Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akisalimiana na Mke wa Balozi wa Cuba Nchini Tanzania aliyemaliza muda wake Balozi Ernesto Gomez Diaz nyumbani kwake Mazizini Nje kidogo ya Mji wa Zanzibar.
Balozi wa Cuba Nchini Tanzania aliyemaliza muda wake wa utumishi Bw. Ernesto Gomez Diaz akiwa na Mkewe kulia wakimuaga Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Mazizini nje kidogo ya Mji wa Zanzibar.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akimpongeza Balozi wa Cuba Nchini Tanzania aliyemaliza muda wake Bw. Ernesto Gomez Diaz kwa kazi yake nzuri iliyochangia kuimarika zaidi kwa uhusiano kati ya Cuba na Tanzania.
Zanzibar itaendelea kuwa mshirika mkubwa wa Jamuhuri ya Watu wa Cuba kutokana na Historia ya muda mrefu kati ya Mataifa hayo mawili rafiki tokea Mapinduzi ya Zanzibar ya Mwaka 1964.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi ametoa kauli hiyo wakati alipokuwa akizungumza na Balozi wa Jamuhuri ya Watu wa Cuba Nchini Tanzania Bw. Ernesto Gomez Diaz aliyefika Nyumbani kwake Mazizini nje kidogo ya Mji wa Zanzibar kumuaga baada ya kumalizika muda wake wa utumishi hapa Tanzania.
Amesema Sekta ya Afya Zanzibar kuwa ni miongoni mwa maeneo yaliyopata fursa ya kuimarika Kitaalamu na utendaji kufuatia Mpango wa Wataalamu Mabingwa wa Afya wa Cuba kuwafundisha Madaktari
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar alimpongeza Balozi Ernesto Gomez Diaz kwa juhudi zake za kuendelea kuunganisha nguvu ya uhusiano uliopo kati ya Zanzibar na Cuba.
Balozi Seif amemuahidi Bw. Ernesto Gomez kwamba Wazanzibari watahakikisha wanaendeleza mazuri yote aliyoyaacha Balozi huyo kwa kuyafanyia kazi.
Aidha Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar alimuomba Bw. Ernesto kuwa Balozi mpya wa Tanzania na Zanzibar kwa ujumla atakaporejea nyumbani kwa kuzitangaza fursa za uwekezaji zilizopo Nchini ili Wawekezaji wa Cuba wapate fursa ya kuweka Vitega Uchumi vyao hapa Nchini.
Mapema Balozi wa Jamuhuri ya Watu wa Cuba aliyemaliza muda wake Nchini Tanzania Bw. Ernesto Gomez Diaz alielezea matumaini yake kwamba Mpango wa kufundisha Madaktari Wazalendo chini ya usimamizi wa Madaktari Mabingwa wa Cuba utasaidia kupunguza uhaba wa Madaktari Zanzibar.
0 comments:
Post a Comment