Sunday, January 4, 2015

FUNDI SANIFU MSAIDIZI (UPIMAJI ARDHI) - (ASSISTANT WATER WORKS TECHNICIAN GEOMETRIC) – NAFASI 24


FUNDI SANIFU MSAIDIZI (UPIMAJI ARDHI) - (ASSISTANT WATER WORKS TECHNICIAN GEOMETRIC) – NAFASI 24
Wakala wa Vipimo ni Taasisi (Wakala) ya Serikali iliyochini ya Wizara ya Viwanda na Biashara. Taasisi hii iliundwa kwa mujibu wa Sheria ya Wakala za Serikali Sura Na. 245, mapitio ya mwaka 2002. Wakala wa Vipimo ilianzishwa rasmi tarehe 13 Mei, 2002 kwa amri ya Serikali Na. 194 (Government Order No. 194) na kutangazwa tarehe 17 Mei, 2002. Wakala wa Vipimo ina jukumu la kumlinda mlaji kwa kuhakiki vipimo vyote vinavyotumika katika sekta za Biashara, Afya, Usalama na Mazingira.

FUNDI SANIFU MSAIDIZI (UPIMAJI ARDHI) - (ASSISTANT WATER WORKS TECHNICIAN GEOMETRIC) – NAFASI 24

Nafasi hizi ni kwa ajili ya Katibu Mkuu Wizara ya Maji.

2.1 MAJUKUMU YA KAZI

Kufanya kazi kwa kuongozwa na chini ya uangalizi wa Fundi Sanifu aoyesajiliwa ili aweze;

Kushirikiana na Wahandisi wa Maji na kuwaongoza walengwa katika kuchagua njia za kupitisha bomba kwa ajili ya miradi ya maji na usafi wa mazingira;

Kupima hali ya kijiografia ya maeneo ya inayokusudiwa kujengwa au yenye miradi ya maji na usafi wa mazingira ili kuwezesha usanifu wa miundo mbinu miradi;

Kupima uwekaji wa vifaa vya miundo mbinu kwenye ardhi wakati wa ujenzi wa miradi ya maji na usafi wa mazingira;

Kunakili na kutunza taarifa za upimaji wa ardhi kwa ajili ya miundo mbinu ya miradi ya maji na usafi wa mazingira kwa namna inayokubalika kwa mchoraji wa ramani za usanifu wa miradi kufanya kazi yake kwa unadhifu;kuchora ramani za maeneo ya miradi ya maji na usafi wa mazingira kwa namna zote zinazokubalika kwa ajili ya kuwezesha usanifu wa miundo mbinu ya maji na usafi wa mazingira;

Kumsaidia Fundi Sanifu katika kazi za upimaji ardhi.

2.2 SIFA ZA MWOMBAJI

• Kuajiriwa wahitimu wa kidato cha nne waliohudhuria na kufaulu mafunzo ya mwaka mmoja kutoka Chuo cha Maji au Chuo chochote kinachitambuliwa na Serikali ambao wana Cheti cha ufundi Daraja III (Water Works Technician Geometric).

2.3 MSHAHARA

•  Kwa kuzingatia Ngazi za mishahara ya Serikali yaani TGS A kwa mwezi.

NB: MASHARITI YA JUMLA KWA KAZI ZOTE.

i.       Waombaji wote wawe ni Raia wa Tanzania na wenye umri usiozidi miaka 45

ii.       Waombaji wote waambatishe cheti cha kuzaliwa.

iii.      Waombaji ambao tayari ni watumishi wa Umma na wamejipatia sifa za kuingilia katika kada tofauti na walizonazo, wapitishe barua zao za maombi ya nafasi za kazi kwa waajiri wao na Waajiri wajiridhishe ipasavyo.

iv.       Nafasi ya kazi inayoombwa iandikwe juu ya bahasha, kutozingatiwa hili kutasababisha maombi ya kazi kuwa batili.

v.       Waombaji  waambatishe  maelezo  binafsi  yanayojitosheleza  (Detailed C.V)  yenye

anwani na namba za simu za kuaminika pamoja na majina ya wadhamini (referees) watatu wa kuaminika.

vi.    Maombi yote yaambatane na vyeti vya taaluma, maelezo, nakala za vyeti vya kidato cha nne na kidato cha sita kwa wale waliofikia kiwango hicho na vyeti vya kuhitimu


mafunzo mbalimbali kwa kuzingatia sifa za kazi husika. Viambatanisho hivyo vibanwe sawa sawa kuondoa uwezekano wa kudondoka au kupotea.

-       Postgraduate/Degree/Advanced Diploma/Diploma/Certificates.

-       Cheti cha mtihani wa kidato cha IV na VI

-       Computer Certificate

-       Vyeti vya kitaaluma (Professional certificates from respective boards) 

-       Picha moja "Passport size" ya hivi karibuni iandikwe jina kwa nyuma. 

vii.       Testmonials", "Provisional Results", "Statement of results", hati matokeo za kidato cha nne na sita (FORM IV AND FORM VI RESULTS SLIPS) HAVITAKUBALIWA. 

viii.       Waombaji waliosoma nje ya Tanzania wahakikishe vyeti vyao vimehakikiwa na kuidhinishwa na Mamlaka husika (TCU na NECTA).

ix.       Waombaji waliostaafishwa katika Utumishi wa Umma hawaruhusiwi kuomba isipokuwa kama wanakibali cha Katibu Mkuu Kiongozi.

x.       Waombaji kazi ambao tayari ni waajiriwa katika nafasi za kuingilia walioko katika Utumishi wa umma wasiombe na wanatakiwa kuzingatia maelekezo yaliyo katika Waraka Na CAC. 45/257/01/D/140 wa tarehe 30 Novemba 2010.

xi.       Uwasilishaji wa taarifa na sifa za kugushi wahusika watachukuliwa hatua za kisheria.

xii.       Mwisho wa kupokea barua za maombi ni tarehe 18 Januari, 2015

xiii.      Aidha, uwasilishaji wa barua kwa mkono katika ofisi za Sekretarieti ya ajira HAURUHUSIWI.

xiv.       Maombi yanaweza kuandikwa kwa Lugha ya Kiswahili au Kiingereza na yatumwe kupitia posta kwa anuani ifuatayo.



Katibu,
AU
Secretary,
Sekretariati ya Ajira katika

Public Service Recruitment
Utumishi wa Umma,

Secretariat,
SLP.63100,

P.O.Box 63100
Dar es Salaam.

Dar es Salaam.


0 comments:

Post a Comment