Monday, August 19, 2013

MWANZA YALIPOKEA KWA SHANGWE TAMASHA LA KILI MUSIC TOUR 2012



MWANZA YALIPOKEA KWA SHANGWE TAMASHA LA KILI MUSIC TOUR 2012
Msanii wa Muziki wa Kizazi kipya (Bongo Fleva),Nassib Abdul a.k.a Diamond akiwajibika jukwaani sambamba na madansa wake wakati wa Onyesho Kabambe la Kilimanjaro Tanzania Music Tour 2013,lililofanyika kwenye Uwanja wa CCM Kirumba,jijini Mwanza mwishoni mwa wiki na kuhudhuliwa na maelfu ya wakazi wa Mwanza na mikoa ya Jirani waliokataa kupitwa na Onyesho hilo kabambe.
Mkali wa Ryms afahamikae kama Joseph Haule au ukipenda waweza muita Profesa Jay wa Mitulinga akiwapagawisha vilivyo wakazi wa Jiji la Mwanza waliofurika kwa wingi ndani ya Uwanja wa CCM Kirumba kwenye Onyesho Kabambe la Kilimanjaro Tanzania Music Tour 2013,lililofanyika kwenye Uwanja wa CCM Kirumba,jijini Mwanza mwishoni mwa wiki na kuhudhuliwa na maelfu ya wakazi wa Mwanza
Mwanamuziki bora wa Hip Hop hapa nchini kwa mwaka 2013, Kala Jeremiah akiwarusha mashabiki wake waliofurika kwa wingi katika Uwanja wa CCM Kirumba,jijini Mwanza mwishoni mwa wiki.
Bob Junior na madansa wake.
Mkali wa RnB,Ben Pol akifanya vitu vyake jukwaani.
Ngoooshaaa....... Ngoooshaaaa....Ngooooshaaaaaa....... au ukipenda waweza muita Fareed Kubanda kwa jina alilopewa na Wazazi wake na pia waweza muita Fid Q akikamua vilivyo ndani ya Uwanja wa nyumbani huku shangwe zikitawala uwanjani hapo.
Shangwe tupu zilitawala uwanjani hao.




0 comments:

Post a Comment