Sunday, February 24, 2013

YANGA NA AZAM KATIKA PICHA LEO TAIFA,REFA AOKOLEWA NA POLISI



Kipa wa Yanga SC, Ally Mustafa 'Barthez' akiwa amedaka mpira mbele ya kiungo wa Azam FC, Humphrey Mieno na nyuma yake ni kiungo mwingine wa timu hiyo, Khamis Mcha 'Vialli', huku beki wake, Kevin Yondan (kushoto) akiwa tayari kutoa msaada katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara jioni ya leo Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam. Yanga ilishinda 1-0.

Wachezaji wa Yanga, kutoka kulia Haruna Niyonzima, Oscar Joshua na Athumani Iddi 'Chuji' wakijadiliana wakati mchezo uliposimama kwa muda ili Barthez atibiwe baada ya kuumia

Mshambuliaji hatari wa Azam FC, Kipre Tchetche raia wa Ivory Coast, akitafuta mbinu za kumtoka beki wa Yanga, Kevin Yondan.

Niyonzima (8) aliyeshikana mikono na Hamisi Kiiza akielekea eneo la mashabiki wa Yanga kushangilia baada ya kufunga

Mabeki; David Mwantika wa Azam mbele akikabiliana na Kevin Yondan wa Yanga

John Bocco akimiliki mpira mbele ya beki wa Yanga, Nadir Haroub 'Cannavaro' 

Mchezaji bora wa mechi ya leo; Haruna Niyonzima akiwa ameupitia mpira miguuni mwa mshambuliaji wa Azam, Seif Abdallah 

Hamisi Kiiza kushoto akigombea mpira na David Mwantika, kulia ni Chuji na Salum Abubakar 'Sure Boy'

Jerry Tegete akipiga shuti huku David Mwantika akiweka mguu

Kipa Ally Mustafa 'Barthez' akiinuka baada ya kutibiwa na Daktari, Nassor Matuzya. Mbele yake ni Yondan akimfuatilia

Simon Msuva akienda chini baada ya kupigwa kwanja na beki wa Azam

Kikosi cha Azam leo 

Kikosi cha Yanga leo

Barthez amelala chini baada ya kuumia, huku mshambuliaji wa Azam, John Bocco 'Adebayor' akizungumza na refa Hashim Abdallah


Niyonzima akimtoka Mieno

Barthez anadondoka na mpira baada ya kuudakia juu

Hamisi Kiiza akimueleza jambo beki wa Azam, Mwantika wakati kipa Mwadini Ally akiwa amelala chini baada ya kuumia. Wengine kushoto ni Didier Kvumbangu na refa Hashim Abdallah

Barthez akiwapanga mabeki wake (hawapo pichani) wakati Azam wanapga mpira wa adhabu

Kavumbangu akipasua ukuta wa Azam

Kiiza kushoto akiwatoka mabeki wa Azam

Chuji akinawa maji kupoza mishipa ya kichwa

Kocha wa Azam, Stewart Hall akitoka uwanjani kinyonge baada ya mechi

Refa Hashim Abdallah akisindikizwa na Polisi kutoka uwanjani baada ya mechi 

Wachezaji wa Azam wakimzonga refa wakimtuhumu kumaliza mechi kabla ya muda

Kocha wa Yanga, Ernie Brandts wa Uholanzi akiwapungia mikono mashabiki wake baada ya mechi

Hamisi Kiiza kulia akigombea mpira na beki Joackins Atudo wa Azam

Msuva akitafuta mbinu za kumtoka beki wa Azam

Joackins Atudo akimuondoa njianui Msuva 

Jerry Tegete akimtoka Salum Waziri wa Azam

Tegete amepiga tik tak mbele ya mabeki wa Azam

Niyonzima akiambaa na mpira mbele ya wachezaji wa Azam

Niyonzima anamtoka Mcha

Niyonzima anamtoka Mcha

Viungo bora; Salum Abubakar 'Sure Boy' wa Azam akigombea mpira na Frank Domayo wa Yanga. Nyuma ni Chuji akiwa tayari kuingilia

Sure Boy anaambaa na mpira pembeni ya Tegete

Frank Domayo akimvisha kanzu Kipre Tchetche

Sure Boy anamtoka Kavumbangu

Sure Boy anawatoka viungo wa Yanga Domayo na Chuji kulia. Mbele ni Yondan(PICHA ZOTE NI KUTOKA BONGOSTAZ.COM

0 comments:

Post a Comment