Friday, May 22, 2015

KUITWA KWENYE USAILI UTAKAOANZA TAREHE 25-29 MEI 2015

TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI

Katibu wa  Sekretarieti  ya  Ajira  katika  Utumishi wa  Umma  kwa  niaba
Wizara, Idara zinazojitegemea na Wakala za Serikali (MDAs) anatarajia
kuendesha  usaili  na  hatimaye  kuwapangia  vituo  vya  kazi,  waombaji
kazi watakaofaulu usaili.

Wasailiwa walioitwa kwenye usaili wanapaswa kuzingatia yafuatayo:

1. Ukaguzi  wa  vyeti  utafanyika  saa 1:00 kabla  ya  muda  wa  mtihani  wa
mchujo kuanza.
2.Usaili utaanza saa moja na nusu asubuhi (1:30) na utafanyika mahali
na tarehe kama inavyoonesha katika nafasi husika.
3. Kuja na kitambulisho kwa ajili ya utambuzi mfano: kitambulisho cha
mkazi, kupigia kura, kazi, hati ya kusafirian.k
4.  Kuja  na  Vyeti  Halisi  (original  certificates)  vya  kuanzia  kidato  cha
nne,  sita,  Stashahada,Stashahada  ya  Juu,  Shahada  na  kuendelea
kutegemeana na sifa za mwombaji.
5.  "Testmonials",  "Provisional  Results",  "Statement  of  results",
hatimatokeo  za  kidato  cha  nne  na  sita  (FORM  IV  AND  FORM  VI
RESULTS SLIPS) HAVITAKUBALIWA.
6. Kila msailiwa aje na picha moja (Passport size).
7. Kila msailiwa atajigharamia kwa chakula, usafiri na malazi.
8.Kila msailiwa azingatie tarehe na eneo alilopangiwa kufanyiwa usaili
9.Kila  msailiwa  aje  na  cheti  halisi  cha  kuzaliwa  (Original  Birth
Certificate)
2
10.Kwa  wale  waliosoma  nje  ya  Tanzania  wahakikishe  vyeti  vyao
vimehakikiwa na kuidhinishwa na mamlaka husika (TCU & NECTA)
11.Wale  ambao  majina  yao  hayakuonekana  katika  tangazo  hili
watambue  kuwa  maombi  yao  hayakufanikiwa  na  wasisite  kuomba
tena mara nafasi za kazi zitakapotangazwa.

KUITWA KWENYE USAILI UTAKAOANZA TAREHE 25-29 MEI 2015

0 comments:

Post a Comment