Thursday, November 13, 2014

Ajira Halmashauri ya Wilaya ya Serengeti - Nov 2014



Ajira Halmashauri ya Wilaya ya Serengeti - Nov 2014
Dereva wa Mitambo II
Location > Serengeti

SIfA:
Awe amehitimu kidato channe IV
Awe na leseni Daraja la "G' Ya kuendcsha mitambo na ujuzi wa kutunza vyombo mbalimbali vya mitambo hiyo.
Awe na uzoefu wa kuendesha mitambo kwa muda usiopungua saa mia tatu (300) au miezi (3)
bila kusababaisha ajali.
Kuendesha mitambo kikamilifu bila kusimamiwa.
Kuweka vipimo mbalimbali vinavyotakiwa kufuatana na kazi anayofanya na jinsi anavyoelekezwa
na kiongozi wa kazi hiyo.
Kutoa huduma ya kwanza ya matengenezo ya mitambo na pia aweze kutoa maelekezo sahihi ya ubovu wa mitambo anapotakiwa kufanya hivyo.
Kuandika vizuri "Log Sheet' na kuweka kimbula sahihi ya matumizi ya vifaa kwa mfano:- mafuta, grisi na vipuri.

MSHAHARA:
Mshahara wa kuanzia ni kima cha serikali katika ngazi ya TGOS. A kwa mwezi.
 
Katibu Mahsusi III ( X 3 )
Location > Serengeti 

SlFA
Awe amehitimu kidato cha IV.
Awe amehudhuria mafunzo ya uhazili na kufaulu mtihani wa hatua ya tatu.
Awe amefaulu somo la Hati Mkato ya Kiswahili na kiingereza maneno 80 kwa dakika moja.
Awe amepata mafunzo ya Kompyuta kutoka chuo chochote kinachotambuliwa na serikali na
kupata cheti katika program za Windows, Microsoft Office, Internet, Email na Publisher.
KAZI NA MAJUKUMU:
Kuchapa barua, taarifa na nyaraka za kawaida.
Kupokea wageni na kuwasikiliza shida zao na kuwaelekeza sehemu wanapoweza
kushughulikiwa.
Kutunza raarifaj'kumbukumbu za matukio, miadi, wageni, tarehe za vikao, safari za Mkuu wake
na raliba ya kazi zingine zilizopangwa kumuarifu Mkuu wake kwa wakati unaohitajika.
Kutafuta na kumpatia Mkuu wake, majalada, nyaraka au kitu chochote kinachohitajika katika
shughuli za kazi hapo ofisini
Kufikisha maelekezo ya Mkuu wake wa kazi kwa wasaidizi wake na pia kumuarifu kuhusu taalifa
zozote anazokuwa amepewa na wasaidizi hao.
Kupokea majalada, kuyagawa kwa Maofisa walio katika sehemu alipo, kwa kuyakusanya,
kuyatunza na kuyarudisha sehemu zinazohusika.
Kutekeleza kazi zote atakazokuwa amepangiwa na msimamizi wake wa kazi.

MSHAHARA:
Mshahara wa kuanzia ni kima cha serikali katika ngazi ya TGS. B kwa mwezi.

Msaidizi Wa Kumbukumbu II( X2)
Location > Serengeti 
SIFA:
Awe amehitimu kidato cha nne (VI)
Awe na cheti cha utunzaji Kumbukumbu katika mojawapo ya fani za
Masjala na Afya.

MAJUKUMU YA KAZI:
Kutafuta kumbukumbu/nyaraka/mafaili yanayohitajiwa na wasomaji.
Kudhibitisha upokeaji, uandikishaji wa kumbukumbuj'nyaraka.
Kuchambua, kuorodhesha na kupanga kumbukumbu /nyaraka katika makundi kulingana na
somo husika (Classification and boxing) kwa ajili ya matumizi ya ofisi.
Kuweka/kupanga kumbukumbuj nyaraka katika reki (File racks/cabinets) katika
masjala/vyumba vya kuhifadhia kumbukumbu.
Kuweka kumbukumbu (Barua, nyaraka n.k) katika mafaili.

MSHAHARA:
Mshahara wa kuanzia ni kima cha serikali katika ngazi ya TGS. B kwa mwezi.

Mlinzi
Location > Serengeti
SIFA:
Awe amehitimu kidato cha Nne (IV)
Awe amefaulu mafunzo ya Mgambo/Polisi/JKT au mafunzo ya zimamoto kutoka katika Chuo kinachotambuliwa na Serikali.

MAJUKUMU
Kuhakikisha kwamba mali yeyote ya Ofisi inayotolewa Iangoni (nje ya Of is i) ina hati
yaidhini.
Kuhakikisha kuwa mali yote inayoingizwa Iangoni inazo hati za uhalali wake.
Kulinda usalama wa majengo, Ofisi na mali za Ofisi mchana na usiku
Kuhakikisha kwamba milango na madirisha yote yamefungwa ipasavyo mwisho wa
saa za kazi.
Kuhakikisha kwamba wageni wote wanaoingia katika eneo Ia Ofisi wanaidhini ya
kufanya hivyo.
Kupambana na majanga yoyote yatakayotokea katika sehemu ya kazi kama vile moto,
mafuriko, n.k na kutoa taarifa katika vyombo vinavyohusika kama vile Polisi na
zimamoto.
Kutoa ushauri wa jinsi ya kuboresha huduma ya ulinzi mahali pa kazi.

MSHAHARA
Mshahara wa kuanzia ni kima cha Serikali katika ngazi ya TGOS 'A' kwa mwezi

Afisa Mtendaji Wa Kijiji III( X 26)
Location > Serengeti

SlFA:
Awe na Elimu ya kidato cha nne (IV) au sita (VI)
Aliyehitimu mafunzo ya Astashahada/Stashahada katika moja ya fani zifuatazo: Utawala, Sheria,
Elimu ya Jamii, Usimamizi wa fedha, Maendeleo ya Jamii, na sayansi ya sanaa kutoka chuo cha
serikali za mitaa Hombolo, Dodoma au chuo chochote kinachotambuliwa na serikali.

KAZI NA MAJUKUMU
Afisa Masuuli na Mtendaji Mkuu wa Serikali ya kijiji.
Kusimamia ulinzi na usalama wa raia na mali zao.
Kuwa mlinzi wa Amani na Msimamizi, wa utawala bora katika kijiji.
Kuratibu na kusimamia upangaji wa utekelezaji wa mipango ya maendeleo ya kijiji.
Katibu wa mikutano na kamati zote za Halmashauri ya Kijiji.
Kuandaa Taarifa za utekelezaji wa kazi katika eneo lake na kuhamasisha wananchi katika
kuandaa na kutekeleza mikakati ya kuondoa njaa, umaskini na kuongeza uzalishaji mali.
Kusimamia, kukusanya na kuhifadhi kumbukumbu zote na nyaraka za kijiji.
,Mwenyekiti wa kikao cha Wataalamu waliopo katika kijiji.
Kupokea, kusikiliza na kutatua malalamiko na migogoro ya wananchi.
Kusimamia utungaji wa sheria ndogo za kijiji na
Atawajibika kwa Mtendaji wa kata.

MSHAHARA:
Mshahara wa kuanzia ni kima cha serikali katika ngazi ya TGS. B kwa mwezi.

APPLICATION INSTRUCTIONS:

MAELEKEZO YA JUMLA KWA WAOMBAJI WOTE
Kila mwombaji awe na wadhamini wawili wa kuaminika
Kila mwombaji aambatanishe vivuli vya vyeti (Photocopies) vya shule na mafunzo
ya taaluma husika.
Kilamwombaji aambatanishe picha mbili za passport size
Awe na umri usiozidi miaka 45 na awe raia wa Tanzania
Waombaji watakaokidhi sifa wataitwa kwenye usaili
Waombaji watakaoitwa kwenye usaili watatakiwa waje na vyeti halisi (Original
Certificate).
Waombaji waandike anuani zao kwa usahihi na namba zao za simu


Mkurugenzi Mtendaji (W),
Halmashauri ya Wilaya,
S.L.P.176,
Mugumu - Serengeti

Application Deadline: 02 Dec 2014


0 comments:

Post a Comment