Sheikh Ponda anakabiliwa na mashtaka matatu ambayo ni kutotii amri halali iliyotolewa na Mahakama ya Kisutu ya kutokutoa maneno yenye kuharibu imani za dini na kushawishi watu kutenda kosa ambayo anadaiwa kuyatenda Agosti 10, 2013 jioni katika eneo la Kiwanja cha Ndege, Morogoro.
Jana, Sheikh Ponda alifikishwa mahakamani akisindikizwa na polisi waliokuwa na silaha za moto na mabomu ya machozi, huku wafuasi wake wakizuiwa nje ya uzio wa Mahakama hiyo kwa sababu za kiusalama.
Mara baada ya kutajwa kwa kesi hiyo, Hakimu Moyo alisema jalada la kesi hiyo, bado halijarudi kutoka Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam, hivyo kuiahirisha kesi hiyo hadi Mei 26, mwaka huu itakapotajwa tena.
Upande wa mashtaka uliwasilisha ombi mahakamani hapo kutaka Sheikh Ponda kuhojiwa na polisi kuhusiana na mashtaka yanayomkabili. Hakimu Moyo alikubali ombi hilo na kumtaka Sheikh Ponda kuwa na imani na Mahakama hiyo, akisema itatenda haki kwa mujibu wa sheria na si vinginevyo.
MWANANCHI
0 comments:
Post a Comment