Thursday, August 22, 2013

Safari ya Mwisho ya Marehemu Nemela Phillip Mangula



Safari ya Mwisho ya Marehemu Nemela Phillip Mangula
Hii ndio safari ya Mwisho ya Dada yetu Nemela Phillip Mangula aliezikwa jana huko Kijijini kwao,Mkoani Njombe na mazishi yake kuhudhuliwa na watu mbali mbali.
Baba mzazi wa Marehemu Nemela,Mzee Phillip Mangula akisoma wasifu wa Marehemu mwanae wakati wa Mazishi yake yaliyofanyika jana huko kijijini kwao,Kushoto ni Mama Mzazi wa Marehemu.
Mjumbe wa Kamati kuu ya CCM ambaye pia ni Waziri wa Nchi ofisi ya Rais mahusiano Uratibu wa sera Mhe. Stephen Wasira akitoa salamu za Chama wakati wa Mazishi hayo.
Baadhi ya viongozi wa Chama,Serikali na Bunge walishiriki mazishi ya Nemela Phillip Mangula huko Mkoani Njombe.
Viongozi wa Chama kutoka kushoto ni Mwenyekiti wa Vijana Taifa Mhe. Sadifa , Mwenyekiti wa Wazazi Taifa Ndg. Bulembo, Mjumbe wa NEC -Temeke Ndg. Magesa na Katibu wa uchumi wa Vijana wakijadiliana mambo muhimu ya Kitaifa huko Mkoani Njombe wakati wa mazishi ya Nemela Phillip Mangula.



0 comments:

Post a Comment