Wednesday, August 8, 2012

KATIBU MKUU KIONGOZI BALOZI SEFUE ATEMBELEA HAZINA NANENANE DODOMA.


Mkuu wa kitengo cha Menejimenti ya Mikataba kutoka Wakala wa Huduma ya Ununuzi Serikalini [GPSA]  Mordecai Matto (kulia) akitoa maelezo kwa Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue(kushoto) mjini Dodoma juu ya kudhibiti matumizi mabaya ya fedha za umma yaliyokuwa.

Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue (wa pili kulia)  akisamiliana na watumishi na Chuo Cha Usimamizi wa Fedha (IFM)Mchambuzi wa Mifumo ya Komputya Ibrahim Sultan (katikati) na Afisa Taalum Mwandamizi Mkiramwene Msafiri(kushoto) mjini Dodoma alipotembelea banda la Wizara ya Fedha kwenye maonyesho ya wakulima ya nanenane mjini Dodoma.

Mchumi Mwandamizi Idara ya Bajeti Wizara ya Fedha Adam Msumule ( wa pili kushoto)  akitoa maelezo kwa Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue(mwenye miwani) jinsi wanavyoelimisha wananchi juu ya uchambuzi wa bajeti kwa njia rahisa ili waweze kujua mapato na matumizi ya serikali kwa mwaka husika  wa fedha wakati Kiongozi huyo Mwandamizi wa serikali alipotembelea banda la Wizara ya Fedha kwenye maonyesho ya wakulima ya nanenane mjini Dodoma.

Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue(kulia)  akisaini kitabu cha wageni  mjini Dodoma alipotembelea banda la Wizara ya Fedha kwenye maonyesho ya wakulima ya nanenane mjini Dodoma kuona shughuli mbalimbali za Wizara hiyo katika maonyesho ya nanenae.Kushoto ni Afisa kutoka Wizara ya Fedha Ramadhan Omary.(Picha na Hazina).




0 comments:

Post a Comment