Wednesday, May 21, 2014

JOTI AJA NA "SANDUKU LA BABU"

 
 
 
 
MSANII wa Komedi Bongo Lucas Mhuvile 'Joti' ametengeneza filamu inayokwenda kwa jina la Sanduku la Babu. Msanii huyo anajivunia aina ya mfumo aliotumia katika kuandaa sinema hiyo kwa kuirekodi na kushiriki katika nafasi zote pekee yake na kuifanya kuwa filamu sawa na iliyoshirikisha wasanii wengi.
Filamu hiyo ambayo inaonekana ni ya maajabu ni kutokana na Teknolojia iliyotumika kwa nafasi zote kuchezwa na mhusika mmoja, ambapo Joti amecheza katika sinema ya Sanduku la Babu kucheza nafasi ya Babu wa Sumbawanga, Bi. Kiboga, Amijee, na kuwashirikisha kidogo wasanii chipukizi.
"Nilikuwa nikifikiria sana kuhusu kuingia katika tasnia ya filamu kwani nilitaka kujua baada ya kutengeneza kazi yangu nitaipeleka wapi? Lakini baada ya kukutana na Proin Promotions nilibaini kuwa hawa wanaweza kufikisha kazi yangu ninapotaka ifike, hivyo ninaiingiza sokoni tarehe 26. May. 2014,"anasema Joti.
Naye msemaji wa kampuni ya Proin Promotion Mr. Evance amesema kuwa kampuni imejipanga kuhakikisha kazi ya Sanduku la Babu inamfikia kila mtu kwani msanii huyo ni kipenzi cha wapenda filamu na vichekesho nchini
Amesema kampuni imejipanga kuwafikishia walaji kwa wakati muafaka.
Joti anasema kuwa kazi hiyo ameiandaa kwa muda wa miaka miwili, kulingana na Teknolojia iliyotumika kwani kila mara ilimpasa baada ya kutengeneza na kuangaliwa na watalaamu kisha kumweleza abadilishe matukio kitu kilichomfanya atumie muda mrefu.
Msanii huyu ambaye anatoka katika kundi mahiri la Orijino Komedi, linaloundwa na wasanii kama Masanja Mkandamizaji, Mac Reagan Kipara, Mpoki Joti na Wakuvanga, pamoja na kutoka na sinema ya Sanduku la Babu bado yupo katika kundi hiyo ni sehemu ya kujiongezea kipato.
MSANII wa Komedi Bongo Lucas Mhuvile 'Joti' akiandaa promo ya "Sanduku la Babu"
MSANII wa Komedi Bongo Lucas Mhuvile 'Joti' akiwa kama Amijee
MSANII wa Komedi Bongo Lucas Mhuvile 'Joti' akiwa kama Bi Kiboga

Related Posts:

  • Institutions of Accountability Specialist Institutions of Accountability Specialist Pamoja Twajenga is a four-year, USAID-funded program designed to provide selected Tanzanian Civil Society Organizations (CSO) and … Read More
  • Research Coordinator (1) Position Research Coordinator (1) Position Columbia University's ICAP Global Health Action in Tanzania, works in partnership with the Ministries of Health and Social Welfare (MOH… Read More
  • VACANT POST FOR EXPERIENCED TOUR CONSULTANTS  VACANT POST FOR EXPERIENCED TOUR CONSULTANTS "Parsalaw, Nenduvoto" <NParsalaw@abercrombiekent.co.tz> Jun 30 01:29PM  ABERCROMBIE & KENT IS LOOKING FOR EXPERIENCED TOUR CONSULTANTS  A… Read More
  • OFFICE ASSISTANT (36 POSTS) OFFICE ASSISTANT (36 POSTS) 7.3 Office Assistant (36 POSTS) 7.3.1 DUTY STATION: Headquarters (5), Dar es salaam (5), Arusha (1), Sumbawanga (2),Iringa (1) Songea (1), Li… Read More
  • RECEPTIONIST (14 POSTS) RECEPTIONIST (14 POSTS) Receptionist (14 POSTS): 7.5.1 DUTY STATION: Headquarters (4) Arusha (1), Dar es salaam (4), Dodoma (1), Shinyanga (1), Mwanza (1), Pwani (1), Ge… Read More

0 comments:

Post a Comment