Thursday, August 22, 2013

Wahudumu wa zahanati watuhumiwa kufanya ngono na wagonjwa


Wahudumu wa zahanati watuhumiwa kufanya ngono na wagonjwa
Watumishi wawili katika zahanati ya Mwanhala wilayani Nzega, wamekumbwa na kashfa ya kufanya mapenzi na wagonjwa hospitalini.

Kutokana na kashfa hiyo, Mkuu wa Wilaya ya Nzega, Bitun Msangi, ameiagiza Halmashauri ya Wilaya ya Nzega, kuchukua hatua kali za kinidhamu kwa watumishi hao.

Agizo la mkuu huyo limetolewa hivi karibuni, baada ya Diwani wa kata ya Utwigu, Sawaka Shita kuwalalamikia watumishi hao mbele ya Baraza la Madiwani, kwa kukithiri kufanya mapenzi na wagonjwa nyakati za kazi, licha ya kuonywa kwa mara kadhaa.

Diwani huyo aliliambia baraza hilo kuwa vitendo hivyo vinahatarisha maisha ya watumishi hao  na ya 
wananchi, hususani waliotembea nao na kutishia kuvunja ndoa za wananchi.

Alidai kuwa taarifa hizo za malalamiko, zilishafika katika ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji, tayari kwa utekelezaji, lakini  wananchi wa kata hiyo walitaka kuifunga zahanati hiyo, baada ya kukithiri vitendo hivyo vya kufanya mapenzi katika wodi zilizopo.

Aliomba baraza liwahamishe na kuwachukulia hatua kali za kinidhamu  watumishi hao, ambapo majina yao yamehifadhiwa kwa usalama wao, huku jitihada za kuwachukulia hatua  zikifanyika.

Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo, Patric Mbozu alisema  suala hilo ni la hatari na linapaswa kufuatiliwa kwa umakini ili lipatiwe ufumbuzi na  wananchi waendelee kupatiwa huduma za tiba.

Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri hiyo, Abraham Mdeme alikiri kupokea malalamiko hayo na kuahidi kuwa suala hilo, litafuatiliwa mapema ikiwemo kuwahamisha kwa kufuata taratibu zilizopo.

Mkuu wa Wilaya ya Nzega, Msangi alisema watumishi hao, wamevunja maadili ya afya, hususani kufanya ngono katika wodi za zahanati kwa nyakati za kazi. --- Ziro99 blog



0 comments:

Post a Comment