Wednesday, May 14, 2014

SAUTI SOL, RADIO &WEASEL, DJ TIRA KUPAMBA ZIARA YA KUHAMASISHA UTOAJI WA TUZO ZA MUZIKI ZA MTV JIJINI DAR KESHO

 
Ikiwa imebaki siku moja kufika ziara ya uhamasishaji wa tuzo za MTV wasanii kutoka sehemu mbalimbali nje ya Tanzania wanatarajiwa wasili jijini Dar es Salaam siku ya kesho kwa ajili ya maandalizi ya sherehe hiyo itakayo fanyika Club Bilicanas.

Wasanii watakao wasili siku ya kesho ni pamoja na Diamond aliyekua Uingereza, Proffesor (Afrika Kusini), Sauti Sol na Amani kutoka Kenya na Radio na weasel wa Uganda ambao wanatarajiwa kupanda jukwaani siku ya Ijumaa ya tarehe 16 Mei ndani ya ukumbi wa club Bilicanas.

Mbali na wasanii hao pia DJ Tira kutoka Afrika Kusini ambae pia ni DJ wa kituo cha Televisheni cha MTV Base nae anatarajiwa kuwasili siku ya kesho kwa ajili ya shughuli hiyo, ataungana na ma DJ wengine wakali kutoka hapa hapa Tanzania ambao watatoa burudani katika sherehe hiyo ya uhamasishaji wa tuzo za MAMA, nao ni pamoja na DJ Zero, DJ Steve B, na DJ Mafuvu.

Sherehe hizo zinalenga kuhamasisha wananchi katika kushiriki kikamilifu katika tuzo hizo na hapa nchini, zitafanyika Club Bilicanas , katika jiji la Dar es Salaam naTiketi zitauzwa mlangoni kwa bei ya shilingi 15,000 kwa mtu moja, mwezi ujao wasanii wataelekea jiji Lagos Nigeria kwa ajili ya uhamasishaji pia.
Vilevile  wasanii  kutoka Afrika Kusini akina mafikizolo na Davido wa Nigeria wamependekezwa kwenye vipengele vingi Zaidi ya moja, wamependekezwa katika vipengele vinne muhimu, hivyo wameumana katika kuwania tuzo za msani bora wa mwaka pamoja na wimbo bora wa kushirikishwa pia.

Pia kutakua na washiriki wawili  ambao ni Radio na weasel wa Uganda , na Kenya msanii Amini kupitia wimbo wake wa kiboko changu alioshirikiana na Radio and Weasel nao utashindanishwa.

MTV leadership ward, ni tuzo inayo lenga vijana wa Afrika wanaume na wanawake wenye umri mdogo mpaka miaka 40 ambao wanafanya vizuri kwenye mambo mbalimbali ikiwemo muziki biashara na science. MTV pia inatambua mafanikio ya muzkik na wana muziki ambao wana wakilisha Afrika nchini na inje ya Afrika.

MAMA 2014 itausisha wasanii  wa Afrika na wa Kimataifa pamoja ikiwa pamoja na tuzo 'sahihi kwa kushirikiana kati ya wasanii wa muziki na tamaduni mbalimbali.

Upigaji kura MTV Africa Awards uko wazi kwenya  www.mtvbase.com kuanzia 16 April 2014 mpaka usiku wa manene  4 Juni 2014.

Kwa maelezo Zaidi juu ya MTV Afrika Muziki Awards kwaZulu –Natal, tembelea tovuti www.mtvbase.com, like us on Facebook at www.Facebook.com/MTVBaseVerified, or follow us on Twitter @MTVBaseAfrica. To join the conversation about the awards please use the hashtag #MTVMAMA.

0 comments:

Post a Comment