mshahara TGS B kwa mwezi.

 

10.0 SEKTA YA MIFUGO

10.1   DAKTARI WA MIFUGO DARAJA LA II (VETERINARY OFFICER GRADE II ) -
           
NAFASI 4

Nafasi hizi ni kwa ajili ya Halmashauri ya Wilaya ya Chato

10.1.1 MAJUKUMU YA KAZI

·   Kutoa huduma  za Afya ya Mifugo

·   Kufanya Uchunguzi wa Magonjwa ya Mifugo katika eneo au sehemu alipo.

·   Kutayarisha  na  kusimamia  mipango  ya  kuzuia  kuthibiti,  na  kutokomeza
     
magonjwa ya mifugo katika eneo lake.

 

10.1.2 SIFA ZA MWOMBAJI

·   Kuajiriwa wenye Shahada ya kwanza ya Tiba ya Mifugo kutoka Chuo Kikuu cha
      Sokoine cha Kilimo au Chuo kingine kinachotambuliwa na Serikali Nambao
     
wamesajiriwa na bodi ya Madaktari wa Mifugo nchini.

 

10.1.3 MSHAHARA

Kwa kuzingatia Ngazi za mishahara ya Serikali yaani TGS F. kwa mwezi

 

MADARAKA

·   Anaweza kupewa majukumu ya/ Madaraka ya kuwa DSMS AU DVO

 

 

9


 

 

 

 

 

 

10.2   AFISA  MIFUGO  MSAIDIZI  DARAJA  LA  II  (LIVESTOCK  FIELD  OFFICER
            GRADE II) - NAFASI 14

Nafasi hizi ni kwa ajili ya Halmashauri ya Manispaa ya Lindi na Halmashauri ya Wilaya ya Chato

10.2.1 MAJUKUMU YA KAZI

·   Atafanya uchunguzi wa magonjwa ya mifugo kwa wafugaji wa eneo lake.

·   Kwa kushirikiana na wakaguzi wa Afya, atakagua nyama na machinjio mara kwa
      mara.

·    Atakusanya takwimu za nyama na mazao yatokanayo na  mifugo kama ngozi na
     
kuandika ripoti

·   Atatibu magojwa ya mifugo chini ya usimamizi wa Daktari wa Mifugo  na kushauri
     
wafugaji jinsi ya kukinga mifugo dhidi ya magonjwa

·   Atatembelea wafugaji mara kwa mara na kuwapa ushauri fasaha wa kitaalamu
     
katika eneo la kazi

·   Atakusanya takwimu zote za maendeleo ya mifugo katika eneo lake.

·    Atashauri na kusimamia ujenzi wa majosho, machinjio, vibanio, na miundo
     
mbinu inayohusiana na ufugaji bora.

·   Atasimamia uchanganyaji wa dawa ya josho.

·    Atahusika na uhamilishaji (Artificial Insermination) na uzalishaji (Breeding) wa
     
mifugo kwa ujumla

·   Atashauri wafugaji kuhusu mbinu bora za kuzalisha maziwa na utunzaji wa
     
ndama.

·   Atafanya kazi zingine za fani yake kama atakavyopangiwa na mkuu wake wa
     
kazi.

 

10.2.2 SIFA ZA MWOMBAJI

·   Kuajiriwa wahitimu wa kidato cha sita waliofuzu mafunzo ya Stashahada ya
     
mifugo   kutoka chuo cha kilimo na mifugo (MATI AU LITI) au chuo kingine
     
chochote kinachotambuliwa na Serikali

10.2.3 MSHAHARA

Kwa kuzingatia Ngazi za mishahara ya Serikali yaani TGS C kwa mwezi

11.0    SEKTA YA KILIMO

11.1   AFISA KILIMO DARAJA LA II (GRADE II ) - NAFASI 2

Nafasi hizi ni kwa ajili ya Halmashauri ya Manispaa ya Sumbawanga

11.1.1 MAJUKUMU YA KAZI

·   Kudhibiti visumbufu vya mazao na mimea.

·   Kukusanya takwimu za bei za mazao kila wiki na kila mwezi.

·   Kukusanya takwimu za upatikanaji wa mazao katika masoko kila wiki/kila mwezi.

·   Kuendesha mafunzo ya wataalam wa kilimo.

·   Kufanya ukaguzi wa ubora na matumizi ya pembejeo na zana.

·   Ufuatiliaji wa mwenendo wa soko la mazao ya biashara.

 

10


 

 

 

 

 

 

 

·   Kuendesha mafunzo juu ya hifadhi bora ya udongo na maji.

·   Kutoa habari juu ya teknolojia mpya kwa wadau.

·   Kuandaa/kuandika taarifa za utekelezaji kwa sekta ndogo ya mazao.

·   Kusimamia/kuendeleza taaluma ya uzalishaji mboga, matunda, maua na mazao
      mengine.

·   Kusimamia/kuendeleza uzalishaji wa mbegu bora.

·   Kuandaa, kutayarisha kufunga na kusambaza mbegu bora.

·   Kufanya majaribio ya magonjwa kwenye mbegu.

·   Kufanya ukaguzi wa mbegu mpya kwa kushirikiana na watafiti wa mbegu kabla
      ya kupitishwa.

·   Kuendesha mafunzo ya kuzalisha mboga, matunda, maua na viungo.

·   Kuhamasisha uzalishaji wa mazao ya bustani.

·   Kufanya utafiti mdogo mdogo wa mazao yanayofaa kulimwa katika sehemu ya
     
kilimo cha umwagiliaji.

·   Kufanya utafiti wa udongo.

·   Kuhamasisha uanzishaji wa vikundi vya wakulima/wamwagiliaji.

·   Kuzalisha mbegu za msingi baada ya kuzalishwa na watafiti.

·   Kuendesha/kusimamia  vishamba  vya  majaribio  vya  mbegu  na  uchunguzi
     
maabara ili kuondoa utata juu ya mbegu.

 

11.1.2 SIFA ZA MWOMBAJI

·   Kuajiriwa wenye Shahada ya kilimo au Shahada ya Sayansi waliojiimarisha
      katika mchepuo wa kilimo kutoka Chuo Kikuu cha Kilimo Sokoine au vyuo
     
vingine vinavyotambuliwa na Serikali.

 

11.1.3 MSHAHARA

Kwa kuzingatia Ngazi za mishahara ya Serikali yaani TGS D kwa mwezi.

 

11.2   AFISA KILIMO MSAIDIZI DARAJA LA II (GRADE II ) - NAFASI 3

Nafasi hizi ni kwa ajili ya Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru na Halmashauri ya Mji Njombe

11.2.1 MAJUKUMU YA KAZI

·   Kushirikiana na watafiti kuendesha vishamba vya majaribio.

·   Kukusanya/kuhifadhi takwimu za majaribio.

·   Kuwafundisha wakulima mbinu za kilimo bora.

·   Kuwafikishia wakulima matokeo ya utafiti.

·   Kuwafundisha wakulima mbinu bora za kilimo, matumizi ya mbolea na madawa,
      pembejeo za kilimo.

·   Kukusanya na kutunza takwimu za mazao na bei kwa wiki, mwezi, robo na
     
mwaka ngazi ya halmashauri.

·   Kukusanya takwimu za mvua.

·   Kushiriki katika savei za kilimo.

 

11


 

 

 

 

 

·   Kushirikiana na vikundi vya wakulima kuhusu matatizo na teknolojia sahihi za
     
kutumia.

·   Kupanga mipango ya uzalishaji.

·   Kupima uotaji wa mbegu na kusimamia taratibu za ukaguzi.

·   Kutathmini na kusavei maeneo ya vyanzo vya maji kwa ajiili ya kuhifadhi.

·   Kutunza miti mizazi.

·   Kuwatambua wasambazaji wa pembejeo.

·   Kutoa mafunzo ya lishe kwa wakulima.

·   Kufanya vipimo vya ubora, unyevunyevu na uotaji wa mbegu.

·   Kusimamia taratibu za ukaguzi.

·   Kudhibiti visumbufu vya mazao na mimea.

·   Kusimamia shughuli za kila siku za majaribio ya kilimo.

·   Kuwaelimisha wakulima juu ya matumizi bora ya udongo na maji.

·   Kutoa ushauri wa kilimo mseto.

·   Kuandaa sheria ndogo za hifadhi ya mazingira.

·   Kutoa taaluma ya uzalishaji wa mboga, matunda, maua na viungo

 

Anaweza kuwa Bwana Shamba wa Kata/Kijiji.

 

11.2.2 SIFA ZA MWOMBAJI

·   Kuajiriwa wahitimu wa Kidato cha Sita (VI) wenye stashahada ya kilimo kutoka
     
vyuo vinavyotambuliwa na Serikali.

 

11.2.3 MSHAHARA

Kwa kuzingatia Ngazi za mishahara ya Serikali yaani TGS C kwa mwezi.

12.0    SEKTA YA AFYA

12.1   DAKTARI DARAJA LA II (GRADE II ) - NAFASI 4

Nafasi hizi ni kwa ajili ya Katibu Tawala Mkoa wa Arusha, Morogoro na Halmashauri ya Wilaya ya Chato

12.1.1 MAJUKUMU YA KAZI

·   Kufanya  kazi  zote  za  matibabu  hospitalini  zinazohusiana  na  magonjwa
     
mbalimbali yakiwemo magonjwa ya watoto, magonjwa ya kina mama na upasuaji
     
wa dharura

·   Kutoa na kusimamia elimu  ya afya pamoja na kuboresha afya ya jamii katika
     
Wilaya na Mikoa au eneo lake la kazi

·   Kuchunguza, kufatilia na kuzuia milipuko ya magonjwa

·   Kutunza takwimu na kuzitumia kama inavyoelekezwa katika misingi ya MTUHA

·   Kupanga na kutathmini huduma za afya katika eneo lake la kazi

·   Kufundisha wanafunzi na watumishi waliopo kwenye eneo lake la kazi

·   Kusimamia na kuelekeza wafanyakazi walio chini yake

·   Kufundisha wanafunzi katika vyuo vya afya vilivyopo eneo lake la kazi

 

12


 

 

 

 

 

 

 

·   Kubuni na kuendesha utafiti na kusambaza matokeo

·   Kubuni na kutayarisha mikakati ya kuinua ubora wa huduma ya fani yake

·   Kushiriki, kuhakiki na kuboresha huduma za afya (medical audit and quality
     
improvement)

·   Kutoa huduma za outreach katika Wilaya/Mkoa wake

·   Kufanya kazi nyingine atakazopangiwa na mkuu wake wa kazi zinazohusiana na
      elimu, uzoefu na ujuzi wake

 

12.1.2 SIFA ZA MWOMBAJI

·   Kuajiriwa   wenye   Shahada   ya   Udaktari   kutoka   Vyuo   Vikuu/   Vyuo
     
vinavyotambuliwa na Serikali waliomaliza mafunzo ya kazi "Interniship" ya muda
      usiopungua miezi kumi na miwili na kupata usajili kutoka Baraza la Madaktari
     
Tanganyika (Medical Council of Tanganyika)

 

12.1.3 MSHAHARA

Kwa kuzingatia Ngazi za mishahara ya Serikali yaani TGHS E. kwa mwezi.

 

12.2   DAKTARI MSAIDIZI ( GRADE II ) - NAFASI 4

Nafasi hizi ni kwa ajili ya Katibu Tawala Mkoa wa Arusha, Halmashauri ya Wilaya ya Chato na Rungwe

12.2.1 MAJUKUMU YA KAZI

·   Kutambua matatizo ya wagonjwa na kutoa huduma za tiba, kinga na huduma
     
kwa kina mama na watoto

·   Kufanya upasuaji wa dharura na wa kawaida

·   Kupanga, kutekeleza na kutathmini huduma za afya sehemu zao za kazi

·   Kupanga utekelezaji wa mipango ya kukabili majanga na dharura mbalimbali

·   Kufanya utafiti katika maeneo mbalimbali ya afya ili kuboresha utoaji huduma

·   Kufanya kazi nyingine atakazopangiwa na mkuu wake wa kazi zinazohusiana na
      elimu, uzoefu na ujuzi wake

 

12.2.2 SIFA ZA MWOMBAJI

·   Kuajiriwa wenye Stashahada ya juu ya Tiba ya miaka isiyopungua miaka miwili

(2) kutoka chuo kinachotambuliwa na Serikali walio na leseni ya kufaaynya kazi kutoka Baraza la Madaktari Tanganyika (Medical Council of Tanganyika) pamoja na uzoefu wa kazi kwa muda usiopungua miaka mitatu

 

12.2.3 MSHAHARA

Kwa kuzingatia Ngazi za mishahara ya Serikali yaani TGHS C kwa mwezi.

12.3   AFISA AFYA MAZINGIRA DARAJA LA II (ENVIRONMENT OFFICER GRADE
            II) - NAFASI 1

Nafasi hizi ni kwa ajili ya Katibu Tawala Mkoa wa Rukwa

12.3.1 MAJUKUMU YA KAZI

 

13


 

 

 

 

 

·   Kutoa ushauri na kusimamia njia bora za usambazaji wa maji safi na salama na
      utupaji wa taka

·   Kuelimisha jamiii juu ya mbinu za kujikinga na milipuko ya magonjwa

·   Kukusanya na kuchambua takwimu za Afya ya Mazingira

·   Kusimamia utekelezaji wa Sheria zinazohusu Afya ya Mazingira

·   Kuandaa taarifa za utekelezaji na kuziwasilisha katika mamlaka husika

·   Kuandaa na kufuatilia mikakati ya kuboresha na kusimamia usalalma wa afya
     
kazini

·   Kuhakiki afya bandarini na mipakani

·   Kuratibu na kuhakiki kaguzi za vyakula, maji, kemikali, viwanda, sehemu za kazi
      na maeneo ya jamii

·   Kufanya kazi nyingine atakazopangiwa na mkuu wake wa kazi zinazohusiana na
      elimu, uzoefu na ujuzi wake

 

12.3.2 SIFA ZA MWOMBAJI

·   Kuajiriwa wenye Shahada ya Sayansi za Afya ya Mazingira na mafunzo kazini na
     
kusajiliwa na Bodi ya Wataalam wa Afya Mazingira

 

12.3.3 MSHAHARA

Kwa kuzingatia Ngazi za mishahara ya Serikali yaani TGHS C kwa mwezi.

 

12.4   AFISA AFYA MAZINGIRA MSAIDIZI (GRADE II ) - NAFASI 2

Nafasi hizi ni kwa ajili ya Halmashauri ya Wilaya ya Babati na Rufiji

12.4.1 MAJUKUMU YA KAZI

·   Kudhibiti na kuzuia milipuko ya wagonjwa

·   Kupambana na kuzuia wadudu na wanyama wanaoeneza magonjwa

·   Kusimamia uzikaji wa maiti zisizotambuliwa na zile zinazotokana na magonjwa
     
ya kuambukiza

·   Kuandaa taarifa mbalimbali za Afya  ya Mazingira katika ngazi ya kata na
     
kuziwasilisha katika mamlaka husika

·   Kukusanya na kuchambua takwimu za Afya ya Mazingira katika kata na kutoa
     
mrejesho ili kuchukua hatua zinazostahili

·   Kutoa elimu ya afya ya mazingira kwa jamii

·   Kukagua mazingira katika sehemu vinapotengenezwa vyakula ili kuhakikisha
     
usalama na afya ya jamii

·   Kusimamia sheria za afya ya mazingira katika ngazi ya  Kata pamoja na kusaidia
     
jamii katika kutengeneza sheria ndogondogo

·   Kuhamasisha jamii katika kuboresha vyanzo vya maji na Usafi wa Mazingira

·   Kuhamasisha jamii kuhusu utekelezajiwa Huduma za Afya ya msingi katika ngazi
     
ya Kata

·   Kufanya kazi nyingine atakazopangiwa na mkuu wake wa kazi zinazohusiana na
      elimu, uzoefu na ujuzi wake

 

14


 

 

 

 

 

 

 

12.4.2 SIFA ZA MWOMBAJI

·   Kuajiriwa wenye Stashahada ya Sayansi ya Afya ya Mazingira ya miaka mitatu
     
kutoka chuo kinachotambuliwa na Serikali na awe amesajiliwa na Bodi  ya
     
Wataalam wa Afya Mazingira

 

10.1.1 MSHAHARA

Kwa kuzingatia Ngazi za mishahara ya Serikali yaani TGHS B kwa mwezi.

 

12.5   AFISA MUUGUZI DARAJA LA II (NURSING OFFICER GRADE II) - NAFASI 6

Nafasi hizi ni kwa ajili ya Katibu Tawala Mkoa wa Morogoro, Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga na Halmashauri ya Mji Njombe

12.5.1 MAJUKUMU YA KAZI

·   Kufanya kazi za kiuguzi za kuhudumia wateja katika jamii, hospitalini na sehemu
      zote zinapotolewa huduma za afya

·   Kukusanya takwimu muhimu za afya

·   Kuwaelekeza na kusimamia wauguzi walio chini yake

·   Kutoa huduma kwa wagonjwa majumbani

·   Kutoa ushauri nasaha

·   Kutayarisha mpango wa kazi kwa ajili ya huduma za uuguzi

·   Kutoa huduma za kinga na uzazi

·   Kuelimisha wagonjwa na jamii

·   Kufanya kazi nyingine atakazopangiwa na mkuu wake wa kazi zinazohusiana na
      elimu, uzoefu na ujuzi wake

 

12.5.2 SIFA ZA MWOMBAJI

·   Kuajiriwa wenye Shahada ya Uuguzi kutoka Chuo Kikuu kinachotambuliwa na
      Serikali, waliohitimu mafunzo ya vitendo kazini (Internship) ya mwaka mmoja,
     
waliosajiliwa na Baraza la Wauguzi na Wakunga Tanzania

 

12.5.3 MSHAHARA

Kwa kuzingatia Ngazi za mishahara ya Serikali yaani TGHS C kwa mwezi.

12.6   AFISA MUUGUZI MSAIDIZI DARAJA LA II (ASSISTANT NURSING OFFICER
            GRADE II ) - NAFASI 12

Nafasi hizi ni kwa ajili ya Katibu Tawala Mkoa wa Mara, Rukwa, Kigoma, Halmashauri ya Jiji la Mwanza, Halmashauri ya Wilaya ya Babati, Mbozi, Mtwara na Monduli

12.6.1 MAJUKUMU YA KAZI

·   Kutoa huduma za uuguzi

·   Kukusanya takwimu muhimu za afya

·   Kuwaelekeza kazi wauuguzi walio chini yake

·   Kuwaelimisha wagonjwa na jamii kuhusu matatizo yao ya kiafya

·   Kutoa huduma za kinga na uzazi

 

 

15


 

 

 

 

 

·   Kufanya kazi nyingine atakazopangiwa na mkuu wake wa kazi zinazohusiana na
      elimu, uzoefu na ujuzi wake

 

12.6.2 SIFA ZA MWOMBAJI

·   Kuajiriwa wenye Stashahada (Diploma) ya Uuguzi ya muda usiopungua miaka
     
miwili kutoka Chuo kinachotambuliwa na Serikali, waliohitimu mafunzo ya vitendo
     
kazini (Internship) ya mwaka mmoja, waliosajiliwa na Baraza la Wauguzi na
     
Wakunga Tanzania

 

10.1.2 MSHAHARA

Kwa kuzingatia Ngazi za mishahara ya Serikali yaani TGHS B kwa mwezi.

 

12.7   MUUGUZI DARAJA LA II (NURSE GRADE II ) - NAFASI 18

Nafasi hizi ni kwa ajili ya Katibu Tawala Mkoa wa Arusha, Iringa, Mara, Rukwa, Kigoma Halmashauri ya Wilaya ya Simanjiro, Mtwara, Rufiji, Rungwe na Tandahimba

12.7.1 MAJUKUMU YA KAZI

·   Kufanya kazi za kiuguzi za kuhudumia wateja katika jamii, hospitali na sehemu
     
zote zinapotolewa huduma za afya

·   Kusimamia na kuratibu kazi zote za wahudumu wa afya katika sehemu yake ya
      kazi

·   Kukusanya takwimu na kutayarisha taarifa za utendaji wake wa kazi

·   Kutoa huduma kwa wagonjwa majumbani

·   Kutoa ushauri nasaha

·   Kutoa huduma za kinga na uzazi wa mpango

·   Kutoa huduma za uzazi na afya ya mototo

·   Kuwaelimisha wagonjwa na jamii kuhusu matatizo yao ya kiafya

·   Kufuatilia utunzaji wa vitendea kazi katika maeneo yake ya kazi

·   Kufanya kazi nyingine atakazopangiwa na mkuu wake wa kazi zinazohusiana na
      elimu, uzoefu na ujuzi wake

 

12.7.2 SIFA ZA MWOMBAJI

·   Kuajiriwa  wenye  cheti  cha  Uuguzi  cha  miaka  miwili  kutoka  katika  Chuo
     
kinachotambuliwa na Serikali na kuandikishwa (Enrolled) na Baraza la Wauguzi
      na Wakunga Tanzania

 

12.7.3 MSHAHARA

Kwa kuzingatia Ngazi za mishahara ya Serikali yaani TGHS A kwa mwezi.

12.8   TABIBU DARAJA LA II (GRADE II ) - NAFASI 17

Nafasi hizi ni kwa ajili ya Katibu Tawala Mkoa wa Kigoma, Halmashauri ya Wilaya ya
Babati, Chato, Rufiji, Mbinga, Rungwe, Tunduru, Tandahimba na Halmashauri ya Mji
Njombe

 

 

16


 

 

 

 

 

 

 

12.8.1 MAJUKUMU YA KAZI

·   Kufanya kazi zote zinazofanywa na Tabibu Msaidizi

·   Kutambua na kutibu magonjwa ya kawaida

·   Kusimamia utendaji wa watumishi walio chini yake na kufanya upasuaji mdogo

·   Kushauri na kuhamasisha wananchi kuchangia huduma za Afya za Mfuko wa
     
Afya ya Jamii

·   Kuweka kumbukumbu za vifaa na zana za kutolea huduma

·   Kuweka kumbukumbu, kuandaa na kutoa taarifa za utekelezaji

·   Kufanya kazi nyingine atakazopangiwa na mkuu wake wa kazi zinazohusiana na
      elimu, uzoefu na ujuzi wake

 

12.8.2 SIFA ZA MWOMBAJI

·   Kuajiriwa wahitimu wa kidato cha nne/sita wenye Stashahada ya Tabibu ya
     
muda usiopungua miaka mitatu kutoka Chuo kinachotambuliwa na Serikali

 

12.8.3 MSHAHARA

Kwa kuzingatia Ngazi za mishahara ya Serikali yaani TGHS B kwa mwezi.

 

12.9   TABIBU MSAIDIZI DARAJA LA II (ASSISTANT GRADE II) - NAFASI 5

Nafasi hizi ni kwa ajili ya Halmashauri ya Wilaya ya Babati, Chato, Mtwara, Rufiji na Tunduru

12.9.1 MAJUKUMU YA KAZI

·   Kutoa huduma za Kinga na Tiba

·   Kutambua na kutibu magonjwa

·   Kutoa huduma ya Afya ya Msingi (Primary Health Care)

·   Kufanya kazi nyingine atakazopangiwa na mkuu wake wa kazi zinazohusiana na
      elimu, uzoefu na ujuzi wake

 

12.9.2 SIFA ZA MWOMBAJI

·   Kuajiriwa wenye Cheti cha Mtihani wa Taifa wa kidato cha nne (IV) ambao
     
wamehitimu Mafunzo ya Miaka Miwili ya Tabibu Wasaidizi (Clinical Assistants
     
Certificate)

 

12.9.3 MSHAHARA

Kwa kuzingatia Ngazi za mishahara ya Serikali yaani TGHS A kwa mwezi.

 

12.10 FIZIOTHERAPIA DARAJA LA II (PHYSIOTHERAPIST GRADE II ) - NAFASI 1

Nafasi hii ni kwa ajili ya Katibu Tawala Mkoa wa Arusha

12.10.1          MAJUKUMU YA KAZI

·   Kutoa tiba kwa kuzoeza viungo/kwa vitendo

·   Kukusanya na kutunza takwimu na taarifa za mgonjwa

·   Kutunza vifaa vya kutolea tiba

·   Kutoa elimu ya Afya kwa jamii kuhusu kutambua dalili na kuzuia ulemavu

17


 

 

 

 

 

·   Kufanya kazi nyingine atakazopangiwa na mkuu wake wa kazi zinazohusiana na
      elimu, uzoefu na ujuzi wake

 

12.10.2          SIFA ZA MWOMBAJI

·   Kuajiriwa wahitimu wa kidato cha nne/sita wenye Stashahada ya miaka mitatu
     
katika fani ya Fiziotherapia kutoka Chuo kinachotambuliwa na Serikali

 

12.10.3          MSHAHARA

Kwa kuzingatia Ngazi za mishahara ya Serikali yaani TGHS B kwa mwezi.

12.11 MTEKNOJOJIA DARAJA LA II - MAABARA (TECHNOLOGIST GRADE II) -
           
NAFASI 11

Nafasi hizi ni kwa ajili ya Halmashauri ya Wilaya ya Babati, Mbinga, Monduli, Mpanda, Rufiji na Simanjiro

12.11.1          MAJUKUMU YA KAZI

·   Kupima sampuli zinazoletwa maabara

·   Kuhifadhi sampuli zinazotakiwa kufanyiwa uchunguzi au kupelekwa Maabara za
      ngazi za juu

·   Kufanya  kazi  za  ukaguzi  wa  maabara  ambazo  zimepatikana  wakati  wa
     
uchunguzi

·   Kufundisha watumishi walio chini yake

·   Kufanya kazi nyingine atakazopangiwa na mkuu wake wa kazi zinazohusiana na
      elimu, uzoefu na ujuzi wake

 

12.11.2          SIFA ZA MWOMBAJI

·   Kuajiriwa wenye Stashahada ya katika fani ya Uteknolojia ya muda wa miaka
     
mitatu katika fani ya Maabara kutoka chuo kinachotambuliwa na Seriakli na
     
ambao wamesajiliwa na Mabaraza pale inapohusika

 

12.11.3          MSHAHARA

Kwa kuzingatia Ngazi za mishahara ya Serikali yaani TGHS B kwa mwezi.

12.12 MTEKNOJOJIA DARAJA LA II - DAWA (TECHNOLOGIST GRADE II) NAFASI
           
1

Nafasi hii ni kwa ajili ya Halmashauri ya Jiji la Mwanza,

12.12.1          MAJUKUMU YA KAZI

·   Kuainisha, kuandaa na kuagiza mahitaji ya dawa na vfaa tiba katika eneo lake la
      kazi

·   Kugawa dawa na vifaa tiba kwa wagonjwa na watumishi

·   Kuhifadhi dawa na vifaa tiba

·   Kuelimisha jamii kuhusu matumizi sahihi ya dawa

·   Kukagua dawa, vifaa tiba kemikali, vitendanishi na vipodozi katika eneo lake la
     
kazi

 

18


 

 

 

 

 

 

 

·   Kutoa taarifa juu ya madhara yatokanayo na matumizi ya dawa na vifaa tiba

·   Kuratibu kazi za kamati ya dawa na vifaa tiba

·   Kufanya  uchuguzi  wa  ubora  wa  dawa,  vifaa  tiba  kemikali,  vitendanishi  na
      vipodozi

·   Kufanya kaguzi mbalimbali katika sehemu zinazohifadhiwa dawa

·   Kusimamia utendaji wa kazi watumishi walio chini yake

·   Kutunza kumbukumbu za dawa na vifaa tiba

·   Kufanya kazi nyingine atakazopangiwa na mkuu wake wa kazi zinazohusiana na
      elimu, uzoefu na ujuzi wake

 

12.12.2          SIFA ZA MWOMBAJI

·   Kuajiriwa wenye Stashahada ya katika fani ya Uteknolojia ya muda wa miaka
     
mitatu katika fani ya Madawa kutoka chuo kinachotambuliwa na Seriakli na
     
ambao wamesajiliwa na Mabaraza pale inapohusika

 

12.12.3          MSHAHARA

Kwa kuzingatia Ngazi za mishahara ya Serikali yaani TGHS B kwa mwezi.

 

12.13 MTEKNOJOJIA  MSAIDIZI     -  MAABARA  (ASSISTSNT  TECHNOLOGIST  -

LABORATORY) - NAFASI 2

Nafasi hizi ni kwa ajili ya Halmashauri ya Wilaya ya Rungwe

12.13.1          MAJUKUMU YA KAZI

·   Kuandaa vitendanishi (reagents) vya kufanyia vipimo vya Maabara

·   Kufanya kazi za awali sampuli zinazoletwa maabara

·   Kukusanya damu kutoka kwa wagonjwa na watu wanaojitolea

·   Kurekodi matokeo ya vipimo kwenye regista

·   Kutayarisha vifaa vya kazi

·   Kuhifadhi kwa mujibu wa taratibu sampuli zote zinazohitaji kuhifadhiwa baada ya
     
uchunguzi

·   Kufanya kazi nyingine atakazopangiwa na mkuu wake wa kazi zinazohusiana na
      elimu, uzoefu na ujuzi wake

 

12.13.2          SIFA ZA MWOMBAJI

·   Kuajiriwa wahitimu wa kidato cha nne wenye cheti cha miaka miwili katika fani ya
     
Maabara kutoka Chuo kinachotambuliwa na Serikali na ambao wamesajiliwa na
      Mabaraza pale inapohusika

 

12.13.3          MSHAHARA

Kwa kuzingatia Ngazi za mishahara ya Serikali yaani TGHS A kwa mwezi.

 

12.14 MHUDUMU WA AFYA (MEDICAL ATTENDANT) - NAFASI 26

Nafasi hizi ni kwa ajili ya Katibu Tawala Mkoa wa Kigoma, Ruvuma, Halmashauri ya
Manispaa  ya  Sumbawanga,  Halmashauri  ya  Wilaya  ya  Babati,  Mbozi,  Mpanda,

19


 

 

 

 

 

 

 

Monduli,  Rufiji,  Rungwe,  Simanjiro,  Tandahimba,  Mbinga  na  Halmashauri  ya  Mji Njombe

12.14.1          MAJUKUMU YA KAZI

·   Kufanya kazi atakazopangiwa na mkuu wake wa kazi zinazohusiana na elimu,
     
uzoefu na ujuzi wake

 

12.14.2          SIFA ZA MWOMBAJI

·   Kuajiriwa wahitimu wa kidato cha nne waliopata mafunzo ya mwaka mmoja
     
katika fani ya afya

 

12.14.3          MSHAHARA

Kwa kuzingatia Ngazi za mishahara ya Serikali yaani TGHOS A kwa mwezi.

13.0    MKAGUZI WA HESABU WA NDANI DARAJA LA II (INTERNAL AUDITOR
     
GRADE II) - NAFASI 15

Nafasi hizi ni kwa ajili ya Waajiri Mbalimbali katika Utumishi wa Umma

13.1 MAJUKUMU YA KAZI

·   Kufanya ukaguzi wa hesabu katika idara

·   Kusahihisha na kuidhinisha ripoti za ukaguzi

·   Kusahihisha na kuidhinisha hoja za ukaguzi wa ndani (Internal Audit Queries)

 

13.2 SIFA ZA MWOMBAJI

·   Kuajiriwa  wahitimu  wa  kidato  cha  sita  wenye  cheti  cha  kati  cha  Uhasibu
     
(Intermidiate Stage) kinachotolewa na NBAA au sifa zinazolingana na hizo. Au

·   Kuajiriwa wenye Shahada ya Biashara/ Sanaa yenye uelekeo wa Uhasibu au
     
Stashahada ya juu ya Uhasibu (Advanced Diploma in Accounting) kutoka vyuo
      au Taasisi yoyote inayotambuliwa na Serikali.

 

13.3 MSHAHARA

Kwa kuzingatia Ngazi za mishahara ya Serikali yaani TGS D kwa mwezi.

14.0    MHASIBU DARAJA LA II (ACCOUNTANT GRADE II) - NAFASI 15 Nafasi hizi ni kwa ajili ya Waajiri Mbalimbali katika Utumishi wa Umma

14.1 MAJUKUMU YA KAZI

·   Kuidhinisha hati za malipo.

·   Kuandika taarifa ya mapato na matumizi ya mwezi.

·   Kusimamia Wahasibu Wasaidizi katika kazi zao za kila siku.

·   Kusimamia shughuli za uhasibu kwenye Kitengo cha Idara.

·   Kuandika taarifa ya maduhuli.

 

 

 

 

 

20


 

 

 

 

 

 

 

14.2 SIFA ZA MWOMBAJI

Kuajiriwa wenye 'mojawapo' ya sifa zilizotajwa hapa chini:-

·    'Intermediate certificate' inayotolewa na NBAA.

·   Shahada ya Biashara/Sanaa yenye mwelekeo wa Uhasibu au Stashahada ya juu
      ya Uhasibu kutoka Chuo Kikuu/Taasisi yoyote inayotambuliwa na Serikali.

·   Stashahada ya Juu ya Uhasibu Serikalini (Advanced Diploma in Government
     
Accounting)

 

14.3 MSHAHARA

Kwa kuzingatia Ngazi za mishahara ya Serikali yaani TGS D kwa mwezi.

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

21

 

0 comments:

Post a Comment