Saturday, December 20, 2014

TANGAZO LA KUITWA CHUONI KWA WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA NA JESHI LA MAGEREZA



TANGAZO LA KUITWA CHUONI KWA WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA NA JESHI LA MAGEREZA
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI
(Jeshi la Magereza)
Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza Tanzania Bara, anawatangazia wafuatao kuwa wamechaguliwa kujiunga na Jeshi la Magereza baada ya kufaulu mitihani ya usaili iliyofanyika kati ya tarehe 10 Desemba, 2014 hadi 17 Desemba, 2014 katika Bwalo Kuu la Maafisa Magereza Ukonga, Jijini Dar es Salaam pamoja na wale wa Kidato cha Nne na Sita waliosailiwa kutoka Kambi mbalimbali za JKT.
Wahusika wote wanatakiwa kuripoti Ofisi za Magereza za Mikoa husika ifikapo tarehe 30 Desemba, 2014 tayari kwa safari ya kwenda Chuo cha Mafunzo ya Awali kilichopo Kiwira Tukuyu Mkoani Mbeya. Mafunzo yatafunguliwa rasmi tarehe 8 Januari, 2015 hivyo mwisho wa kuripoti Chuoni ni tarehe 7 Januari, 2015. Yeyote atakayeshindwa kuripoti kwa tarehe ya mwisho iliyotamkwa kwenye tangazo hili hatapokelewa na atarudishwa kwa gharama zake.
Wahusika wanatakiwa 
kuzingatia mambo yafuatayo:-
i. Vyeti halisi vya masomo na kuzaliwa, vikiwa na nakala 5 za kila cheti,
ii. Picha za rangi(pass-port size) 5 za hivi karibuni,
iii. Fedha taslim Tzs.90,000/=,
iv. Kalamu za wino, kalamu za risasi na madaftari ya kutosha,
v. Chandarua cheupe cha duara ft 31/2, shuka nyeupe mbili, mto wenye foronya nyeupe zisizo na maua/maandishi,
vi. Cheti cha Afya kutoka Hospitali ya Serikali, 
vii. Nguo za kiraia za kutosha, sweta, raba (brown au nyeusi) na soksi, 
viii. Kwa wale wenye kadi za bima za afya waje nazo, na
ix. Kila mwanafunzi atajitegemea kwa nauli ya kwenda.

Tangazo hili linapatikana kwenye Mbao za Matangazo zilizopo Bwalo Kuu la Magereza, tovuti ya Magereza kwa anwani ya www.magereza.go.tz sanjari na blog ya Magereza kwa anwani ya www.magereza.blogspot.com


Imetolewa na Kamishna Jenerali wa Magereza.

J.C. Minja
KAMISHNA JENERALI WA MAGEREZA
Bofya hapo chini kuona majina ya waliochaguliwa kwa mchanganuo ufuatao:-


Related Posts:

  • Senior Facilitators_SWISSCONTACTJob Title : Senior Facilitators Source : The Guardian, June 9, 2011 Requirements : Should possess a Degree in community development or vocational training or education … Read More
  • AccountantJob Title : Accountant Source : Daily News, June 9, 2011 Requirements : Intermediate Accounting qualification from a recognized institution Job Descri… Read More
  • Programme Finance Assistant_UNDPJob Title : Programme Finance Assistant Source : The Guardian, June 9, 2011 Requirements : Secondary education with specialized certification in accounting and finance … Read More
  • Neno la leoHere is your word for today:Verse:           Hebrews 6:13-14 God made a promise to Abraham saying, 'I will certainly bless you richly and I will multiply your descendants.' - God made promises to Abraham.- God kept th… Read More
  • Vita Ya Chadema Na CCM: Tafsiri YanguNdugu zangu, NIONAVYO, kuna  upepo mgumu wa kisiasa unaovuma sasa kwenye nchi yetu. Ndio, upepo mwingine ni mgumu wenye kutingisha matawi ya miti na hata makoti tuyavaayo. Kamata-kamata hii ya sasa  na matumizi ya nguvu ni is… Read More

0 comments:

Post a Comment