Monday, November 17, 2014

MSAIDIZI WA OFISI (OFFICE ASSISTANT) – NAFASI 30


MSAIDIZI WA OFISI (OFFICE ASSISTANT) – NAFASI 30

OFISI YA RAIS SEKRETARIETI YA AJIRA KATIKA UTUMISHI WA UMMA
TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI
Sekretariati ya Ajira katika Utumishi wa Umma ni chombo ambacho kimeundwa kwa
mujibu wa Sheria ya Utumishi wa Umma Na. 8 ya mwaka 2002 kama ilivyorekebishwa
na Sheria Na. 18 ya mwaka 2007 kifungu 29(1). Kwa mujibu wa Sheria hiyo, chombo
hiki, pamoja na kazi zingine kimepewa jukumu la kutangaza nafasi wazi za kazi
zinazotokea katika Utumishi wa Umma kwa niaba ya Waajiri (Taasisi za Umma).
Katibu wa Sekretarieti ya Ajira Katika Utumishi wa Umma anakaribisha maombi ya
Watanzania wenye sifa na uwezo wa kujaza Nafasi za kazi 119.
NB: MASHARITI YA JUMLA KWA KAZI ZOTE.
Waombaji wote wawe ni Raia wa Tanzania na wenye umri usiozidi miaka 45
i. Waombaji wote waambatishe cheti cha kuzaliwa.
ii. Waombaji ambao tayari ni watumishi wa Umma na wamejipatia sifa za kuingilia
katika kada tofauti na walizonazo, wapitishe barua zao za maombi ya nafasi za
kazi kwa waajiri wao na Waajiri wajiridhishe ipasavyo.
iii. Nafasi ya kazi inayoombwa iandikwe juu ya bahasha, kutozingatiwa hili
kutasababisha maombi ya kazi kuwa batili.
iv. Waombaji waambatishe maelezo binafsi yanayojitosheleza (Detailed C.V) yenye
anwani na namba za simu za kuaminika pamoja na majina ya wadhamini (referees)
watatu wa kuaminika.
v. Maombi yote yaambatane na vyeti vya taaluma, maelezo, nakala za vyeti vya
kidato cha nne na kidato cha sita kwa wale waliofikia kiwango hicho na vyeti vya
kuhitimu mafunzo mbalimbali kwa kuzingatia sifa za kazi husika. Viambatanisho
hivyo vibanwe sawa sawa kuondoa uwezekano wa kudondoka kupotea.
2
- Postgraduate/Degree/Advanced Diploma/Diploma/Certificates.
- Cheti cha mtihani wa kidato cha IV na VI
- Computer Certificate
- Vyeti vya kitaaluma (Professional certificates from respective boards)
- Picha moja "Passport size" ya hivi karibuni iandikwe jina kwa nyuma.
vi. Testmonials", "Provisional Results", "Statement of results", hati matokeo za
kidato cha nne na sita (FORM
IV AND FORM VI RESULTS SLIPS) HAVITAKUBALIWA.
vii. Waombaji waliosoma nje ya Tanzania wahakikishe vyeti vyao vimehakikiwa na
kuidhinishwa na Mamlaka husika (TCU na NECTA).
viii. Waombaji waliostaafishwa katika Utumishi wa Umma hawaruhusiwi kuomba
isipokuwa kama wanakibali cha Katibu Mkuu Kiongozi.
ix. Waombaji kazi ambao tayari ni waajiriwa katika nafasi za kuingilia walioko
katika utumishi wa umma wasiombe na wanatakiwa kuzingatia maelekezo
yaliyo katika Waraka Na CAC. 45/257/01/D/140 wa tarehe 30 Novemba, 2010.
x. Uwasilishaji wa taarifa na sifa za kugushi wahusika watachukuliwa hatua za
kisheria.
xi. Mwisho wa kupokea barua za maombi ni tarehe 27 Novemba, 2014
xii. Aidha, uwasilishaji wa barua kwa mkono katika ofisi za Sekretarieti ya ajira
HAURUHUSIWI.
xiii. Maombi yanaweza kuandikwa kwa Lugha ya Kiswahili au Kiingereza na yatumwe
kupitia posta kwa anuani ifuatayo.
Katibu,
Sekretariati ya Ajira katika
Utumishi wa Umma,
SLP.63100,
Dar es Salaam.

AU


Secretary,

Public Service Recruitment
Secretariat,
P.O.Box 63100
Dar es Salaam.
12.0 MSAIDIZI WA OFISI (OFFICE ASSISTANT) – NAFASI 30
12.1 MAJUKUMU YA KAZI
• Kufanya usafi wa ofisi na mazingira ya nje na ndani ikiwa ni pamoja na kufagia,
kufuta vumbi, kupiga deki, kukata majani, kupalilia bustani, kumwagilia maji
bustani, kupanda maua au miti na kusafisha vyoo.
• Kuchukua na kupeleka majalada na hati nyingine kwa maofsa waoaohusika na
kuyarudisha sehemu zinazohusika.
• Kusambaza barua za Ofisi kama jinsi atakavyoelekezwa.
• Kutayarisha chai ya ofisi.
• Kupeleka mfuko wa posta na kuchukua barua kutoka Posta.
• Kuhakikisha kwamba vifaa vya ofisi vinaweka sehemu zinazostahili.
9
• Kufungua Milango na Madirisha ya Ofisi wakati wa Asubuhi na Jioni kuyafunga
baada ya Saa za Kazi.
• Kudurufu barua au machapisho kwenye mashine za kudurufia.
• Kuweka katika majalada nakala za barua zilizochapwa katika ofisi walizomo.
• Kutunza vifaa vya ofisi na kutoa ripoti kila vinapoharibika.
12.2 SIFA ZA MWOMBAJI
• Kuajiriwa wahitimu wa kidato cha nne waliofaulu vizuri katika masomo ya
Kiingereza, Kiswahili na Hisabati.
12.3 MSHAHARA
• Kwa kuzingatia viwango vya Serikali ngazi ya Mshahara TGOS.A kwa mwezi.


0 comments:

Post a Comment