Thursday, August 22, 2013

FAMILIA YA MASOGANGE YAMWACHIA MUNGU



FAMILIA YA MASOGANGE YAMWACHIA MUNGU
 
Agnes Gerald Waya 'Masogange'.
FAMILIA ya Video Queen wa Bongo, Agnes Gerald Waya 'Masogange' inadaiwa kumwachia Mungu ishu ya binti huyo kukamatwa na madawa ya kulevya Julai 5, mwaka huu nchini Afrika Kusini.
Kwa mujibu wa ndugu mmoja wa familia hiyo aliyeomba jina lake lisitiriwe, wameamua kumwachia Mungu ishu hiyo kwani ndiye anayejua ukweli.
"Unajua baba wa Masogange (mzee Gerald Waya) ni mlokole, sasa amekabidhi ishu nzima mikononi mwa Mungu kwa hiyo hayuko tayari kusemasema maneno ambayo hayatakuwa na faida," alisema ndugu huyo.
Habari zinazidi kudai kwamba, mzee huyo aliwahi kuchukizwa na kitendo cha binti yake huyo kujiingiza kwenye sanaa, hadi kuonekana akinengua kwenye muziki.
Hilo liliwahi kubainishwa na Masogange mwenyewe miaka ya nyuma alipohojiwa na gazeti ndugu na hili (Ijumaa) kupitia safu ya Ten Questions (Maswali Kumi) ambapo ilikuwa hivi:
TQ: Inasemekana umetokea kwenye familia ambayo imeiva kidini, walokole, wao wanachukuliaje suala la wewe kuingia kwenye mambo ya kuuza sura tena wakati mwingine kwenye mavazi ya kimitego?
Agnes: Mh! Baba yangu hataki kabisa kusikia mambo ya muziki na niliwahi kukosana naye lakini nalazimisha kwa kuwa ni moja ya ajira.
Jitihada za kumpata baba wa Masogange ziligonga mwamba baada ya namba iliyotolewa na ndugu huyo kutokuwa hewani.
Masogange na nduguye, Mellisa Edward walikamatwa kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Oliver Tambo, Afrika Kusini wakiwa na 'unga' kilo 150 aina ya crystal methamphetamine wenye thamani ya shilingi bilioni 6.8.

0 comments:

Post a Comment