Tuesday, December 30, 2014

AFISA MTENDAJI KIJIJI DARAJA LA III (NAFASI 32)



AFISA MTENDAJI KIJIJI DARAJA LA III (NAFASI 32)
HALMASHAURI YA WILAYA YA ULANGA
TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI
Mkurugenzi Mtendaji (W) Ulanga anawatangazia wananchi wote walio na sifa kwamba  nafasi za kazi kama zifuatavyo
AFISA MTENDAJI KIJIJI DARAJA LA III (NAFASI 32)
SIFA
•    kuajiriwa kidato cha Nne au sita na kuendelea na kuhitimu mafunzo ya stashahada/Cheti katika moja ya fani zifuatazo; Utawala, sheria, Elimu ya Jamii na Maendeleo ya jamii kutoka Chuo chochote kinachotambuliwa na serikali
KAZI ZA KUFANYA
•    kusimamia ulinzi na usalama wa raia katika eneo lake
•    katibu wa mikutano yote ya Halmashauri ya Kijiji
•    kuandaa taarifa ya utekelezaji na kuwasilisha
•    afisa Masuuli na Mtendaji Mkuu wa serilkali ya Kijiji
MSHAHARA; kiwango cha mshahara ni ngazi ya TGS.B yaani 345,000/= kwa mwezi
MASHARTI YA JUMLA YA WAOMBAJI
•    Awe ni raia wa Tanzania
•    Awe na umri wa miaka 18-41
•    Awe hajawahi kuhukumiwa na kufungwa/kukabiliwa na kosa la jinai au kufukuzwa kazi.
•    Watumishi wa umma walioajiliwa hawapaswi kuomba
•    Maombi yote yaandikwe kwa mkono na kuambatanisha makala za vyeti vya Shule na taaluma, passport size mbili (2)
•    CV
Mwisho wa kutuma maombi ni tarehe 15/01/2015 saa 9:30 Alasiri na maombi yote yatumwe kwa anwani
MKURUGENZI MTENDAJI (W)
S.L.P 22
MAHENGE/ULANGA


0 comments:

Post a Comment