Thursday, August 22, 2013

Mgomo unaendelea TAZARA Mbeya: Wafanyakazi, Walinzi na Wastaafu waungana



Mgomo unaendelea TAZARA Mbeya: Wafanyakazi, Walinzi na Wastaafu waungana
WAFANYAKAZI wa Shirika la Reli ya TAZARA Mkoani Mbeya wameingia katika mgomo kwa muda usiojulikana wakishinikiza Uongozi wa Shirika hilo kuwalipa mishahara yao ya miezi mine (4).

Aidha, watumishi hao wapatao zaidi ya 400 pia wamemwomba Waziri Mkuu, Mizengo Pinda kuingilia mgogoro huo kwa kile walichodai kuwa Ahadi ya Waziri wa Uchukuzi, Dk Harrison Mwakyembe aliyoitoa Agosti 3, mwaka huu alipozungumza na wafanyakazi kuwa ameshindwa kuitekeleza.

Wakizungumza na waandishi wa habari katika Ofisi za TAZARA zilizopo Iyunga jijini Mbeya baada ya maandamano yaliyoishia katika Ofisi ya mwajiri, walisema Shirika hilo limeshindwa kuwalipa mishahara tangu mwezi Mei mwaka huu na kusababisha Wafanyakazi kuishi maisha ya taabu.

Walisema madai yao yameanza muda mrefu hali iliyopelekea Waziri Mwakyembe kufika na kuzungumza nao na kuahidi kuwa ifikapo Agosti 22, mwaka huu Menejimenti iwe imelipa mishahara ya watumishi wote ikiwa ni pamoja na kukusanya madeni ya wateja wao yanayofikia Shilingi bilioni 5/-.

Walisema hadi sasa hakuna kilichotekelezwa hali iliyowalazimu kugoma kujishughulisha na kazi yoyote inayohusu TAZARA hadi hapo watakapolipwa mishahara yao au Waziri Mkuu atakapoingilia na kutatua madai yao. Bofya hapa kusoma habari nzima (na picha zaidi) kwenye Mbeya Yetu blog



0 comments:

Post a Comment