Friday, September 5, 2014

MENEJA WA AFYA NA USAFI


MENEJA WA AFYA NA USAFI
From the Mwananchi Newspaper of 5th September
Shirika la Masoko ya Karikaoo ni Shirika la Umma lililoanzishwa kwa mujibu wa Sheria ya Bunge Na.32 ya mwaka 1974 na kupewa majukumu ya kusimamia na kuendesha Soko Kuu la Kariakoo pamoja na Masoko mengine yatakayokuwa chini ya usimamizi wa Shirika pia kujenga Masoko mengine mapya katika Jiji la Dar es Salaam na kusimamia uendeshaji wake. Shirika linakaribisha maombi ya kazi


Meneja wa Afya na Usafi

Sifa
Awe na Shahada ya afya ya umma, Sayansi ya Mazingira au sifa zozote zinazolingana na hizo kutoka Chuo chachote kinachotambulika
na Serikali pamoja na uzoefu wa kazi usiopungua miaka sila (6).
Kazi na Majukumu
• Kuongoza Idara ya Afya na Usafi
• Kubuni, kupendekeza na kutekeleza sera ambazo zitahakikisha kuwa viwango vya ubora wa bidhaa zinatosheleza viwango
vinavyokubalika kisheria.
• Kubuni mipango na kutoa maelekezo ambayo yatahakikisha kuwa Soko linakuwa safi
• Kuhakikisha kuwa hakuna madhara yatakayoweza kuwaathiri watumiaji wa bidhaa za soko la Kariakoo.
• Kubuni mipango ya kuweka Soko katika hali ya usafi iii kuepuka madhara yanayoweza kuwapata watumiaji wa bidhaa za Soko
la Kariakoo.
• Kushauri Meneja Mkuu mambo vote yanayohusu Afya na Usafi katika Soko
• Kusimamia kazi zote zinazohusika na huduma ya Afya ya Umma.
• Kusimamia ubora wa bidhaa zinazouzwa Sokoni.
• Kusimamia usafi wa Soko na mazingira yake.
• Kushauri MeneJa Mkuu wakati wa ununuzi wa vifaa na zana kwa ajili ya Idara ya Afya na Usafi wa Soko.
• Kuandaa Bajeti ya Idara.
• Kufanya kazi zozote kama atakavyoelekezwa na Meneja Mkuu.


APPLICATION INSTRUCTIONS:

Masharti ya Jumla
Muombaji sharti awe raia wa Tanzania
Barua ya maombi, ikiambatishwa na wasifu binafsi pamoja na nakala ya vyeti vya kidato cha nne au sita, mafunzo, cheti cha kuzaliwa.
Nakala moja fiumwe kwa njia ya kawaida "hard copy' na nyingine kwa njia ya mtandao "soft copy' ifumwe kwa andersonshaka@yahoo.com
MENEJA MKUU
Shirika la masoko ya Kariakoo
SLP 15789
DAR ES SALAAM


0 comments:

Post a Comment