Monday, October 29, 2012

MAHAFALI YA 14 KIDATO CHA NNE SEKONDARI LOYOLA


 Mgeni rasmi Dk. Mary Mwanjelwa akizindua jarida la shule.
 Mkuu wa Shule hiyo, Dk. Binamungu Mukasa akitoa hotuba yake
 Mgeni rasmi katika mahali hayo, Dk. Mary Mwanjelwa akitoa hotuba yake
 Mbunge wa Viti Maalum (CCM) mkoa wa Mbeya, Dk. Mary Mwanjelwa akimkadhi cheti mmoja wa wanafunzi waliofanya vizuri, David Michael Machuche wakati wa mahafali ya 14 ya Shule ya Sekondari ya Loyola yaliyofanyika jijini Dar es Salaam.
  Mbunge wa Viti Maalum (CCM) mkoa wa Mbeya, Dk. Mary Mwanjelwa akimkadhi cheti, Asinta John Mpesa wakati wa mahafali ya 14 ya Shule ya Sekondari ya Loyola yaliyofanyika jijini Dar es Salaam.
 Mbunge wa Viti Maalum (CCM) mkoa wa Mbeya, Dk. Mary Mwanjelwa akimkadhi cheti mwalimu wa shule hiyo, Sista Anastella wakati wa mahafali ya 14 ya Shule ya Sekondari ya Loyola yaliyofanyika jijini Dar es Salaam.
 David Michael Machuche (katikati) akiwa na wahitimu wenzake
 Baadhi ya wahitimu wa Kidato cha nne wa Shule ya Sekondari Loyola wakiingia kwenye ukumbi wa mahafali shuleni hapo Mabibo jijini Dar es Salaam. (Picha na Habari Mseto Blog)
 Baadhi ya wahitimu wa Kidato cha nne wa Shule ya Sekondari Loyola wakimsikiliza mgeni rasmi wa mahafali ya 14 shuleni hapo.
 Baadhi ya wawakilishi wa Chuo cha St. Paul cha London Uingereza wakisikiliza hotuba ya mgeni rasm, Dk. Mary Mwanjelwa (MP)

NA SALUM MKANDEMBA

UONGOZI wa Shule ya Sekondari ya Loyola, Dar es Salaam, umeshauriwa kuandaa programu maalum ya kuwasomesha wahitimu wa kidato cha nne katika kipindi cha kusubiri matokeo ya kujiunga na kidato cha tano.

Ushauri huo mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam na Mbunge wa Viti Maalum (CCM), Mary Mwanjelwa, katika  mahafali ya 14 ya kidato cha nne shuleni hapo ambako  alikuwa mgeni rasmi.

Mwanjelwa alisema ili kuwajengea wahitimu hao mazingira ya utayari wa masomo ya kidato cha tano, kuna haja ya shule kuandaa ratiba itakayowapa wanafunzi masomo hayo, ili kutopoteza maarifa waliyoyapata shuleni hapo.

Pamoja na hilo, mbunge  huyo aliupongeza uongozi wa Loyola kwa kuifanya kuwa moja ya shule za kupigiwa mfano nchini na kuwataka walimu kuhakikisha wanaendelea kulibakisha juu jina la shule hiyo.

Mwanjelwa akaupongeza uongozi wa shule hiyo chini ya Mkuu wa Shule, Binamungu Mukasa, na kusema akiwa mmoja wa wazazi wa wahitimu hao 182, anatambua kazi kubwa inayofanywa na timu nzima ya walimu shuleni hapo katika kuwajenga vijana kielimu, kiimani na kimaadili.

Katika hotuba yake, Binamungu aliwashukuru wazazi na kusema mafanikio ya kielimu kwa wahitimu hao yametokana na juhudi za pamoja za wao (wazazi), walimu na wanafunzi.

Related Posts:

  • Middle East Jobs Laboratory Manager - Oman ( 5-30plus yrs. )ICP GulfBidbid - Oman One of the leading Contractors in the GCC is seeking a Laboratory Manager for a major Infrastructure Project in Oman. Our client is one of the busiest Contra… Read More
  • Middle East Jobs Senior Lab Technician ( 4-8 yrs. )Lonestar Alpha Laboratories LLC Muscat - Oman• Reporting to Lab Supervisor. • Ensures that all tests are carried out as specified in the Job Orders. • Does sample preparation as per test… Read More
  • Middle East Jobs Petrochemical Engineer ( 1-10 yrs. )S & A Abahsain Co. Ltd. - Chemical Manufacturing Dammam/Khobar/Eastern Province - Saudi ArabiaPetrochemical Engineer • Meet all production parameters. • Capacity realization with… Read More
  • Nafasi za Kazi Serikalini Nyingi mnoVACANCIES ANNOUNCEMENT The Public Service Recruitment Secretariat was established in accordance with section No.29 (1) of the Public Service (Amendment) Act No.18 of 2007. One of the main functions of this organ is to adverti… Read More
  • Middle East JobsLaboratory Techician ( 8-15 yrs. ) Al Maharah Oilfield & Recruitment ServicesAbu Dhabi - United Arab EmiratesVacancy : Laboratory Technician urgently required for Oil & Gas Industry Sector in Abu Dhabi. Requireme… Read More

0 comments:

Post a Comment