By News
Wadau wa masuala ya elimu na wabunge wanataka suala la mgomo wa walimu, madai ya wanafunzi na hatma ya sekta ya elimu lijadiliwe kwa dharura bungeni.
Kwa mujibu wa Mbunge wa Ubungo, John Mnyika , wanafunzi na wadau wengine wa elimu wanataka Bunge lipewe fursa ya kutimiza wajibu wake wa kikatiba kuisimamia serikali itekeleze madai ya walimu na kuepusha athari za migogoro inayoendelea mashuleni.
Mnyika amedai kuwa suala la yatokanayo na mgomo wa walimu hususani hali tete ya sekta ya elimu kwenye shule za umma haliko mahakamani, kilichopo mahakamani ni mgogoro kati ya Chama cha Walimu Tanzania (CWT) na serikali kuhusu madai ya walimu.
Amefafanua kuwa masuala yanayosubiri uamuzi wa mahakama ambayo yamewekewa masharti kwa mujibu wa kanuni 64 (1) (c) yanaweza kuruhusiwa kujadiliwa bungeni kwa muongozo na utaratibu utakaowezesha majadiliano kufanyika bila kuingilia uhuru wa mahakama kwa kuzingatia kanuni ya 5 (1) ya Kanuni za Kudumu za Bunge.
Mnyika amesisitiza uwa masuala yanayosubiri uamuzi wa mahakama ambayo yamewekewa masharti kwa mujibu wa kanuni 64 (1) (c) yanaweza kuruhusiwa kujadiliwa bungeni kwa muongozo na utaratibu utakaowezesha majadiliano kufanyika bila kuingilia uhuru wa mahakama kwa kuzingatia kanuni ya 5 (1) ya Kanuni za Kudumu za Bunge
WaNafunzi wakiwa darasani huku walimu wakiwa kwenye mgomo jijini Dar ers Salaam leo.PICHA;ROMI

0 comments:
Post a Comment