Wednesday, August 1, 2012

ASSAH MWAMBENE ATEULIWA KUWA MKURUGENZI MKUU MPYA WA IDARA YA HABARI, MAELEZO.


Wizara ya Habari, Vijana Utamaduni, hii leo imetangaza uteuzi wa Assah Mwambene, kuwa Mkurugenzi Mkuu mpya wa Idara ya Habari, Maelezo.

Taarifa iliyotolewa leo hii na Wizara hiyo imesema uteuzi huo umeanza mwezi mwezi uliopita ambapo anachukua nafasi iliyokuwa imeachwa wazi na Clement Mshana ambaye mwaka jana aliteuliwa kuwa Mkurugenzi wa Shirika la Utangazaji Tanzania, TBC.

Kabla ya uteuzi huo, Mwambene alikuwa Kaimu Mkuu wa kitengo cha mawasiliano Serikalini katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, pia aliwahi kufanya kazi katika kampuni ya magezeti ya Serikali, TSN.


taarifa via TBC, saa saba mchana.

0 comments:

Post a Comment