Thursday, August 22, 2013

WAKULIMA WA SHAYIRI BABATI WANUFAIKA NA MSAADA WA PEMBEJEO ZA TBL



WAKULIMA WA SHAYIRI BABATI WANUFAIKA NA MSAADA WA PEMBEJEO ZA TBL
 Mhasibu wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Octaty Minja (kushoto), akioneshwa na mkurugenzi wa kampuni ya Agric Evolution inayomiliki shamba la kuzalisha shayiri katika Kijiji
cha Sigino, Kata ya Sigino, , wilayani Babati, Manyara, .David Bagereza  (wa pili kushoto), ubora wa shayiri ambayo amekuwa akiilima katika shamba hilo lenye ukubwa wa ekari 3000.Kulia ni mwandishi wa habari,Eliya Mbonea. Maofisa wa TBL na wageni wengine wakiwemo waandishi wa habari walitembelea hivi karibuni shamba hilo la shayiri inayotumika kutengenezea bia katika viwanda vya TBL nchini.TBL imekuwa ikiwasaidia pembejeo wakulima  zao hilo.
 Mhasibu wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Octaty Minja (kushoto),akioneshwa na mkurugenzi wa kampuni ya Agric Evolution inayomiliki shamba la kuzalisha shayiri katika Kijiji cha Sigino, Kata ya Sigino, , wilayani Babati, Manyara, .David Bagereza  (wa pili kushoto), ubora wa shayiri ambayo amekuwa akiilima katika shamba hilo lenye ukubwa wa ekari 3000. Maofisa wa TBL na wageni wengine wakiwemo waandishi wa habari walitembelea hivi karibuni shamba hilo la shayiri inayotumika kutengenezea bia katika viwanda vya TBL nchini.TBL imekuwa ikiwasaidia pembejeo wakulima  zao hilo.
 Machine ya kuvuna shayiri ikimwaga shayiri iliyokwishavunwa hivi karibuni katika shamba lenye ekari 3000 la David Bagereza lililopo katika Kijiji cha Sigino, Kata ya Sigino, , wilayani Babati, Manyara, kabla ya kupakiwa kwenye magunia na kusafirishwa kwenda viwanda vya Kampuni ya Bia Tanzania (TBL)  kutengeneza bia. Kampuni ya TBL imekuwa ikiwasaidia pembejeo  wakulima zao hilo.
Wafanyakazi wa shamba la kampuni ya Agric Evolution lililoko katika Kata ya Sigino, Kijiji cha Sigino,wilayani Babati, Manyara,wakiweka shayiri iliyokwisha vunwa kwenye magunia tayari kusafirishwa kwenda kiwanda cha biacha TBL jijini Arusha hivi karibuni.



0 comments:

Post a Comment