Thursday, August 22, 2013

NORA: PIGA UA PENZI LANGU HALIFI



NORA: PIGA UA PENZI LANGU HALIFI

 
STAA wa sinema za Kibongo, Nuru Nassoro 'Nora' amefunguka kuwa licha ya wafitini kulichokonoa penzi lake kwa masengenyo kila kukicha, kamwe hawezi kukata tamaa.

 
Akizungumza na kinasa sauti cha Amani, Nora alisema kwa kipindi kirefu watu wamekuwa wakihoji staili yake ya maisha na penzi lake na mwigizaji Geofrey Kusila huku wakisengenya kuwa litakufa lakini kila wakisema yeye hajali.
"Wengi sana wananisema, wananifuatilia sana maisha yangu. Nawaomba waniache kwani mimi sijazaliwa kwa ajili ya kusemwasemwa.
"Kwanza unanifuatilia maisha yangu ili iweje? Kwa nini usifanye yako ukayaacha yangu. Kupitia hapa najua watakuwa wamenisoma, leo siwataji kwa majina," alisema Nora ambaye mbali na uigizaji anasukuma maisha yake kwa kitega uchumi cha glosari kilichopo maeneo ya Kinondoni, jijini Dar.

0 comments:

Post a Comment