Arsene Wenger amefarijika kubeba kombe la FA baada ya kuifunga Hull City katika uwanja wa Wembley.
KLABU ya Arsenal ndani ya saa 72 zijazo inatarajia kumpatia Aserne Wenger mkataba wa paundi milioni 24 kwa mwaka na paundi milioni 100 kwa ajili ya usajili baada ya kufanikiwa kuondoa ukame wa miaka 9 bila kombe.
kupitia mtandao rafiki wa Sportsmail inafahamu kuwa Wenger atasaini mkataba wa miaka mitatu ambao utampatia paundi milioni 8 kwa kila msimu.
Pia atapewa hela nyingi zaidi za usajili katika historia ya Asernal ili kusuka kikosi kwa ajili ya kuutafuta ubingwa wa Ligi kuu kwa mara ya kwanza toka mwaka 2004. Maelfu ya mashabiki wa Asernal walijumuika kushangilia ubingwa wa FA kwa mara ya kwanza ndani ya miaka 9.
Baada ya kutwaa ubingwa, Wenger amefanya maamuzi ya kubaki Emirates.
Alipoulizwa kama atasaini mkataba mpya mapema, alisema: "Ndiyo-kwasababu naenda Brazil juni 10".
Wenger atapewa paundi milioni 100 kwa ajili ya usajili. Lengo lake la kwanza ni kumshawishi beki wake wa pembeni Bacary Sagna na mlinda mlango, Lukasz Fabianski ili wabakie klabuni hapo.
Pia anahitaji mshambuliaji mmoja wa kati, kiungo wa ukabaji na beki wa kulia.
Jembe la kazi: Mshambuliaji wa Real Madrid, Karim Benzema (katikati) ndiye chaguo la kwanza kwa Arsenal katika usajili wa majira ya kiangazi.
Wenger pia anavutiwa na kiungo wa Bayer Leverkusen, Lars Bender (kulia)
Mshambuliaji wa Bayern Munich, Mario Mandzukic pia anaivutia Arsenal
0 comments:
Post a Comment