Wednesday, May 21, 2014

KATIBA MPYA TUNAITAKA,LAKINI ISIWE YA KUKOROGA VICHWA VYA WATU - KINANA

 
 
 
 
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akihutubia katika mkutano wa hadhara katika Stendi ya Manyoni, wilayani Manyoni, Singida. "Katiba tunaitaka, lakini isiwe ya  mazingaombwe ya kukoroga vichwa vya watu,ndugu tusitoane macho, tusing'oane meno kwa ajili ya katiba ambayo hata ikija mpya haiwezi kugeuza chai ya rangi kuwa ya maziwa"  alisema Kinana katika mkutano huo.Ndugu Kinana yupo mkoani humo kwa ziara ya siku 8 akitokea mkoani Tabora ambako alikuwa na ziara ya siku 11.
 Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye, akihutubia kwenye mkutano wa hadhara ambao pia ulihudhuriwa na Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana katika Stendi ya Manyoni, willayani Manyoni, Singida . Nape amesema kitendo cha vyama vya upinzani kuunda Ukawa umekirahisishia CCM kuvishambulia vyama hivyo kwa pamoja badala ya kimoja kimoja.
Sehemu ya umati wa watu wakifuatilia yaliyokuwa yakizungumzwa uwanjani hapo.
 Mbunge wa Jimbo la Manyoni Mashariki, Kapteni John Chiligati akiwahutubi wananchi wa mji wa Manyoni mapema kwenye stendi ya mabasi Manyoni.
 Kinana akizindua nyumba Mfugaji huyo ya kisasa kabisa . Kulia ni Mfugaji Mihangwa mmiliki wa nyumba hiyo.
Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana (haonekani pichani) na wajumbe wengine wakitoka nje ya nyumba ya kisasa ya Mfugaji Mihangwa mara baada ya kuikagua,Bwan.Mihangwa aliuza ng'ombe  zake 200 na kubaki  na ng'ombe 100 kwa ajili ya ujenzi wa nyumba hiyo ya kisasa kama ionekanavyo pichani.
 jengo la maabara ya Shule ya Sekondari Heka kama lionekanavyo pichani
  Kinana akisaidia kumpatia tofali fundi wa jengo la maabara ya Shule ya Sekondari Heka wakati wa ziara yake katika Jimbo ya Manyoni Mashariki. Kulia ni Mbunge wa Jimbo la Manyoni Mashariki, Kapteni John Chiligat nae akishiriki kwwenye ujenzi huo.

PICHA NA MICHUZIJR-MANYONI SINGIDA
KWA PICHA ZAIDI BOFYA HAPA

0 comments:

Post a Comment