Monday, August 26, 2013

CCM: Mansour Himid avuliwa uanachama, Sixtus Mapunda amrithi Martine Shigela




CCM: Mansour Himid avuliwa uanachama, Sixtus Mapunda amrithi Martine Shigela
Picture
Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete akiongoza kikao cha NEC, mjini Dodoma leo mchana. Kushoto ni Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana.
HALMASHAURI Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) leo imemaliza kikao chake cha siku tatu chini ya Mwenyekiti wake, Rais Jakaya Kikwete ikiwa imeridhia mapendekezo kadhaa ya Kamati Kuu ya CCM, ikiwemo kumfuta uongozi Mbunge wa jimbo la Mjini Magharibi, Zanzibar,  Mansor Yusuf Himid.

Kufuatia hatua hiyo, CCM itatoa taarifa kwa Spika wa Baraza la Wawakilishi kuondoa udhamini wake kwa mwanachama huyo kama Mjumbe wa Baraza hilo kwa jimbo la Kiembesamaki.

Kikao hicho pia kimeridhia, uteuzi wa Makatibu wateule wapya wa Jumuia za CCM, za Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM), Jumuiya ya Wazazi na Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT).

Hatua hiyo itamfanya Spika wa Baraza hilo kutangaza kiti cha jimbo hilo kuwa wazi na kuitishwa uchaguzi mdogo wa kugombea nafasi hiyo.

Mjumbe wa kamati kuu ya halmashauri kuu ya CCM Taifa Daud, Ismail akizungumza na Zenji FM radio amesema kikao hicho kimefikia uamuzi huo baada ya kupokea madai ya mkoa wa Magharib kutaka
mwanachama huyo afukuzwe kwa madai ya kupinga sera ya Serikali mbili ya Muungano inayoungwa  mkono na CCM. 

Hata hivyo Himid ambaey pia ni mjume wa kamati ya maridhiano Zanzibar, endapo hajaridhishwa na uamuzi wa kufukuzwa kwake anaweza kukata rufaa Mahakama Kuu kupinga uamuzi huo.

Himid aliwahi kuwa Waziri asiekuwa na Wizara ya Maalum katika awamu ya saba ya uongozi inayongozwa na Dk Ali Mohammed Shein. Pia aliwahi kuwa Naibu Waziri wa Wizara ya Kilimo kabla ya kuwa Waziri wa Maji Ujenzi, Nishati na Ardhi katika Utawala wa rais Amani Abeid Karume.

Himid alionekana kichocheo kutaka kuliondoa suala na mafuta na gesi asilia kwenye orodha ya Mambo ya Muungano pamoja na kuchukizwa na matatizo ya Muungano yanayoikandamiza Zanzibar.

Hivi karibuni mwenyekiti wa Kamati ya Maridhiano, Mzee Hassan Moyo alisema kufukuzwa kwa Himid hakutathiri shughuli za Kamati hiyo katika kutetea Muungano wa mkataba.


UTEUZI

Kikao hicho pia kimeridhia, uteuzi wa Makatibu wateule wapya wa Jumuiya za CCM, za Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM), Jumuia ya Wazazi na Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT).

Katika uteuzi huo mapendekezo hayo yaliyofanywa na Kamati Kuu ya CCM na kuridhiwa na NEC, kwa upande wa UVCCM ameteuliwa aliyekuwa Kaimu Katibu wa CCM mkoa wa Morogoro, Sixtus Mapunda na kwa upande wa Jumuia ya Wazazi ni Mjumbe wa NEC kutoka Pemba, Seif Shabani Mohamed, huku kwa upande wa UWT akiachwa Katibu Mkuu wa sasa, Amina Makilagi.

Mapunda atachukua nafasi iliyokuwa imneshikiwa na Martine Shigela ambaye ameongoza UVCCM kwa miaka mitano sasa, na Seif Shabani Mohammed kutoka Pemba akichukua nafasi iliyokuwa ikishikiliwa na Hamis Suleiman Dadi ambaye pia amekuwa katika wadhifa kwa miaka mitano sasa.

Pia, NEC imeridhia mapendekezo  ya Kamati Kuu kwa ajili ya kuziba nafasi Makatibu wa CCM wa mikoa mitatu ya Morogoro, Kaskazini Pemba na Geita ambayo kwa mujibu wa maelezo yaliyotolewa imekuwa wazi kwa muda mrefu sasa kutrokana na sababu mbalimbali ikiwemo kifo.

Kufuatia mapendekezo hayo ya Kamati Kuu, ambayo yameridhiwa na NEC, walioteuliwa na mikoa yao ikiwa kwenye mabano ni Msaidizi Kitengo cha  Uchaguzi, CCM Ofdisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Romuli Rojas John (Morogoro), aliyekuwa Katibu Katibu wa wilaya ya Mkinga, Kassim Mabrouk Mbarak (Kaskazini Pemba) na aliyekuwa Katibu wa CCM Igunga, Mary Maziku (Geita).

Kuhusu sakata la madiwani wa Bukoba mjini, CCM imesema suala hilo, linaendelea kushughulikiwa ambapo baada ya kikao hicho cha NEC, Kamati kuu iliendelea kukutana na viongozi wa wilaya ya Bukoba, Mwenyekiti wa CCM na Katibu wa wilaya hiyo.

Mapema kabla ya kikao cha NEC, Kamati Kuu ilikutana na Mbunge wa Bukoba mjini Khamis Kagasheki na Meya wa Manispaa ya Bukoba mjini na kuwahoji, wakati jana Kamati Kuu ilikutana na  Mwenyekiti na Katibu wa CCM mkoa wa Kagera.

Taarifa Rasmi ya CCM ya majina ya Makatibu wa Wilaya walioteuliwa na NEC

  1. Ndugu Ashura Amanzi
  2. Ndugu Rukia Saidi Mkindu
  3. Ndugu Elias J. Mpanda
  4. Ndugu Jonathan M. Mabihya
  5. Ndugu Mulla Othman Zuberi
  6. Ndugu Jumanne Kapinga
  7. Ndugu Ali Haji Makame
  8. Ndugu Jacob G. Makune
  9. Ndugu Juma A. Mpeli
  10. Ndugu Hawa Nanganjau
  11. Ndugu Abdulrahman Shake
  12. Ndugu Subira Mohamed Ameir
  13. Ndugu Abdallah Shaban Kazwika
  14. Ndugu Juma Bakari Nachembe
  15. Ndugu Josephat Ndulango
  16. Ndugu Rajab Uhonde
  17. Ndugu Abeid Maila
  18. Ndugu Mohamed Lawa
  19. Ndugu Mariam Sangito Kaaya
  20. Ndugu Bakar Lwasa Mfaume
  21. Ndugu Julius Peter
  22. Ndugu Jumanne Kitundu Mginga
  23. Ndugu Mathias Nyombi
  24. Ndugu Mohamed Hassan Moyo

---
Habari hii ni kwa mujibu wa BASHIR NKOROMO akiwa Dodoma NA Zanzibar Islamic New blog 



Related Posts:

  • Various Jobs in Middle East    Integrity Engineer - Pipeline Division ( 3-10 yrs. )Island Falcon Technical ServicesAbu Dhabi - United Arab EmiratesIDENTIFICATION Job Title : Integrity Engineer Division : Pipelines Division PURPOSE T… Read More
  • Middle East JobsChemist ( 5-10 yrs. ) Ras Al Khaimah Cement CompanyUAE - United Arab EmiratesMain duties: • Ensure the implementation of Quality plan to achieve quality control objectives. • Maintaining testing equipments, testing conditi… Read More
  • T.E. Metallurgical Lab R&D - Papua T.E. Metallurgical Lab R&D - PapuaCountry: Indonesia Region: PapuaVacancy Description:The Technical Expert, Metallurgical Lab R&D will assist the national staff in metallurgical and process engineering by mentoring a… Read More
  • Middle East Jobs Laboratory Technicians and Instructors ( 3-10 yrs. )CALEDONIAN COLLEGE OF ENGINEERING Muscat - OmanCaledonian College has over 30 engineering laboratories and seeks laboratory technicians and/or instructors in the followin… Read More
  • Various Mining Post.Process Engineer - Gravity Separation - UKCountry: United KingdomRegion: Devon Vacancy Description:Wolf Minerals are planning to start tungsten mining at Hemerdon near Plymouth in Devon, UK. This open pit mine will produce … Read More

0 comments:

Post a Comment