Mkuu wa Wilaya ya Chamwino Bi. Fatuma Ally akizungumza machache wakati wa uzinduzi rasmi wa ufugaji wa kuku wa kibiashara kwa Chama kimoja cha ushirika Chenye wanachama wasiopungua mia mbili ambacho tayari kimeundwa na wakazi wa wilaya hiyo.
Baadhi ya Wadau wa Chama hicho wakifatilia maelezo wa Mkuu wa Wilaya
Na Abdulaziz Video,Chamwino.
Mkuu wa Wilaya ya Chamwino Bi. Fatuma Ally amezindua rasmi ufugaji wa kuku kibiashara wilayani humo kwa Chama kimoja cha ushirika Chenye wanachama wasiopungua mia mbili ambacho tayari kimeundwa wilayani humo.
Mkutano huo wa aina yake uliokutanisha baadhi ya viongozi,Mabenki,NGOS,wakulima,wafugaji,Wenye maduka,mama Ntilie,Wenye mabucha,wachuuza kuku,Wenye hoteli,Wenye mashine za kusaga na kukamua mafuta na wataaalamu wa mifugo .
Mkutano huo uliokuwa katika sura yenye kuonyesha bayana dhana ya " SMARTPARTNERSHIP ambapo Wananchi wa wilayani Chamwino mkoani Dodoma wamehimizwa kuwekeza kwenye ufugaji kuku wa asili ili waweze kukabilina na baa la njaa linalosababishwa na mabadiliko ya tabia ya nchi.
Akifungua mkutano wa wadau wa ufugaji kuku wilayani humo,Mkuu wa Wilaya hiyo Fatma Ally alisema ufugaji bora wa kuku wa asili unao nafasi kubwa ya kukwamua jamii kiuchumi ambapo wananchi wa wilaya hiyo kuweza kujiwezesha kujitosheleza kwa chakula kwa ufugaji kuku ili kuziba pengo la ukame kwa kuwa wananchi wataweza kununua chakula cha kutosha kwa mahitaji ya kaya zao.
"Wilaya yetu inakabiliwa na ukame ambao hata mtama hauwezi kustawi…wananchi hawanabudi kuwekeza kwenye uzalishaji wa kuku ili kipato kitokanacho na ufugaji huo kiweze kutumika kununua chakula " alisema Ally.
Aliongeza kuwa "Mkutano huu unalenga kuwaktanisha wazalishaji na walaji ili kurahisisha masoko…ili kuhakikisha soko haliyumbishwi na walanguzi tutaunda ushirika wa wafugaji kuku utakaosimamia soko hilo katika wilaya yetu ".
Awali mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya hiyo, Adrian Jungu alisema tayari halmashauri yake imenunua majogoo 3400 wa kisasa na wamegaiwa kwa wafugaji wilayani humo ili kurahisisha ufugaji sambamba na ufugaji bora wa kuku wa asili.
"Hadi sasa wilaya inakadiriwa kuwa na kuku 350,000,tunaweza kuzalisha zaidi na kuwa mkombozi wa kipato cha wananchi wetu ambao wanalazimika kujitosheleza kwa chakula kutokana na ukame" alisema Jungu na kufafanua kuwa "Ili kurahisisha ufugaji huo, wananchi tunawahamasisha wajiunge kwenye vikundi mbalimbali, viwepo vya utengenezaji chakula cha kuku, kutotolesha vifaranga, kutibu magonjwa na vya masoko nasi kuwaunga mkono.
0 comments:
Post a Comment