1.5 AFISA UGAVI MKUU DARAJA LA I - NAFASI 1
1.5.2 MAJUKUMU YA KAZI
• Kushauri juu ya Sera ya Ununuzi na Ugavi katika Wakala;
• Kushauri juu ya Mfumo wa Mtandao wa Ununuzi na Ugavi kwa kutumia kompyuta, "e-procurement";
• Kutathmini taarifa ya vifaa vinavyotumika na Wakala ili kujua aina ya kasi ya vifaa husika kwa hatua zaidi;
• Kusimamia utayarishaji wa Mpango wa manunuzi wa Wakala;
• Kusimamia utayarishaji wa makisio ya vifaa vinavyohitajika katika Wakala;
• Kusimamia upimaji wa utendaji wa Maafisa Ugavi walio chini yake;
• Kumshauri Mtendaji Mkuu kuhusu namna bora kutekeleza majukumu yanayohusu ununuzi, utunzaji na ugavi katika Wakala;
1.5.3 SIFA ZA MWOMBAJI
• Kuajiriwa wenye Shahada ya Ugavi na Shahada/Stashahada ya Uzamili katika fani za Biashara au Ugavi kutoka vyuo vinavyotambuliwa na Bodi ya Taifa ya Usimamizi wa Vifaa, na uzoefu wa kazi usiopungua miaka kumi na mbili (12).
1.5.4 MSHAHARA
• Kwa kuzingatia ngazi za mishahara ya Serikali yaani WMAS 7 kwa mwezi
NB: MASHARITI YA JUMLA KWA KAZI ZOTE.
i. Waombaji wote wawe ni Raia wa Tanzania na wenye umri usiozidi miaka 45
ii. Waombaji wote waambatishe cheti cha kuzaliwa.
iii. Waombaji ambao tayari ni watumishi wa Umma na wamejipatia sifa za kuingilia katika kada tofauti na walizonazo, wapitishe barua zao za maombi ya nafasi za kazi kwa waajiri wao na Waajiri wajiridhishe ipasavyo.
iv. Nafasi ya kazi inayoombwa iandikwe juu ya bahasha, kutozingatiwa hili kutasababisha maombi ya kazi kuwa batili.
v. Waombaji waambatishe maelezo binafsi yanayojitosheleza (Detailed C.V) yenye anwani na namba za simu za kuaminika pamoja na majina ya wadhamini (referees) watatu wa kuaminika.
vi. Maombi yote yaambatane na vyeti vya taaluma, maelezo, nakala za vyeti vya kidato cha nne na kidato cha sita kwa wale waliofikia kiwango hicho na vyeti vya kuhitimu
mafunzo mbalimbali kwa kuzingatia sifa za kazi husika. Viambatanisho hivyo vibanwe sawa sawa kuondoa uwezekano wa kudondoka au kupotea.
- Postgraduate/Degree/Advanced Diploma/Diploma/Certificates.
- Cheti cha mtihani wa kidato cha IV na VI
- Computer Certificate
- Vyeti vya kitaaluma (Professional certificates from respective boards)
- Picha moja "Passport size" ya hivi karibuni iandikwe jina kwa nyuma.
vii. Testmonials", "Provisional Results", "Statement of results", hati matokeo za kidato cha nne na sita (FORM IV AND FORM VI RESULTS SLIPS) HAVITAKUBALIWA.
viii. Waombaji waliosoma nje ya Tanzania wahakikishe vyeti vyao vimehakikiwa na kuidhinishwa na Mamlaka husika (TCU na NECTA).
ix. Waombaji waliostaafishwa katika Utumishi wa Umma hawaruhusiwi kuomba isipokuwa kama wanakibali cha Katibu Mkuu Kiongozi.
x. Waombaji kazi ambao tayari ni waajiriwa katika nafasi za kuingilia walioko katika Utumishi wa umma wasiombe na wanatakiwa kuzingatia maelekezo yaliyo katika Waraka Na CAC. 45/257/01/D/140 wa tarehe 30 Novemba 2010.
xi. Uwasilishaji wa taarifa na sifa za kugushi wahusika watachukuliwa hatua za kisheria.
xii. Mwisho wa kupokea barua za maombi ni tarehe14 Octoba, 2014
xiii. Aidha, uwasilishaji wa barua kwa mkono katika ofisi za Sekretarieti ya ajira HAURUHUSIWI.
xiv. Maombi yanaweza kuandikwa kwa Lugha ya Kiswahili au Kiingereza na yatumwe kupitia posta kwa anuani ifuatayo.
Katibu, AU Secretary,
Sekretariati ya Ajira katika Public Service Recruitment
Utumishi wa Umma, Secretariat,
SLP.63100, P.O.Box 63100
Dar es Salaam. Dar es Salaam.
0 comments:
Post a Comment