Meja charles Mhagama |
MWENYEKITI wa chama cha Demokrasia na Mendeleo (CHADEMA) Mkoa wa Ruvuma Joseph Fuime amefikishwa katika mahakama ya hakimu mkazi mwandamizi mfawidhi wa Wilaya ya Songea kujibu malalamiko ya kumdhalilisha Meya wa manispaa ya Songea Charles Mhagama kwa kumuita Fisi, nyang'au, beberu na fisadi kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye viwanja vya soko kuu Songea.
Akisoma malalamiko hayo Hakimu mkazi mwandamizi mfawidhi wa mahakama ya Wilaya hiyo Joackim Tiganga alisema kuwa mahakama ilipokea malalamiko toka kwa Mheshimiwa Charles Mhagama meya wa manisapaa ya Songea pia ni diwani wa kata ya Matogoro ambayo yapo kwenye kesi ya madai namba 6 ya mwaka 2014 ya udhalilishaji.
Joseph Fuime |
Hakimu Tiganga alieleza mahakamani hapo kuwa inadaiwa Machi 29 mwaka huu majira ya saa za jioni katika eneo la soko kuu Songea Fuime ambaye pia ni diwani wa kata ya mjini(CHADEMA) akiwa kwenye mkutano wa CHADEMA kwenye jukwaa huku akiwahutubia wanachi alitoa maneno ya kashfa kwa Mhugama kwa kumuita Fisi, nyang'au, beberu na fisadi.
Pia alisema kuwa Fuime anadaiwa kuwa aliwaambia wananchi kwenye mkutano huo wa hadhara ukiona madudu hayo yamevimba mtumbo ujuwe kuwa ndani ya matumbo hayo mnafedha za wananchi ni wala rushwa hivyo ameiomba mahakama itamke kuwa maneno hayo aliyoyatoa Fuime kuwa ni kashfa.
Alieleza zaidi kuwa kutokana na hali hiyo Mhagama amedai fidia ya sh. milioni 100 kwa kumkashfu kumuita fisi, nyang'au, beberu na fisadi, pia amedai fidia ya sh. milioni 30 kwa kumdharilisha kumuita anatumbo kubwa na mla rushwa hivyo na kufanya jumla ya fidia yote kuwa ni sh. milioni 130 pia ameiomba mahakama hiyo gharama za uendeshaji wa kesi arudishiwe na nafuu nyingine yeyote ambayo mahakama itaona inafaa.
Hata hivyo mshitakiwa amekanusha malalamiko hayo hivyo kesi imehairishwa hadi Juni 9 mwaka huu itakapoanza kusikilizwa.
0 comments:
Post a Comment