Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na Mbunge wa Jimbo la Lindi mjini, Salum Baruani, wakati alipowasili kwenye Shule ya Sekondari Mnolela, Lindi kwa ajili ya kuzindua Jengo la Utawala la shule hiyo, juzi Januari 21, 2012, wakati akiwa katika ziara yake ya Mkoa wa Lindi.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akifurahia ngoma ya asili wakati alipowasili kwenye shule ya Sekondari ya Mnolela, alipofika kuzindua Jengo la Utawala la shule hiyo, akiwa katika ziara yake ya Mkoa wa Lindi juzi, Januari 21, 2012.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akifunua kitambaa ikiwa ni ishara ya kuweka jiwe la Msingi katika jengo jipya la Utawala la Shule ya Sekondari Mnolela, iliyopo kijiji cha Luhokwe, wakati akiwa katika ziara yake ya Mkoa wa Lindi juzi Januari 21, 2012.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiongozana na baadhi ya viongozi wa Mkoa wa Lindi, kuelekea kukagua ujenzi wa jengo la Bweni la wasichana shule ya Sekondari ya Kineng'ene, akiwa katika ziara yake ya Mkoa wa Lindi, juzi Januari 21, 2012.
Picha na Muhidin Sufiani-OMR Kwa Hisani ya Global publishers.
0 comments:
Post a Comment