Saturday, October 4, 2014

AFISA VIPIMO DARAJA LA II- NAFASI 17



AFISA VIPIMO DARAJA LA II- NAFASI 17

1.4 AFISA VIPIMO DARAJA LA II- NAFASI 17
1.4.2 MAJUKUMU YA KAZI
• Kukagua, kuhakiki na kuvirekebisha vipimo vya wafanyabiashara;
• Kutunza na kuhifadhi vifaa vya kitaalamu vitumikavyo katika utendaji wa kazi;
• Kutoa ushauri kuhusu masuala ya uhakiki na matumizi ya vipimo;
• Kufanya upelelezi kuhusu ukiukwaji wa Sheria ya vipimo;
• Kupokea na kufanyia kazi malalamiko ya wadau na wateja;


1.4.3 SIFA ZA MWOMBAJI
• Kuajiriwa mwenye Shahada ya kwanza katika fani ya Legal Metrology au Legal and Industrial Metrology kutoka Chuo kinachotambuliwa na Serikali. Au
• Kuajiriwa mwenye Shahada katika fani ya Uhandisi / Sanyansi ambao wamepata crash programme in Legal and Industrial Metrology isiyopungua miezi mine (4) kutoka Chuo kinachotambuliwa na Serikali. Au
• Kuajiriwa mwenye Shahada katika fani ya Uhandisi / Sayansi ambao wamehitimu Stashahada ya Uzamili (Postgraduate Diploma) katika fani ya Vipimo kutoka Chuo kinachotambuliwa na Serikali.
• Kuajiriwa mwenye Stashahada ya juu katika fani ya Legal Metrology / Legal and Industrial Metrology kutoka Chuo kinachotambuliwa na Serikali.
1.4.4 MSHAHARA
• Kwa kuzingatia ngazi za mishahara ya Serikali yaani WMAS 3 kwa mwezi.

NB: MASHARITI YA JUMLA KWA KAZI ZOTE.
i. Waombaji wote wawe ni Raia wa Tanzania na wenye umri usiozidi miaka 45
ii. Waombaji wote waambatishe cheti cha kuzaliwa.
iii. Waombaji ambao tayari ni watumishi wa Umma na wamejipatia sifa za kuingilia katika kada tofauti na walizonazo, wapitishe barua zao za maombi ya nafasi za kazi kwa waajiri wao na Waajiri wajiridhishe ipasavyo.
iv. Nafasi ya kazi inayoombwa iandikwe juu ya bahasha, kutozingatiwa hili kutasababisha maombi ya kazi kuwa batili.
v. Waombaji waambatishe maelezo binafsi yanayojitosheleza (Detailed C.V) yenye anwani na namba za simu za kuaminika pamoja na majina ya wadhamini (referees) watatu wa kuaminika.
vi. Maombi yote yaambatane na vyeti vya taaluma, maelezo, nakala za vyeti vya kidato cha nne na kidato cha sita kwa wale waliofikia kiwango hicho na vyeti vya kuhitimu
mafunzo mbalimbali kwa kuzingatia sifa za kazi husika. Viambatanisho hivyo vibanwe sawa sawa kuondoa uwezekano wa kudondoka au kupotea.
- Postgraduate/Degree/Advanced Diploma/Diploma/Certificates.
- Cheti cha mtihani wa kidato cha IV na VI
- Computer Certificate
- Vyeti vya kitaaluma (Professional certificates from respective boards)
- Picha moja "Passport size" ya hivi karibuni iandikwe jina kwa nyuma.
vii. Testmonials", "Provisional Results", "Statement of results", hati matokeo za kidato cha nne na sita (FORM IV AND FORM VI RESULTS SLIPS) HAVITAKUBALIWA.
viii. Waombaji waliosoma nje ya Tanzania wahakikishe vyeti vyao vimehakikiwa na kuidhinishwa na Mamlaka husika (TCU na NECTA).
ix. Waombaji waliostaafishwa katika Utumishi wa Umma hawaruhusiwi kuomba isipokuwa kama wanakibali cha Katibu Mkuu Kiongozi.
x. Waombaji kazi ambao tayari ni waajiriwa katika nafasi za kuingilia walioko katika Utumishi wa umma wasiombe na wanatakiwa kuzingatia maelekezo yaliyo katika Waraka Na CAC. 45/257/01/D/140 wa tarehe 30 Novemba 2010.
xi. Uwasilishaji wa taarifa na sifa za kugushi wahusika watachukuliwa hatua za kisheria.
xii. Mwisho wa kupokea barua za maombi ni tarehe14 Octoba, 2014
xiii. Aidha, uwasilishaji wa barua kwa mkono katika ofisi za Sekretarieti ya ajira HAURUHUSIWI.
xiv. Maombi yanaweza kuandikwa kwa Lugha ya Kiswahili au Kiingereza na yatumwe kupitia posta kwa anuani ifuatayo.
Katibu, AU Secretary,
Sekretariati ya Ajira katika Public Service Recruitment
Utumishi wa Umma, Secretariat,
SLP.63100, P.O.Box 63100
Dar es Salaam. Dar es Salaam.


0 comments:

Post a Comment