Mshambuliaji wa Arsenal, Olivier Giroud akishangilia bao lake la dakika ya 23 ya mchezo.
Santi Cazorla wa Arsenal akikwaana na Paulinho (kushoto).
MSHAMBULIAJI wa Arsenal, Olivier Giroud leo amepeleka kilio Tottenham baada ya kuipatia timu yake bao la ushindi katika dakika ya 23 ya mchezo. Giroud aliunganisha krosi safi kutoka kwa Theo Walcott na kuwafanya vijana wa Wenger kuibuka kifua mbele na pointi tatu dhidi ya mahasimu wao Tottenham Hotspur. Mechi hiyo imepigwa katika Uwanja wa Emirates jijini London na Arsenal wameshinda bao 1-0.Katika mtanange huo, vikosi vilikuwa kama ifuatavyo:
Arsenal: Szczesny, Jenkinson, Mertesacker, Koscielny, Gibbs, Ramsey, Wilshere (Flamini 43), Rosicky (Monreal 78), Cazorla, Walcott (Sagna 90)
Tottenham: Lloris; Walker, Dawson, Vertonghen, Rose; Capoue (Sandro 74), Paulinho; Townsend (Lamela 74), Dembele (Defoe 68), Chadli; Soldado
0 comments:
Post a Comment