Thursday, November 13, 2014

Kazi Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu - Nov 2014


Kazi Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu - Nov 2014
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu anawatangazia Nafasi za Kazi
na Watanzania wenye sifa na uwezo wa kujaza Nafasi za kazi kama ifuatavyo:-
Nafasi hizi ni kwa ajili ya Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu.

 Mtendaji Wa Kijiji III ( X 20)
Location > Mbulu

SIFA ZA MWOMBAJI
Kuajiriwa wenye Elimu ya Kidato cha Nne (IV) AU Sita (VI) aliyehitimu mafunzo ya
Astashahada/Cheti katika moja ya fani zifuatazo: Utawala, Sheria, Elimu ya jamii
(Sociology), Usimamizi wa Fedha, Maendeleo ya Jamii na Sayansi ya Sanaa kutoka Chuo
cha Serikali za Mitaa Hombolo, Dodoma au Chuo chochote kinachotambuliwa na Serikali.

MAJUKUMU YA KAZI
Afisa Masuuli na Mtendaji Mkuu wa Serikali ya Kijiji
Kusimamia Ulinzi na Usalama wa raia na mali zao, kuwa Mlinzi wa Amani na Msimamizi
wa Utawala Bora katika Kijiji
Kuratibu na kusimamia upangaji wa utekelezaji wa Mipango ya Maendeleo ya Kijiji.
Katibu wa Mikutano na Kamati zote za Halmashauri ya Kijiji
Kutafsiri na kusimamia utekelezaji wa Sera, Sheria, Kanuni, Taratibu na Miongozo ya
Serikalikatika Kijiji
Kuandaa Taarifa za Utekelezaji wa kazi katika eneo lake na kuhamasisha wananchi katika
kuandaa na kutekeleza mikakati ya kuondoa njaa, umaskini na kuongeza uzalishaji mali;
Kiongozi wa Wakuu wa Vitengo vya Kitaalam katika Kijiji
Kusimamia, kukusanya na kuhifadhi kumbukumbu zote na Nyaraka za Kijiji
Mwenyekiti wa Kikao cha Wataalamu waliopo katika Kijiji
Kupokea, kusikiliza na kutatua matatizo/malalamiko na migogoro ya Wananchi katika Kijiji
Kusimamia Utungaji wa Sheria Ndogo za Kijiji; na
Atawajibika kwa Mtendaji wa Kata

MSHAHARA
Kwa kuzingatia Ngazi za mishahara ya Serikali yaani TGS B kwa mwezi


APPLICATION INSTRUCTIONS:

Mwombaji awe Raia wa Tanzania na awe tayari kufanya kazi sehemu yoyote kwenye kwenye Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu
Mwombaji awe na umri usiozidi miaka 45 na awe hajawahi kupatikana na kosa la jinai au kufungwa jela
Waombaji waambatishe maelezo binafsi yanayojitosheleza (Detailed CV)
Maombi vote yaambatane na nakala za vyeti vya taaluma, vyeti vya elimu (IV au VI), cheti cha kuzaliwa na picha mbili za rangi za hivi karibuni (Passport Size) na iandikwe
jina nyuma.
Testmonials", "Provisional Results", "Statement of results", hati matokeo za
kidato cha nne na sita (FORM IV AND FQRM VI RESULTS SLIPS)
HAVITAKUBALIWA.
Waombaji waliosoma nje ya Tanzania wahakikishe vyeti vyao vimehakikiwa na
kuidhinishwa na Mamlaka husika (TCU na NECTA).
Waombaji waliostaafishwa katika Utumishi wa Umma hawaruhusiwi kuomba
isipokuwa kama wanakibali cha Katibu Mkuu Kiongozi.
Uwasilishaji wa taarifa na sifa za kugushi wahusika watachukuliwa hatua za kisheria.
Maombi yaandikwe kwa mkono na mwombaji mwenyewe na yatumwekupitia posta
kwa anuani ifuatayo.

MKURUGENZI MTENDAJI (W),
HALMASHAURI YA WlLAYA YA MBULU,
S.L.P.74,
MBULU.
Fortunatus H. Fwema
MKURUGENZI MTENDAJI (W)
HALMASHAURI YA WlLAYA YA MBULU

Application Deadline: 28 Nov 2014


0 comments:

Post a Comment