Friday, September 21, 2012

WILAYA 40 NCHINI KUPATIWA DAWA ZA KUTIBU UGONJWA WA VIKOPE .

Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Dkt. Hussein Mwinyi akiangalia moja ya boksi la dawa za kutibu ugonjwa wa vikope aina ya Zithromax zilizotolewa na kampuni ya kimataifa inayofanya utafiti na utengenezaji wa Dawa ya PFIZER kutoka  Marekani leo jijini Dar es salaam. Wengine ni Bi. Caroline Roan makamu wa Rais wa kampuni hiyo huduma za jamii (katikati) na Dkt. Peter Mbuji Kaimu Mkurugenzi Idara ya Kinga (kushoto).

Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Dkt. Hussein Mwinyi akiwaonyesha wadau waliohudhuria hafla fupi ya makabidhiano chupa ya dawa ya kutibu ugonjwa wa vikope aina ya Zithromax zilizotolewa na kampuni ya kimataifa inayofanya utafiti na utengenezaji wa Dawa ya PFIZER kutoka  Marekani leo jijini Dar es salaam.

Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Dkt. Hussein Mwinyi akiwa katika picha ya pamoja na wadau waliohudhuria hafla fupi ya makabidhiano ya msaada wa dawa za kutibu ugonjwa wa vikope zilizotolewa na kampuni ya PFIZER leo jijini Dar es salaam.

Na. Aron Msigwa –MAELEZO.

Wilaya 40 nchini zitarajia kunufaika na mkakati wa kutokomeza ugonjwa wa Vikope kufuatia kampuni ya kimataifa inayofanya utafiti na utengenezaji wa Dawa ya PFIZER kutoka  Marekani kupitia mpango wa kimataifa wa kupambana na Ugonjwa wa vikope kuipatia Tanzania msaada wa dawa aina ya Zithromax kwa ajili ya kupambana na ugonjwa huo.

Akizungumza wakati wa makabidhiano ya dawa hizo leo jijini Dar es salaam ,Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Dkt. Hussein Mwinyi amesema kuwa Wizara ya Afya na Ustawi wa jamii kwa kushirikiana na wadau mbalimbali imekua ikifanya mikakati ya kudhibiti ugonjwa wa Vikope na kutoa elimu ya afya kwa jamii juu ya namna ya kupambana na ugonjwa huo.

Amesema  kuwa Wizara ya afya inaendelea  kupambana na magonjwa yaliyosahauliwa ambayo yamekua yakiathiri watu kwa muda mrefu na kuongeza imekua ikisisitiza mbinu mbalimbali za kukabiliana na ugonjwa huo zikiwemo matumizi ya dawa, uboreshaji wa mazingira ,matumizi ya maji safi na salama pamoja na utoaji wa elimu.

Ameongeza kuwa kampuni ya PFIZER kupitia mpango wa Kimataifa wa kupambana na Ugonjwa wa Vikope kwa mwaka 2012 imeipatia Tanzania msaada wa  chupa 239,952 za dawa ya Zithromax  zikiwa katika mfumo wa kimiminika na chupa za vidonge 17,520.

"Ni matumaini yangu kuwa dawa hizi zitatoa msukumo wa kuondoa magonjwa haya kwa sababu tuna mkakati wa jumla wa kutokomeza na kuondoa kabisa ugonjwa huu na matokeo sasa ni mazuri" amesema.

Kuhusu usalama na ubora wa dawa hizo Dkt. Mwinyi amesema kuwa dawa hizo zinakidhi viwango vya kimataifa na zina ubora na usalama kutokana na matumizi yake katika maeneo mbalimbali nchini toka mwaka 1999.

"Nachosema sasa tiba tunayo, ubora na usalama wake ni wa uhakika wananchi msiwe na hofu yoyote kwa sababu dawa hizi hazina madhara" amesisitiza.

Kwa upande wake makamu wa Rais wa upande wa mahusiano na huduma za jamii wa kampuni hiyo Bi. Caroline Roan amefafanua kuwa kampuni yake itaendelea kushirikiana na Tanzania katika kukabiliana na magonjwa mbalimbali ikiwa ni sehemu ya mchango wake kwa jamii.

Bi. Caroline amesema  kuwa toka mwaka 1999 kampuni ya Pfizer imekuwa ikitoa msaada wa wa dawa za kukabiliana na ugonjwa wa Vikope/ Takoma kupitia mpango wa Kimataifa wa kupambana na ugonjwa huo (ITI).

Kampuni ya Pfizer  ambayo imekua ikitoa misaada ya dawa kwenye sekta ya afya nchini toka 1999 ina makao yake nchini Marekani ni miongoni mwa makampuni makubwa duniani yanayofanya kazi za utafiti, utengenezaji na usambazaji wa dawa katika nchi mbalimbali duniani ikiweka msukumo katika kuhakikisha kuwa binadamu mahali popote pale alipo anapata tiba sahihi na huduma bora za afya.


Related Posts:

  • JOB TITLE: Senior Web DeveloperJOB TITLE: Senior Web DeveloperCreates designs and layouts for websites, corporate intranets, email communications, logos, and online interfaces. Also designs materials for Web-based advertising and marketing campaigns. Selec… Read More
  • TANZANIA PETROLEUM DEVELOPMENT CORPORATION VACANCIES (TPDC)TANZANIA PETROLEUM DEVELOPMENT CORPORATION VACANCIES - ACCOUNTS ASSISTANTS - SECRETARY SEND YOUR HAND WRITTEN APPLICATIONS PLUS CV TO MANAGING DIRECTOR TANZANIA PETROLEUM DEVELOPMENT CORPORATION P.O.BOX 2774 DAR ES … Read More
  • Neno la leoHere is your word for today:Verse:           Psalm 40:2 He drew me up from the pit of destruction, and set my feet upon a rock, making my steps secure.- God is the restorer. - No matter how deep or dark the situation is, God … Read More
  • Switzerland's University Scholarships for TanzaniansScholarships 2012/2013 Switzerland is offering a limited number of university scholarships to Tanzanian students for the academic year 2012/2013 for studies at one of Switzerland's 10 Universities and 2 Federal Institutes… Read More
  • IMMEDIATE JOBVACANCIES IN TANZANIA (ICT MANAGER AND MIS MANAGER) ICT Manager –TanzaniaOur client is looking for a dynamic individual to managetheir ICT Infrastructure for the offices throughout Tanzania. The successfulcandidate must be in possession of an MCSE with CCNA being an added ben… Read More

0 comments:

Post a Comment