Sunday, January 4, 2015

MHIFADHI MAMBO YA KALE II (CONSERVATORS OF ANTIQUITIES GRADE II) – NAFASI 4



MHIFADHI MAMBO YA KALE II (CONSERVATORS OF ANTIQUITIES GRADE II) – NAFASI 4
Wakala wa Vipimo ni Taasisi (Wakala) ya Serikali iliyochini ya Wizara ya Viwanda na Biashara. Taasisi hii iliundwa kwa mujibu wa Sheria ya Wakala za Serikali Sura Na. 245, mapitio ya mwaka 2002. Wakala wa Vipimo ilianzishwa rasmi tarehe 13 Mei, 2002 kwa amri ya Serikali Na. 194 (Government Order No. 194) na kutangazwa tarehe 17 Mei, 2002. Wakala wa Vipimo ina jukumu la kumlinda mlaji kwa kuhakiki vipimo vyote vinavyotumika katika sekta za Biashara, Afya, Usalama na Mazingira.

8.0 MHIFADHI MAMBO YA KALE II (CONSERVATORS OF ANTIQUITIES GRADE II) – NAFASI 4

Nafasi hii ni kwa ajili ya Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii.

8.1 MAJUKUMU YA KAZI

Kushiriki katika kutunza na kuhifadhi mazingira ya vituo na maeneo ya Mambo ya Kale.

Kushiriki katika kufanya kazi za ukarabati wa majengo

Kushiriki katika kuboresha maeneo yenye umuhimu ya kihistoria.

Kushiriki katika kufanya kazi za ufundi

Kuratibu na kupokea wageni mbalimbali wanaotembelea Vituo vya Mambo ya Kale.

Kushiriki katika kufanya utafiti na uhifadhi.

Kushiriki kuandaa tathmini ya maeneo ambayo yamefanyiwa utafiti na uhifadhi.

Kuratibu ushauri wa kurekebisha vipengele vya Sheria ya Mambo ya Kale.

Kuendesha mafunzo ya Elimu ya Jamii kuhusu masuala ya utafiti na uhifadhi kwa njia ya semina, warsha na vipindi vya radio.

Kushiriki katika kuandaa vipindi vya TV na Radio

Kushiriki katika kuandaa kazi za maabara.

Kushiriki katika kuandaa kumbukumbu za mambo ya kale.

8.2 SIFA ZA MWOMBAJI

Kuajiriwa wenye Shahada/stashahada ya juu ya Sayansi ya Jamii au Sayansi ya Asili, waliojiimarisha (major) katika mojawapo ya michepuo ya Jiologia, elimu ya viumbe, Akiolojia, Anthropolojia, Jiografia, Historia, Paleontolojia au Ethnolojia kutoka Vyuo vinavyotambulika na Serikali.

8.3 MSHAHARA

Kwa kuzingatia viwango vya Serikali ngazi ya Mshahara TGS.D kwa mwezi.

NB: MASHARITI YA JUMLA KWA KAZI ZOTE.

i.       Waombaji wote wawe ni Raia wa Tanzania na wenye umri usiozidi miaka 45

ii.       Waombaji wote waambatishe cheti cha kuzaliwa.

iii.      Waombaji ambao tayari ni watumishi wa Umma na wamejipatia sifa za kuingilia katika kada tofauti na walizonazo, wapitishe barua zao za maombi ya nafasi za kazi kwa waajiri wao na Waajiri wajiridhishe ipasavyo.

iv.       Nafasi ya kazi inayoombwa iandikwe juu ya bahasha, kutozingatiwa hili kutasababisha maombi ya kazi kuwa batili.

v.       Waombaji  waambatishe  maelezo  binafsi  yanayojitosheleza  (Detailed C.V)  yenye

anwani na namba za simu za kuaminika pamoja na majina ya wadhamini (referees) watatu wa kuaminika.

vi.    Maombi yote yaambatane na vyeti vya taaluma, maelezo, nakala za vyeti vya kidato cha nne na kidato cha sita kwa wale waliofikia kiwango hicho na vyeti vya kuhitimu


mafunzo mbalimbali kwa kuzingatia sifa za kazi husika. Viambatanisho hivyo vibanwe sawa sawa kuondoa uwezekano wa kudondoka au kupotea.

-       Postgraduate/Degree/Advanced Diploma/Diploma/Certificates.

-       Cheti cha mtihani wa kidato cha IV na VI

-       Computer Certificate

-       Vyeti vya kitaaluma (Professional certificates from respective boards) 

-       Picha moja "Passport size" ya hivi karibuni iandikwe jina kwa nyuma. 

vii.       Testmonials", "Provisional Results", "Statement of results", hati matokeo za kidato cha nne na sita (FORM IV AND FORM VI RESULTS SLIPS) HAVITAKUBALIWA. 

viii.       Waombaji waliosoma nje ya Tanzania wahakikishe vyeti vyao vimehakikiwa na kuidhinishwa na Mamlaka husika (TCU na NECTA).

ix.       Waombaji waliostaafishwa katika Utumishi wa Umma hawaruhusiwi kuomba isipokuwa kama wanakibali cha Katibu Mkuu Kiongozi.

x.       Waombaji kazi ambao tayari ni waajiriwa katika nafasi za kuingilia walioko katika Utumishi wa umma wasiombe na wanatakiwa kuzingatia maelekezo yaliyo katika Waraka Na CAC. 45/257/01/D/140 wa tarehe 30 Novemba 2010.

xi.       Uwasilishaji wa taarifa na sifa za kugushi wahusika watachukuliwa hatua za kisheria.

xii.       Mwisho wa kupokea barua za maombi ni tarehe 18 Januari, 2015

xiii.      Aidha, uwasilishaji wa barua kwa mkono katika ofisi za Sekretarieti ya ajira HAURUHUSIWI.

xiv.       Maombi yanaweza kuandikwa kwa Lugha ya Kiswahili au Kiingereza na yatumwe kupitia posta kwa anuani ifuatayo.



Katibu,
AU
Secretary,
Sekretariati ya Ajira katika

Public Service Recruitment
Utumishi wa Umma,

Secretariat,
SLP.63100,

P.O.Box 63100
Dar es Salaam.

Dar es Salaam.


0 comments:

Post a Comment