
Kuiga ni kawaida kwa wengi.Wapo walioiga mambo fulani na hatimaye wakafanikiwa, na pia wapo walioiga vitu flani wakaharibikiwa.Huyu aliiga na akaharibu kila kitu...
Ni
msanii wa siku nyingi katika fani.Alitamba zaidi akiwa Kaole, na hata
mwanzoni mwa ujio wa filamu za Kanumba alizidi tu
kashaini....
Kiasili
ni mweusi japo siku hizi kuna weupe fulani katika ngozi yake
nyororo.Ana sura nzuri yenye mvuto,umbo aslia la kibantu,meno yake
meupe yamepambwa na mwanya mdogo na kufanya iwe fahari kumuona
akitabasamu...
Hana
kashfa ya kuvaa nguo fupi sana ila aliwahi kukumbwa na skendo kubwa
zaidi.Mkumbuke vizuri.Mrefu wa wastani,anajua kutembea,anaongea kwa
mapozi huku akipenda kulamba papi ya midomo yake. Umemjua???....Hapana, siyo
huyo...!!
Huyu
ni mpole kiasili na anapendwa sana na mama yake.Katika maigizo ana
uwezo wa kukufanya uamini unachoangalia ni kitu halisi.Japo huwezi
kumtaja, ila ndani ya wasanii kumi anapaswa kuwamo...
Na
ingawa mvuto wake umepungua kiasi,ila bado mrembo sana.Lakini wakati
anaigiza Kaole alikuwa mrembo zaidi.Kwa uzuri wake , alivuma na kila
habari inayohusu mwanaume maarufu na mwenye pesa
Habari
ya kutakiwa na kila mwanaume , wenye rangi na vipato tofauti
zilisikika kila kona.Baadhi alitoka nao na wengine haikuwa bahati
yao....
Toka
kitambo almanusura aolewe, ila ni miaka ya juzi juzi ndipo
aliolewa.Uzuri wake si wa kutafuta, kila mwenye macho na ngozi ya
kuhisi atautambua....
Mbali
na majanga yote aliyopitia katika maisha yake,mengine yakibaki
kumchafua na watu kudhani hawezi kuolewa na mwanaume yeyote kabla ya
ile bahati ya mtende akaolewa; yeye aliamua kuachana na ndoa yake kwa
kuona aishi katika umaarufu wake....
Mara
kadhaa alikuwa akiwaambia marafiki zake kuwa, mwenye hadhi na
anayetakiwa kuishi kama Wema Sepetu sio Wema bali ni yeye na wakongwe
wengine waliosotea sanaa na kuipigania kama roho zao na kuilinda kama
mboni ya jicho lao.....
Akaona
ndoa sio mahala pake,bila sababu za msngi akaamua kumwambia mumewe
watengane....Japo haikuwa rahisi ,lakini walitengana!!
Cha
kufurahisha ni kwamba bado Wema anaishi kama Wema na bado yeye
haishi kama Wema Sepetu na ndoa haipo tena...Umemjua
ninayemzungumzia?
0 comments:
Post a Comment