Monday, January 12, 2015

AJIRA HALMASHAURI YA WILAYA YA MAKETE - JAN 2015



AJIRA HALMASHAURI YA WILAYA YA MAKETE - JAN 2015
HALMASHAURI YA WILAYA YA MAKETE

TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI

Mkurugenzi Mtendaji (W) Makete kupitia kibali cha ajira mbadala kilichotolewa na Katibu Mkuu- Utumishi anapenda kuwatangazia wananchi wote wenye sifa za kuweza kuajiliwa kuleta maombi yao ya kazi kama ifuatavyo:-

A. AFISA MTENDAJI KIJIJI III – NAFASI 2
B. MAJUKUMU YA KAZI
(i) Kuwa Afisa Masuuli na MtendajiMkuu wa Serikali ya Kijiji
(ii) Kusimamia utawala bora katika kijiji
(iii) Kusimamia Urinzi na Usalama wa Raia na mali zao
(iv) Kuwa Katibu wa Mikutano na kamati zote za Halmashauri ya Kijiji
(v) Kusimamia, kukusanya na kuhifadhi kumbumbu zote na nyaraka za kijiji

C. NGAZI YA MSHAHARA
Kwa kuzingatia viwango vya Serikali ngazi ya mshahara TGS B kwa mwezi

D. SIFA ZA MWOMBAJI
Wahitimu wa kidato cha nne au sita waliohitimu mafunzo ya Cheti, katika moja ya fani za Utawala, Sheria, Elimu ya Jamii, Usimamizi wa fedha, Maendeleo ya jamiina Sayansi ya Sanaa kutoka Chuo cha Serikali za Mitaa Hombolo, Dodoma au Chuo chochote kinachotambuliwa na Serikali.

E. MASHARTI YA UJUMLA
i. Waombaji wote wawe ni Raia wa Tanzania
ii. Waombaji wote waambatanishe cheti cha kuzaliwa
iii. Waombaji wote wambatanishe na maombi binafsi (CV)
iv. Waombaji waambatanishe picha 1 "Passport Size" ya hivi karibuni na nakala ya vyeti halisi
v. Transcript "Testimonials" na "Provisional Result" au "Statement of Results" havitakubaliwa
vi. Waombaji wawe na umri usiozidi miaka 45 na usiopungua miaka 18

F. MAOMBI YATUMWE KWA:-
Mkurugenzi Mtendaji (W)
Halmashauri ya Wilaya Makete
S.L.P 6
MAKETE

G. MWISHO WA KULETA MAOMBI
Mwisho wa kuleta maombi ni tarehe 30/01/2015 saa 9:30 alasiri. Maombi yote yapelekwe Masjala ta Mkurugenzi (W)


0 comments:

Post a Comment