Saturday, September 27, 2014

FUNDI SANIFU MSAIDIZI MITAMBO YA MAJI (PAMPU) – NAFASI 25-ZINARUDIWA



FUNDI SANIFU MSAIDIZI MITAMBO YA MAJI (PAMPU) – NAFASI 25-ZINARUDIWA


OFISI YA RAIS SEKRETARIETI YA AJIRA KATIKA UTUMISHI WA UMMA
Kumb. Na EA.7/96/01/H/0325 Septemba, 2014

TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI
Sekretariati ya Ajira katika Utumishi wa Umma ni chombo ambacho kimeundwa kwa
mujibu wa Sheria ya Utumishi wa Umma Na. 8 ya mwaka 2002 kama ilivyorekebishwa
na Sheria Na. 18 ya mwaka 2007 kifungu 29(1). Kwa mujibu wa Sheria hiyo, chombo hiki,
pamoja na kazi zingine kimepewa jukumu la kutangaza nafasi wazi za kazi zinazotokea
katika Utumishi wa Umma kwa niaba ya Waajiri (Taasisi za Umma).
Katibu wa Sekretarieti ya Ajira Katika Utumishi wa Umma anakaribisha maombi ya
Watanzania wenye sifa na uwezo wa kujaza nafasi 102 za kazi kwa ajili ya Katibu Mkuu
Wizara ya Maji,
NB: MASHARITI YA JUMLA KWA KAZI ZOTE.
i. Waombaji wote wawe ni Raia wa Tanzania na wenye umri usiozidi miaka 45
ii. Waombaji wote waambatishe cheti cha kuzaliwa.
iii. Waombaji ambao tayari ni watumishi wa Umma na wamejipatia sifa za kuingilia
katika kada tofauti na walizonazo, wapitishe barua zao za maombi ya nafasi za
kazi kwa waajiri wao na Waajiri wajiridhishe ipasavyo.
iv. Nafasi ya kazi inayoombwa iandikwe juu ya bahasha, kutozingatiwa hili
kutasababisha maombi ya kazi kuwa batili.
v. Waombaji waambatishe maelezo binafsi yanayojitosheleza (Detailed C.V) yenye
anwani na namba za simu za kuaminika pamoja na majina ya wadhamini (referees)
watatu wa kuaminika.
vi. Maombi yote yaambatane na vyeti vya taaluma, maelezo, nakala za vyeti vya kidato
cha nne na kidato cha sita kwawale waliofikia kiwango hicho na vyeti vya kuhitimu
mafunzo mbalimbali kwa kuzingatia sifa za kazi husika. Viambatanisho hivyo vibanwe
sawa sawa kuondoa uwezekano wa kudondoka kupotea.
- Postgraduate/Degree/Advanced Diploma/Diploma/Certificates.
- Cheti cha mtihani wa kidato cha IV na VI
- Computer Certificate
- Vyeti vya kitaaluma (Professional certificates from respective boards)
- Picha moja "Passport size" ya hivi karibuni iandikwe jina kwa nyuma.
vii. Testmonials", "Provisional Results", "Statement of results", hati matokeo za
kidato cha nne na sita (FORM IV AND FORM VI RESULTS SLIPS) HAVITAKUBALIWA.
viii. Waombaji waliosoma nje ya Tanzania wahakikishe vyeti vyao vimehakikiwa na
kuidhinishwa na Mamlaka husika (TCU na NECTA).
ix. Waombaji waliostaafishwa katika Utumishi wa Umma hawaruhusiwi kuomba isipokuwa
kama wanakibali cha Katibu Mkuu Kiongozi.
x. Waombaji kazi ambao tayari ni waajiriwa katika nafasi za kuingilia walioko katika
utumishi wa umma wasiombe na wanatakiwa kuzingatia maelekezo yaliyo katika
Waraka Na CAC. 45/257/01/D/140 wa tarehe 30 Novemba 2010.
xi. Uwasilishaji wa taarifa na sifa za kugushi wahusika watachukuliwa hatua za
kisheria.
xii. Mwisho wa kupokea barua za maombi ni tarehe 8 Oktoba, 2014
xiii. Aidha, uwasilishaji wa barua kwa mkono katika ofisi za Sekretarieti ya ajira
HAURUHUSIWI.
xiv. Maombi yanaweza kuandikwa kwa Lugha ya Kiswahili au Kiingereza na yatumwe
kupitia posta kwa anuani ifuatayo.
Katibu,
AU
Secretary,
Sekretariati ya Ajira katika
Public Service Recruitment
Utumishi wa Umma,
Secretariat,
SLP.63100,
P.O.Box 63100
Dar es Salaam.
Dar es Salaam.
Nafasi hizi ni kwa ajili ya Katibu Mkuu Wizara ya Maji.
MAJUKUMU YA KAZI
 Atafanya kazi kwa kuongozwa na chini ya uangalizi wa Fundi Sanifu aliyesajiliwa ili
aweze;
 Kufunga pampu na injini za aina mbalimbali za miradi ya maji na usafi wa mazingira;
 Kufanya usafi na ukaguzi wa pampu na injini za miradi ya maji na usafi wa mazingira kwa ajili ya kukidhi uendeshaji nadhifu, endelevu na kuzuia uharibifu;
 Kuhudumia uendeshaji wa pampu na injini za miradi ya maji;
 Kufanya matengenezo ya kawaida, ya vipindi na ya kuzuia uharibifu wa pampu na injini
kwa kufuata miongozo ya uendeshaji na matengenezo na inapohitajika kwa dharura;
 Kunakiri, kutayarisha, kukusanya, kutunza na kuziwasilisha takwimu za uendeshaji na
matengenezo ya pampu na injini za miradi ya maji;
 Kumsaidia Fundi Sanifu katika kazi za kiufundi.
SIFA ZA MWOMBAJI
 Kuajiriwa wahitimu wa kidato cha nne waliohudhuria na kufaulu mafunzo ya mwaka
mmoja kutoka Chuo cha Maji au Chuo chochote kinachitambuliwa na Serikali ambao
wana Cheti cha ufundi Daraja III (Mitambo Ya Maji (Pampu).
MSHAHARA
 Kwa kuzingatia Ngazi za mishahara ya Serikali yaani TGS A kwa mwezi


Related Posts:

  • Neno la leoHere is your word for today:Verse:           Isaiah 42:5-6 This is what God says - "I, the Lord, have called you; I will take hold of your hand and I will keep you!"Just look what God says He will do. 1. He calls yo… Read More
  • SOCIAL SECURITY REGULATORY AUTHORITY VACANCIESSOCIAL SECURITY REGULATORY AUTHORITY VACANCIES The Social Security Regulatory Authority (SSRA) was established by an Act of Parliament No 8 of 2008 with the major objective of supervising and regulating the social security se… Read More
  • Field Researcher (2 Posts)Savannas Forever Tanzania Employment Opportunities Employment Opportunity Savannas Forever Tanzania (SFTZ) is a Tanzanian non-governmental organization that conducts baseline survey and communication to rural villages on… Read More
  • Associate Site CoordinatorJob Title : Associate Site Coordinator Source : The Guardian, August 17, 2011 Requirements : Bachelor's Degree or Advanced Diploma, preferably in Social Sciences or Public… Read More
  • Various Jobs  Commissioning Engineer ( 5-12 yrs. )CH2M HILLDoha - Qatar QSTec is a joint venture between Qatar Foundation, SolarWorld AG and the Qatar Development Bank and will produce 3,600 tons per year of polysilicon for export to … Read More

0 comments:

Post a Comment