Mwanafunzi wa darasa la saba Shule ya Msingi Hogolo, wa umri wa miaka 14 (jina limehifadhiwa) ambaye ni Mkazi wa Mtaa wa Ikulu Kijiji cha Hogolo wilayani Kongwa ameuawa kwa kunyongwa na kuzikwa kwenye shimo nyuma ya nyumba yao karibu na choo baada ya kubakwa.
Uchunguzi wa awali unaonesha kuwa chanzo cha mauaji hayo yaliyofanyika Jumamosi iliyopita ni wivu wa kimapenzi kwani marehemu enzi za uhai wake, anadaiwa alikuwa amevunja uhusiano na mpenzi wake wa muda mrefu, Heri Aboubakar na kuanzisha uhusiano mpya na Wilfredy Muhaha maarufu Kabo.
Hata hivyo bado haijafahamika muuaji halisi wa marehemu huyo licha ya polisi kuwashikilia watu kadhaa kwa tuhuma za kuhusika na tukio hilo akiwemo mpenzi wake wa sasa, Muhaha.
Mbali na Muhaha wengine wanaoshikiliwa Polisi ni Ashad Jafari ambaye ni mkulima na mkazi wa Mtaa wa Nyerere Hogolo ambaye ni rafiki wa marehemu na Rino Mazoea, mkulima na mkazi wa Ikulu Hogolo wilayani Kongwa ambaye ni kaka wa marehemu.
Kamanda Zelothe Steven alisema wanamtafuta Aboubakar ambaye amekimbia kijijini hapo na hajulikani alipo mpaka sasa. Katika tukio hilo, kaka wa marehemu ambaye pia anashikiliwa Polisi, katika maelezo yake ya awali alidai kusikia purukushani zikitokea usiku wa tukio hilo la mauaji lakini hakutoka usiku huo kushuhudia nini kinaendelea.
Marehemu alikuwa akiishi na babu na bibi yake hapo kijijini na siku ya tukio , walezi hao, walikuwa wameondoka kwenda katika vijiji vya jirani, ambapo bibi yake alikuwa amekwenda Kongwa kwa ajili ya kujengea makaburi na babu yake alikwenda Kijiji cha Banyi Banyi kutembelea wagonjwa.
Source: HabariLeo

0 comments:
Post a Comment