Sunday, January 4, 2015

MHANDISI UJENZI (CIVIL ENGINEER)-(NAFASI 25)




MHANDISI UJENZI (CIVIL ENGINEER)-(NAFASI 25)
MKUFUNZI DARAJA LA II- MHANDISI UJENZI (CIVIL ENGINEER)-(NAFASI 25) Nafasi hii ni kwa ajili ya Katibu Mkuu Wizara ya Maendeleo ya Jamii,Jinsia na Watoto. Wahandisi hawa watafanya kazi ya kufundisha somo la Ujenzi, computer Application na technical drawing katika vyuo (24) vya maendeleo ya Wananchi na chuo cha Maendeleo ya Jamii Missungwi 27.1 MAJUKUMU YA KAZI • Kufundisha somo la uungaji vyuo, computer application na Technical drawing katika vyuo vyuo vya maendeleo ya wananchi. • Kutayarisha mpango wa kazi wa Mafunzo • Kupima Maendeleo ya Wanachuo katika nadharia na vitendo • Kutunza vifaa vya kufundishia • Kufanya na kutoa taarifa za Utafiti • Kutoa Ushauri wa kitaalam • Kuandaaa kanuni na taratibu za kusimamia Mitihani chuoni • Kutunga na kusahihisha Mitihani • Kufanya Utafiti utakaosaidia kutoa majibu kwa matatizo/changamoto mbaimbali katika jamii inayoizunguka chuo • Kutoa ushauri juu ya kuboresha taaluma chuoni na kuendeleza Mafunzo nje ya chuo 27.2 SIFA ZA MWOMBAJI • Kuajiriwa wahitimu wa kidato cha Nne/sita waliofuzu Mafunzo ya Shahada/ stashahada ya juu katika fani ya uhandisi majengo(Civil Engeneering), Uunga vyuma, computer application and technical drawing kutoka katika vyuo vinavyotambuliwa na Serikali 27.3 MSHAHARA Kwa kuzingatia Ngazi za mishahara ya Serikali yaani TGS D/E kwa mwezi.

NB: MASHARITI YA JUMLA KWA KAZI ZOTE.

i.       Waombaji wote wawe ni Raia wa Tanzania na wenye umri usiozidi miaka 45

ii.       Waombaji wote waambatishe cheti cha kuzaliwa.

iii.      Waombaji ambao tayari ni watumishi wa Umma na wamejipatia sifa za kuingilia katika kada tofauti na walizonazo, wapitishe barua zao za maombi ya nafasi za kazi kwa waajiri wao na Waajiri wajiridhishe ipasavyo.

iv.       Nafasi ya kazi inayoombwa iandikwe juu ya bahasha, kutozingatiwa hili kutasababisha maombi ya kazi kuwa batili.

v.       Waombaji  waambatishe  maelezo  binafsi  yanayojitosheleza  (Detailed C.V)  yenye

anwani na namba za simu za kuaminika pamoja na majina ya wadhamini (referees) watatu wa kuaminika.

vi.    Maombi yote yaambatane na vyeti vya taaluma, maelezo, nakala za vyeti vya kidato cha nne na kidato cha sita kwa wale waliofikia kiwango hicho na vyeti vya kuhitimu



mafunzo mbalimbali kwa kuzingatia sifa za kazi husika. Viambatanisho hivyo vibanwe sawa sawa kuondoa uwezekano wa kudondoka au kupotea.

-       Postgraduate/Degree/Advanced Diploma/Diploma/Certificates.

-       Cheti cha mtihani wa kidato cha IV na VI

-       Computer Certificate

-       Vyeti vya kitaaluma (Professional certificates from respective boards) 

-       Picha moja "Passport size" ya hivi karibuni iandikwe jina kwa nyuma. 

vii.       Testmonials", "Provisional Results", "Statement of results", hati matokeo za kidato cha nne na sita (FORM IV AND FORM VI RESULTS SLIPS) HAVITAKUBALIWA. 

viii.       Waombaji waliosoma nje ya Tanzania wahakikishe vyeti vyao vimehakikiwa na kuidhinishwa na Mamlaka husika (TCU na NECTA).

ix.       Waombaji waliostaafishwa katika Utumishi wa Umma hawaruhusiwi kuomba isipokuwa kama wanakibali cha Katibu Mkuu Kiongozi.

x.       Waombaji kazi ambao tayari ni waajiriwa katika nafasi za kuingilia walioko katika Utumishi wa umma wasiombe na wanatakiwa kuzingatia maelekezo yaliyo katika Waraka Na CAC. 45/257/01/D/140 wa tarehe 30 Novemba 2010.

xi.       Uwasilishaji wa taarifa na sifa za kugushi wahusika watachukuliwa hatua za kisheria.

xii.       Mwisho wa kupokea barua za maombi ni tarehe 18 Januari, 2015

xiii.      Aidha, uwasilishaji wa barua kwa mkono katika ofisi za Sekretarieti ya ajira HAURUHUSIWI.

xiv.       Maombi yanaweza kuandikwa kwa Lugha ya Kiswahili au Kiingereza na yatumwe kupitia posta kwa anuani ifuatayo.



Katibu,
AU
Secretary,
Sekretariati ya Ajira katika

Public Service Recruitment
Utumishi wa Umma,

Secretariat,
SLP.63100,

P.O.Box 63100
Dar es Salaam.

Dar es Salaam.


0 comments:

Post a Comment