Wednesday, December 3, 2014

KATIBU MAHSUSI III (NAFASI 7)


KATIBU MAHSUSI III (NAFASI 7)

KATIBU MAHSUSI III (NAFASI 7) 

MAJUKUMU YA KAZI:
Kuchapa barua, taarifa na nyaraka za kawaida.
Kusaidia kupokea wageni na kuwasaili shida zao na kuwaelekeza
sehemu wanapoweza kushughulikiwa.
Kusaidia kutunza kumbukumbu/taarifa za matukio, mihadi,
wageni, tarehe za vikao, safari za Mkuu wake na ratiba ya kazi
zingine zilizopangwa kutekelezwa katika ofisi anamofanyia kazi
na kumuarifu Mkuu wake kwa wakati unaohitajika.
Kusaidia kutafuta na kumpatia Mkuu wake majalada, nyaraka
au kitu chochote kinachohitajika katika shughuli za kazi hapo
ofisini.
Kusaidia kufikisha maelekezo ya Mkuu wake wa kazi kwa
wasaidizi wake na pia kumuarifu kuhusu tarifa zozote anazokuwa
amepewa na wasaidizi hao.
Kusaidia kupokea majalada, kuyagawa kwa Maofisa walio katika
sehemu alipo, na kuyakusanya,kuyatunza na kuyarudisha
sehemu zinazohusika.
Kutekeleza kazi zozote atakazokuwa amepangiwa na Msimamizi
wake wa kazi.

SIFA ZA MWOMBAJI
Kuajiriwa Wahitimu wa kidato cha IV waliohudhuria mafunzo ya
Uhazili na kufaulu mtihani wa Hatua ya Tatu. Wawe wamefaulu
somo la Hati mkato ya Kiswahili na Kiinqereza maneno 80 kwa
dakika moja na wawe wamepata mafunzo ya Kompyuta kutoka
kutoka chuo chochote kinachotambuliwa na Serikali na kupata
cheti katika program za Window, Microsoft Office, Internet, E-mail na Publisher.
MSHAHARA
Kwa kuzingatia Ngazi za mishahara ya Serikali yaani TGS.B kwa mwezi.


MASHART YA JUMLA KWA KAZI ZOTE:
1.    Waoombaji weote wawe raia wa Tanzania wenye umri usiozidi miaka 45.
2.    Waombaji ambao tayari ni watumishi wa umma na wamejipatia sifa katika kada tofauti walizo nazo wapitishe barua zao za maombi ya nafasi za kazi kwa waajiri wao na waajiri wajiridhishe ipasavyo.
3.    Nafasi ya kazi inayoombwa iandikwe juu ya bahasha; kuto kuzingatia hili kutasababisha maombi kuwa batili.
4.    Waombaji waambatanishe maelezo binafsi yanayojitoshereza (detailed CV) yenye anuani na namba za simu zaza kuaminika pamoja na majina ya wadhamini (referees) watatu wa kuaminika.
5.    Maombi yaambatane na nakala za vyeti vya taaluma, maelezo ,vyeti vya kidato cha nne au cha sita kwa wale waliofika kiwango hicho, vyeti vya kuzaliwa na vya kuhitimu mafunzo mbalimbali kwa kuzingatia sifa za kazi husika. Viambatanisho hivyo vibanwe sawa sawa kuondoa uwezekano wadondoka au kupotea. Astashahada/ stashahada/cheti, cheti za mitihani ya kidato cha IV NA VI, cheti cha kompyuta, picha moja ya "passport size" ya hivi karibuni iandikwe jina kwa nyuma.
6.     Testimonials "provisional result" statement of result hati ya matokeo ya kidato cha nne na sita (FORM IV AND VI RESULTS SLIPS) havitakubaliwa.
7.    Waombaji waombaji waliostaafishwa katika utumishi wa umma hawaruhusiwi kuomba isipokuwa kama wanakibari cha katibu mkuu kiongozi.
8.    Uwasilihaji wa taalifa na sifa za kugushi wahsika watachukuliwa hatua za kisheria.
9.     Mwiisho wa kupokea  barua za maombi ni tarehe 16 desemba 2014.
Maombi yanaweza kuandikwa kwa lugha ya Kiswahili au kiingereza na yatumwe kupitia posta kwa anuani ifuatayo:- Mkurugenzi Mtendaji, 
Halmashauri ya Wilaya, Au
S.L.P.52,
Mkuu-Rombo.
District Executive Director,
Rombo District Council,
P.O. Box 52,
Mkuu-Rombo


0 comments:

Post a Comment