WIZARA YA VIWANDA NA BIASHARA
TAARIFA KWA UMMA
UTEUZI WA WAJUMBE WA BODI YA SHIRIKA LA VIWANGO TANZANIA TBS
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, amemteua Prof. CUTHBERT F. MHILU, Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar Es Salaam kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Viwango Tanzania, TBS kuanzia tarehe 18 Februari, 2013.
Kufuatia uteuzi wa Mwenyekiti wa bodi, Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Dkt. Abdallah Omary Kigoda (Mb), ameteua Wajumbe kumi na moja wa Bodi hiyo. Wajumbe walioteuliwa na mahali wanapotoka ni kama ifuatavyo.
S/N | JINA | TAASISI ANAKOTOKA |
01. | Bw. Geofrey Simbeye | Mwakilishi wa TPSF |
02. | Bi. Fatma Riami Diwani | Mwakilishi wa Viwanda Vidogo na Vya kati |
03. | Bw. Michael Kamba | Mwakilishi wa Mwanasheria Mkuu wa Serikali |
04. | Dkt. Pamela L. Sawa | Mwakilishi wa Wizara ya Afya |
05. | Bi. Magdallena Utouh | Mwakilishi wa Tume ya Ushindani |
06. | Bw. Jasson B.B Bagonza | Mwakilishi wa Wizara ya Fedha |
07. | Bw. Juma Rajabu | Mwakilishi wa Umoja wa wajumbe wenye uelewa wa masuala ya Viwango |
08. | Bw. Rashid A. Salum | Mwakilishi wa Umoja wa wajumbe wenye uelewa wa masuala ya Viwango, Zanzibar |
09. | Prof. Ntegua Mdoe | Mwakilishi Vyuo vya Elimu ya Juu |
10. | Dkt. Fidea L. Mgina | Mwakilishi wa Wizara ya Viwanda na Biashara |
11. | Bw. Leandry Kinabo | Kaimu Mkurugenzi Mkuu |
Uteuzi wa wajumbe hawa, unaanza mara moja.
Imetolewa na Wizara ya Viwanda na Biashara
S.L.P 9503
DAR ES SALAAM.
0 comments:
Post a Comment