Tuesday, May 13, 2014

HELKOPTA ILIYODONDOKA NCHINI KENYA NA KUUA 1 PIA KUJERUHI 11

 
 
 
 
Kamanda wa Polisi Kaunti ya Mandera kaskazini mwa Kenya amesema kuwa, mtu mmoja amefariki dunia na wengine kumi na moja kujeruhiwa vibaya baada ya helkopta ya jeshi la nchi hiyo KDF kuanguka katika eneo la makazi ya raia.
Kamanda Noah Mwavanda amesema kuwa, helkopta hiyo ilikuwa imewabeba wanajeshi kutoka eneo la Elwak na kuwapeleka katika mji wa Garissa.

0 comments:

Post a Comment