Tuesday, November 25, 2014

TAARIFA TOKA UHAMIAJI - 11/25/2014




TAARIFA TOKA UHAMIAJI - 11/25/2014
KUITWA MAFUNZONI
Kamishna Mkuu wa Idara ya Uhamiaji anawatangazia wote waliofaulu usaili wa nafasi ya Mkaguzi Msaidizi wa Uhamiaji na kutangazwa kupitia tovuti ya Idara ya Uhamiaji, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi pamoja na Gazeti la Dailynews la Tarehe 14 Julai, 2014 kuwa wanatakiwa kuripoti Kitengo cha Utumishi Makao Makuu ya Idara ya Uhamiaji, mtaa wa Loliondo Kurasini Dar es salaam tarehe 27 Novemba, 2014 saa mbili asubuhi kwa ajili ya safari ya kwenda Mafunzoni Chuo cha Polisi Moshi.
Atakayesoma tangazo hili amjulishe na mwingine.

TANGAZO HILI LIMETOLEWA NA
KAMISHNA MKUU WA UHAMIAJI 
WALIOFAULU USAILI WA NAFASI 228 ZA
KONSTEBO NA KOPLO WA UHAMIAJI
Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi inawatangazia wale wote waliofaulu usaili wa nafasi 228 za Konstebo na Koplo wa Uhamiaji kuripoti Makao Makuu ya Idara ya Uhamiaji, Mtaa wa Loliondo, Kurasini - Dar es Salaam, tarehe 1 Desemba, 2014, siku ya Jumatatu, saa 2:00 asubuhi kwa ajili ya maelekezo zaidi. Aidha, wanatakiwa kwenda wakiwa na vyeti halisi vya masomo / mafunzo, cheti halisi cha kuzaliwa na picha mbili za rangi (passport size). orodha imeambatanishwa



0 comments:

Post a Comment