Sunday, January 4, 2015

MHANDISI DARAJA LA II (MAJI) – WATER RESOURCE WITH GIS ENGINEER – NAFASI 4



MHANDISI DARAJA LA II (MAJI) – WATER RESOURCE WITH GIS ENGINEER – NAFASI 4
Wakala wa Vipimo ni Taasisi (Wakala) ya Serikali iliyochini ya Wizara ya Viwanda na Biashara. Taasisi hii iliundwa kwa mujibu wa Sheria ya Wakala za Serikali Sura Na. 245, mapitio ya mwaka 2002. Wakala wa Vipimo ilianzishwa rasmi tarehe 13 Mei, 2002 kwa amri ya Serikali Na. 194 (Government Order No. 194) na kutangazwa tarehe 17 Mei, 2002. Wakala wa Vipimo ina jukumu la kumlinda mlaji kwa kuhakiki vipimo vyote vinavyotumika katika sekta za Biashara, Afya, Usalama na Mazingira.

MHANDISI DARAJA LA II (MAJI) – WATER RESOURCE WITH GIS ENGINEER – NAFASI 4

Nafasi hizi ni kwa ajili ya Katibu Mkuu Wizara ya Maji.

6.1 MAJUKUMU YA KAZI

Kushughulikia upembuzi yakinifu, usanifu wa ujenzi, uendeshaji na matengenezo ya miundombinu midogo midogo ya usambazaji maji na kushiriki shughuli za upembuzi yakinifu, usanifu, ujenzi, uendeshaji na matengenezo ya miundombinu mikubwa ya ujenzi wa usambazaji maji na usafi wa mazingira.

Kufanyia mapitio taarifa za upembuzi yakinifu na sanifu za ujenzi wa miundombinu ya miradi ya usambazaji maji na usafi wa mazingira.


Kufanyia ukaguzi wa utekelezaji wa ujenzi, uendeshaji na utengenezaji wa miundombinu ya uzalishaji na usambazaji maji na usafi wa mazingira kwa ajili ya kupata ubora unaokusudiwa.

Kushiriki katika kazi ya kupendekeza miradi na kupitia mapendekezo ya miradi (project proposal) ya usambazaji maji na usafi wa mazingira.

Kufanya uchunguzi kuhusu uharibifu wa miundombinu au ajali zinazojitokeza wakati wa utekelezaji wa miradi ya maji na usafi wa mazingira.

Kutayarisha bajeti ya utekelezaji wa shughuli za sekta za maji.

Kusimamia kuratibu na kufuatilia utekelezaji wa ujenzi, uendeshaji na mategenezo ya miundombinu ya miradi ya maji na usafi wa mazingira.

Kukusanya na kutayarisha taarifa mbalimbali za utekelezaji wa shughuli za sekta ya maji kwa ajili ya matumizi ya sekta na kwa ajili ya kujisajili katika bodi ya Wahandisi.

6.2 SIFA ZA MWOMBAJI

• Kuajiriwa wenye Shahada/Stashahada ya juu ya uhandisi wa Maji (Water Resource with GIS) kutoka vyuo vikuu vinavyotambuliwa na Serikali.

6.3 MSHAHARA

• Kwa kuzingatia Ngazi za mishahara ya Serikali yaani TGS E kwa mwezi.

NB: MASHARITI YA JUMLA KWA KAZI ZOTE.

i.       Waombaji wote wawe ni Raia wa Tanzania na wenye umri usiozidi miaka 45

ii.       Waombaji wote waambatishe cheti cha kuzaliwa.

iii.      Waombaji ambao tayari ni watumishi wa Umma na wamejipatia sifa za kuingilia katika kada tofauti na walizonazo, wapitishe barua zao za maombi ya nafasi za kazi kwa waajiri wao na Waajiri wajiridhishe ipasavyo.

iv.       Nafasi ya kazi inayoombwa iandikwe juu ya bahasha, kutozingatiwa hili kutasababisha maombi ya kazi kuwa batili.

v.       Waombaji  waambatishe  maelezo  binafsi  yanayojitosheleza  (Detailed C.V)  yenye

anwani na namba za simu za kuaminika pamoja na majina ya wadhamini (referees) watatu wa kuaminika.

vi.    Maombi yote yaambatane na vyeti vya taaluma, maelezo, nakala za vyeti vya kidato cha nne na kidato cha sita kwa wale waliofikia kiwango hicho na vyeti vya kuhitimu


mafunzo mbalimbali kwa kuzingatia sifa za kazi husika. Viambatanisho hivyo vibanwe sawa sawa kuondoa uwezekano wa kudondoka au kupotea.

-       Postgraduate/Degree/Advanced Diploma/Diploma/Certificates.

-       Cheti cha mtihani wa kidato cha IV na VI

-       Computer Certificate

-       Vyeti vya kitaaluma (Professional certificates from respective boards) 

-       Picha moja "Passport size" ya hivi karibuni iandikwe jina kwa nyuma. 

vii.       Testmonials", "Provisional Results", "Statement of results", hati matokeo za kidato cha nne na sita (FORM IV AND FORM VI RESULTS SLIPS) HAVITAKUBALIWA. 

viii.       Waombaji waliosoma nje ya Tanzania wahakikishe vyeti vyao vimehakikiwa na kuidhinishwa na Mamlaka husika (TCU na NECTA).

ix.       Waombaji waliostaafishwa katika Utumishi wa Umma hawaruhusiwi kuomba isipokuwa kama wanakibali cha Katibu Mkuu Kiongozi.

x.       Waombaji kazi ambao tayari ni waajiriwa katika nafasi za kuingilia walioko katika Utumishi wa umma wasiombe na wanatakiwa kuzingatia maelekezo yaliyo katika Waraka Na CAC. 45/257/01/D/140 wa tarehe 30 Novemba 2010.

xi.       Uwasilishaji wa taarifa na sifa za kugushi wahusika watachukuliwa hatua za kisheria.

xii.       Mwisho wa kupokea barua za maombi ni tarehe 18 Januari, 2015

xiii.      Aidha, uwasilishaji wa barua kwa mkono katika ofisi za Sekretarieti ya ajira HAURUHUSIWI.

xiv.       Maombi yanaweza kuandikwa kwa Lugha ya Kiswahili au Kiingereza na yatumwe kupitia posta kwa anuani ifuatayo.



Katibu,
AU
Secretary,
Sekretariati ya Ajira katika

Public Service Recruitment
Utumishi wa Umma,

Secretariat,
SLP.63100,

P.O.Box 63100
Dar es Salaam.

Dar es Salaam.


0 comments:

Post a Comment