Wednesday, May 14, 2014

KATIBU MKUU WA SHIRIKA LA KIMATAIFA LA USAFIRI WA ANGA (ICAO) BW,RAYMOND BENJAMIN AWASILI NCHINI KWA ZIARA YA KIKAZI

 
 
 
 
Waziri wa Uchukuzi Dk. Harrison Mwakyembe akiongozana na Katibu Mkuu wa Shirika la Kimataifa la Usafiri wa Anga (ICAO) Raymond Benjamin baada ya kuwasilia katika Uwanja wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam,kwa ziara ya kikazi nchini kuanzia leo tarehe 14n hadi 18 Mei 2014. Tanzania ni moja ya nchi mbili ikiwemo Ethiopia atakazotembelea katika Kanda ya ICAO .
Waziri wa Uchukuzi Dk. Harrison Mwakyembe watatu kutoka (kushoto) akiwa na wakurugenzi wa Wakuu wa Mamlaka ya Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCCA) wakimsikiliza kwa makini Katibu Mkuu wa Shirika la Kimataifa la Usafiri wa Anga (ICAO) Raymond Benjamin wakati walipokuwa wakibadilishana mawazo baada ya kuwasili nchini kwa ziara ya kikazi kuanzia leo tarehe 14n hadi 18 Mei 2014.
Waziri wa Uchukuzi Dk. Harrison Mwakyembe akiteta jambo na Katibu Mkuu wa Shirika la Kimataifa la Usafiri wa Anga (ICAO) Raymond Benjamin( Kulia) baada ya kuwasilia katika Uwanja wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam, kwa ziara ya Kiakazi hapa nchini.
Waziri wa Uchukuzi Dk. Harrison Mwakyembe wapili kutoka kushoto akiongea wakati alipokuwa akimkalibisha Katibu Mkuu wa Shirika la Kimataifa la Usafiri wa Anga (ICAO) Raymond Benjamin watatu kutoka (kushoto)baada ya kuwasilia katika Uwanja wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam,kwa ziara ya kikazi nchini kuanzia leo tarehe 14n hadi 18 Mei 2014. Tanzania ni moja ya nchi mbili ikiwemo Ethiopia atakazotembelea katika Kanda ya ICAO .
Katibu Mkuu wa Shirika la Kimataifa la Usafiri wa Anga (ICAO) Raymond Benjamin wa tatu kutoka (kulia) akiwa katika picha ya pamoja na Waziri wa Uchukuzi Dk. Harrison Mwakyembe na Viongozi mbalimbali wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania.

0 comments:

Post a Comment