Monday, May 19, 2014

Mkutano wa 67 wa WHA wafunguliwa leo Jijini Geneva,Uswiss

 
 
 
 
Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii,Mh Dkt. Seif Rashid na Waziri wa Afya wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar,Mh. Dkt. Juma Duni wakifuatilia kwa Makini Mkutano wa 67 wa Shirika la Afya Ulimwenguni (WHA) uliofunguliwa leo Jijini Geneva,Uswiss na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Afya Duniani Dr Margareth Chang.Mada kuu ya Mkutano wa mwaka huu ni "The link between climate and health" yaani Uhusiano kati ya mabadiliko ya tabia nchi na Afya.Vile vile pamoja na Mada nyingi zitakazozungumziwa katika Mkutano huu wa siku Sita, Mke wa Rais wa Zambia Dr Christine Kaseba-Sata ambaye ni Balozi maalum wa Shirika la Afya Ulimwenguni (WHO) kuhusu ukatili wa kijinsia na Bi Melinda Gates,Mwenyekiti mwenza wa Bill&Melinda Gates Foundation wata wasilisha mada kuhusu maeneo hayo.
Baadhi ya Wajumbe wa Tanzania wakiandaa mada zitakazo wasilishwa katika Mkutano huu uliofunguliwa leo Jijini Geneva,Uswiss.

0 comments:

Post a Comment